Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Asanteni sana Tized na christine ibrahim kwa mifano hai yenye mafunzo mazuri,na poleni kwa yote mliyoyapitia,pamoja na yote Utukufu kwa Mungu aliyeweza watetea na kuwasimamisha na mpaka leo tunajifunza kitu kupitia ninyi. Mbarikiwe sana.
 
Last edited by a moderator:
Ebana point ya msingi ni msamaha ila hii kali mtu yupo kitaa hana experience halafu anapata ukurugenzi hii ni noma...sound zingine ni noma aisee...
 
Hongera sana.. Mungu kakuinua ili uwe mfano na uiponye familia yako. Usiipoteze hio nafasi yako.
Mungu hutumia vinavyoonekana vinyonge kuviabisha vinavyoonekana vina nguvu. Hongera sana, Kumbuka Endelea KUUSHINDA UBAYA KWA WEMA na utazidi kubarikiwa. Kumbuka kadiri unavyofanyika msaada kwa wengine, Mungu ataendelea kukufungulia mianya na fursa mbali mbali ili kupitia wewe Yeye akajitwalie utukufu zaidi.

Wakati mwingine ni spirits zinawavaa hawa wandugu... ukimhukumu yeye ni kumuonea pasipo kujua (uchukie uovu lakini mpende muovu ili akabadilike kwa upendo wako).... Siku zote ukitaka kubaki salama BAKI KWENYE NDOA YAKO.

 
Ebana point ya msingi ni msamaha ila hii kali mtu yupo kitaa hana experience halafu anapata ukurugenzi hii ni noma...sound zingine ni noma aisee...

Mungu akikupa kibali hakuna lililo gumu,kama wewe ni mkristo rejea hadithi ya Yusufu na Daudi.
 
Yaani NANDERA nilikuwa sijamuwaza lakini baada ya hii thread ndio nimekumbuka haya .Ukiangalia waliyopitia wengine mimi najionaga nna neema sana ndiyo maana hata siyawazi hayo

Nakuelewa sana bibie. Hata mimi sikuwahi kumpa uzito, wala sina mpango wa kumfata ingawa najua aliko, ila kinyongo/hasira juu yake imeisha. Mambo ya kutetemeka kwa hasira nikiona simu yake au mtu akiniuliza kuhusu yeye yamenitoka. Ningeweza kupata kiharusi buree. Hata yeye akinipigia simu huwa hasemi chochote zaidi ya salamu. Naamini hata kwa hilo anashukuru. Baada ya kumsamehe ndo nilipata hata muda wa kutafakari nikagundua ni afadhali sana alivyojimuvuzisha maana sijui ningekuwa Nandera wa aina gani mimi. Ni hakika kuwa nisingekuwa bora zaidi ya nilivyo sasa. Huwa siishi kumshukuru Mungu kwa kunipitisha kwenye mikono ya babu, bibi na mama yangu. Hata katika mahangaiko yao ya kunifanya niwe mtu katika watu nimejifunza sana. Badala ya kuangalia mahangaiko yao kama sababu ya kumlaumu baba, mimi nayaangalia kama fursa pekee iliyonifundisha maana halisi ya upendo, maana ya kujitoa kwa ajili ya mtu mwingine na vingine vingi sana. Vipo vichache nilivyovikosa kwa kuondoka kwake lakini ni minor sana. Havilingani na neema niliyopata. Kwa hiyo naamini ilikuwa aondoke ili mimi niwe kile Mungu alichotaka niwe.

Mjomba wangu mmoja alifariki nikasikitika sana. kabla ya kifo alikuwa na watoto wake 4 na mke. Walikuwa hawana maelewano, hawana muda na watoto, watoto wanazurura hovyo tu, mara watoro shuleni, mara wadokozi. Hakuna mtu aliyekuwa anaingilia kati kwa sababu wazazi wao walikuwepo. Alivyokufa yule mjomba ndugu wakagawana watoto kuwatunza. Sasa hivi wale watoto wako mbali sana, wamekuwa raia wema wa kutegemewa. Baba yao angekuwepo wangekuwa mateja na wezi. Huwa nikiwaangalia sisikitiki kufa kwa baba yao. Huwa nasema Mungu alimuondoa ili wale watoto wapone. Kwa hiyo si kila jambo baya ila lengo baya.
 
