Alama za wanyama na ndege kwenye nembo za mataifa zina tafsiri yake

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Ama kwa kujuwa au kutokujuwa, alama za wanyama kwenye nembo za mataifa duniani zina maana zake zinazobeba hatma za mataifa hayo ama kisiasa, kiuchumi, kijamii au kiulinzi kutegemea tabia za mnyama au ndege husika.

Uchaguzi wa mnyama au ndege yupi awekwe kwenye nembo ya taifa au atambulike kama alama ya taifa ni mchakato unaohitaji umakini mkubwa kutokana na kwamba unahusu hatma ya taifa husika.

Wengi siri hii hatuijui na inabaki kuwa siri na nguvu ya waasisi wa taifa husika. Hii pia huendana na rangi rasmi ya taifa. Maendeleo ya nchi, falsafa ya nchi, nguvu ya nchi, utangamano wa nchi nk hutegemea alama hizi.

Ufukuaji huu wa siri hii na maarifa haya visivyowekwa wazi sana utazifaa vizazi vipya vya mataifa husika ambavyo havijui misingi ya nchi zao ilivyoasisiwa na kuathiri maisha na hatma zao ama kwa namna ambayo ni chanya au hasi. Hii siyo ramli bali empirical fact (ukweli wa dhahiri). Ebu tuone mifano michache kama vielelezo:

1. Marekani hutumia Tai mwenye upara (Bald Eagle). Tai ni mnyama mwenye nguvu (USA), kuna aina ya tai anayeweza hata kumnyakua binadamu, Tai ni mporaji (USA dhidi ya rasilimali za dunia, inamiliki 15.54% ya GDP ya dunia), Tai anapaa mbali angani (USA ni ya 2 kwenda anga za mbali), Tai anashirikiana na fisi na mbweha kushambulia mawindo (USA na NATO), Tai anategemewa na fisi kuwinda kwa kuangalia mwelekeo wake angani (USA na washirika wake).

2. Urusi inatumia pia Tai lakini mwenye vichwa viwili (Two headed eagle) inamaanisha Urusi ni transcontinental country (nchi inayopatikana mabara 2 kama ilivyo Misri. Urusi iko Asia kwa 77% na Ulaya 23%). Aidha, tabia za Tai za USA ziko pia Urusi ambayo ni nchi ya kwanza kwenda anga za mbali.

3. Israel, bendera yake ina nyota (ile ni ishara ya nyota ya Mfalme Daudi), pia Daudi alikuwa jemedari hodari wa vita hata dhidi ya jitu Goliath. Daudi alipigana vita 9 na kushinda vyote. Hii ni tabia ya Israel ambayo iko vitani kwa miaka 75 tangu uhuru wake.

Nembo ya Israel ina Simba ambayo hii huashiria nguvu na ubabe kama ilivyo nembo ya Kenya pia ambako watu wake ni majasiri na wanaopenda makabiliano na kutopenda zaidi njia ya maridhiano. Yesu alipewa jina la Simba wa kabila la Yuda.

Aidha, nembo ya Israel ina alama ya wanawake 2, mwanamke ni ishara ya malezi na jeshi kubwa, Tz (ambayo pia ina bibi kwenye ngao ya taifa) na Israel zina nguvu za kijeshi kwenye kanda zao na zimelea mataifa, Tz ikifanya ukombozi na malezi Kusini mwa Afrika.

Enzi ya utawala wa Mwl Nyerere wakati wa vita ya Kagera, Urusi iliwahi kusema Tz inaweza kuisumbua kwenye medani kiakili na siyo kisilaha. Kijeshi vita ni matumizi ya akili zaidi ya silaha (ambazo unaweza kutekwa nazo), Tz ilishinda vita ya Kagera kwa kutumia akili (maana haikuwa na uchumi wa vita) ambapo ilitumia mkakati wa kuteka zana za adui na kumpiga nazo.

Aidha, Twiga ni mnyama anayeona mbali na wanyama wenzake humtegemea na kuchunga naye karibu ili awasaidie kuona mbali kulee... Tz iliona mbali na kuasisi ukombozi Kusini mwa Afrika, kuasisi Umoja wa kutofungamana na upande wowote kwenye vita baridi, kuasisi SADC, EAC, kuipigania China ipewe mamlaka/kura ya Veto kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nk nk nk.

4. Uganda inatumia alama ya Korongo ambaye ni ndege asiyechangamana kirahisi na ndege wenzake. Uganda wana shida ya utengano (hawachangamani). Nchi imekuwa na marais 9 hadi sasa. Sir Edward Mutesa II – 1962 – 1966
Apollo Milton Obote (Obote I) – 1966 – 1971
Idi Amin Dada – 1971 – 1979
Yusuf Kironde Lule – 13 April 1979 – 20 June 1979
Godfrey Lukongwa Binaisa – 1979 – 1980
Paul Muwanga – 12 May 1980 – 22 May 1980
Apollo Milton Obote (Obote II) – 1980 – 1985
Tito Okello Lutwa – 1985 – 1986
Yoweri Kaguta Museveni – 1986 to date.

Nigeria pia ina Tai. Nigeria inaunda ndegevita yenyewe, ina makabiano ya wenyewe kwa wenyewe, ni majasiri. Pia Nigeria ina alama ya Farasi wawili, mnyama ambaye anabeba watu na hutumika kwenye vikosi, zamani Farasi walitumika kwenye medani. Barani Afrika Nigeria inatubeba kwenye vitu vingi kwenye medani za kimataifa/duniani kama soccer, ajira za diaspora, lakini Wanigeria wako juu yetu Afrika kwa viwango vya kukosa uaminifu nk

Nitaiendeleza kesho panapo nafasi.
 
You are talking!
Nigeria pia ina Tai. Nigeria inaunda ndegevita yenyewe, ina makabiano ya wenyewe kwa wenyewe, ni majasiri. Pia Nigeria ina alama ya Farasi wawili, mnyama ambaye anabeba watu na hutumika kwenye vikosi, zamani Farasi walitumika kwenye medani. Barani Afrika Nigeria inatubeba kwenye vitu vingi kwenye medani za kimataifa/duniani kama soccer, ajira za diaspora, lakini Wanigeria wako juu yetu Afrika kwa viwango vya kukosa uaminifu nk
 
Back
Top Bottom