Wonderful and interesting story
like, like, like, ....,....,....,....,..................
 
everlenk haya mambo ni mazito sana na sometimes ni yakuacha tu moyo wa mtu uamue.
Nina hasira na machungu juu bora huyo ambaye mkosaji wake kalitambua kosa na kukiri.

mmmmh! jaribu kushare na watu. unaweza ukapata relief kidogo. sio wote tuna uwezo wa kusamehe waliotukosea ila kama huwez kusamehe puuzia tu.
 
Last edited by a moderator:
Wala sijitesi mkuu......ni uamuzi tu. Vile tu hujaujua uzito wa jambo pamoja na wahusika wenyewe as to till now bado wanafanya nini... .ila si rahisi kama unavyofikiria.

 
mmmmh! jaribu kushare na watu. unaweza ukapata relief kidogo. sio wote tuna uwezo wa kusamehe waliotukosea ila kama huwez kusamehe puuzia tu.

Naanzaje sasa kuwapuuzia?
Kwa huu uchungu nilionao?
Hili somo gumu kwangu!

Anyways.....si vyote vya kushare on public.
 

Na wakifa bila kuonyesha nia ya kuomba msamaha utafanyaje? Lakini pole sana kwa yote yaliyo kukuta na kukutesa. Lakini unahitaji kua huru, unajua watu wengine huwa hawatambui makosa yao hata ukiwaambia. Lakini unahitaji kua huru Dada yangu, kumbuka wewe ni bora kuliko wao.
 
Last edited by a moderator:
Thanks NANDERA.

Wasipokuelewa bado kutakua na shida nyingine zaidi ya hii tunayoiadress hapa. Nimejifunz mengi kutoka kwako kwenye huu uzi.

Godbless.
 
Last edited by a moderator:
Wala sijitesi mkuu......ni uamuzi tu. Vile tu hujaujua uzito wa jambo pamoja na wahusika wenyewe as to till now bado wanafanya nini... .ila si rahisi kama unavyofikiria.

Kuwasamehe mimi ni mpaka waoneshe nia otherwise hasira yangu bado i juu yao!

Mkuu hawa watu mpaka niwapitishe na wao kwenye maumivu ndo roho yangu iridhike.
Avemaria mpenzi yaani hiyo hasira na uchungu ulionao ndo mateso yenyewe,wewe waweza kuona kama hujitesi lakini unateseka sana,embu achia hili jambo tangaza msamaha,embu chukua hatua kama Tized alivyosema chagua njia yoyote ambayo utaona yafaa.

Jambo la pili muhimu kamwe kamwe usijiingize kwenye swala la kulipiza kisasi utajiingiza kwenye shida kuu na matatizo mengi,Mungu kasema kisasi ni chake na yeye ni Bwana wa vita,embu liachie jambo hili uone jinsi Mungu atakavyokupigania. Mwachie Mungu yeye ndo muhukumu wa wote.
 
Last edited by a moderator:

Asante sana NANDERA kwa mifano yako hai yenye kufundisha,hakika atukuzwe Mungu aliyekuwezesha kusimama mpaka leo hii azidi kukubariki zaid na zaid,nami naendelea kujifunza kitu hapa hakika MAJARIBU NI MTAJI.
 
Last edited by a moderator:
huo ndo mpango mzima. fanya yako, usamehe ili iweje!!!

Hapana Husninyo msamaha ni lazima,asiposamehe sana sana anazidi kukaa kwenye uchungu wenye hasira na chuki na wala hamna faida anayopata ila ipo faida katika kusamehe,siku atakayoamua kuachilia hata yeye mwenyewe nafsini mwake atajiona ni wa tofauti.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…