Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

everlenk

msamaha ndo kila kitu....!

nikitafakar huwa naishia kufuta machozi...! kuna nguvu kubwa sana ktk msamaha!
mimi nilibakwa na kijana ambaye familia zetu zilikuwa karibu sana..! akakimbia, wakamshaur aje aombe msamaha kifamilia, akakataa, lakn niliwambia mimi nimemsamehe mbele ya wazazi wake na wangu...!

huu ni mwaka wa kumi na mbili sasa, hana analofanya likafanikiwa, had nasikia kawa mlinzi nyumban kwa mtu ( ana degree kabisa), wazazi wake walishawah kuja na kusema nimsamee, nikawaambia nishasamehe since ni yeye tu kutubu kwa Mungu wake.

lakn mi nina maisha yangu familia yenye furaha na amani.
had mme wangu anamuonea huruma.
 
Last edited by a moderator:
HALELUYA MOSHI

Duh!! Pole sana ndugu HALELUYA MOSHI na hongera sana kwa moyo huo, Aisee huu ushuhuda wako umenifurahisha na kuniogopesha pia,loh! Mungu ampe ufahamu ajitambue....hakika kisasi ni cha Muumba.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Avemaria kwa ulivyoumizwa lakini pamoja na yote inabidi utangaze msamaha,kusamehe si rahisi ila inawezekana,fikiria huyu rafiki yetu alibakwa na baba yake mzazi aisee ni jambo linaloumiza sana....samehe hata Baba wa mbinguni atakusamehe wewe makosa yako....

everlenk haya mambo ni mazito sana na sometimes ni yakuacha tu moyo wa mtu uamue.
Nina hasira na machungu juu bora huyo ambaye mkosaji wake kalitambua kosa na kukiri.
 
Last edited by a moderator:
jamani sijui kama nitaweza kuja kumsamehe my x kwa moyo mmoja kabisa???? Cjui aisee najitahidi sana bt najikuta nafikilia aliyonitendea najikuta hasira inaongezeka x100 mungu anisaidie kwa hili.

msamaha pia ni tiba ya maradhi mbalimbali
 
Unamsamehe mtu ambaye nae anaonesha nia ya ndani kabisa ya kutaka msamaha kama hata kuomba msamaha haombia au hata kujiweka katika namna ambayo wewe unaona huyu mtu anajutia kitendo alichokifanya hafanyi aunaanzaje kutoa msamaha .
Mimi binafsi Mungu anisaidie tuu maana na mzazi wangu wa kiume hata pua yake siijui sasa unaanzaje kusamehe mtu ambaye unajua yupo lakini hajaona umuhimu hata wa kukutafuta
Mungu ni mwema ananibariki nami naona baraka zake kwakweli.
 
Pole sana Gemmy ila pamoja na yote kanuni kubwa ya msamaha ni kutoa msamaha hata kabla hujaombwa,samehe tu hata kama muhusika hajitambui,zipo baraka tele za msamaha si za kiuchumi tu,embu msome hapo juu mwenzetu HALELUYA MOSHI alichokifanya alitoa msamaha hata kabla hajaombwa.
 
Mungu anisaidie tuu kwakweli maana mmgh!
 
Hongera sana na endelea na moyo huo huo.

Mda mwingine ni ngumu sana kusamehe, nilishawahi kukaa na kinyongo kwa miaka mitatu mfululizo, rafiki yangu niliyemwamini na kumpa siri zangu alinijeruhi sana, kila nikimuona moyo unadunda sana na kukosa amani, kuna siku nikaja kusoma kitabu kimoja ivi kinaitwa MOYO ULIOJERUHIWA, kile kitabu kilinisaidia sana , nikawa nasoma uku nalia kwa uchungu, karibia kila kitu kilichokuwa kikiongelewa kwenye kitabu kilinihusu mimi na maisha yangu, kile kitabu kilibadilisha maisha yangu, toka siku hyo nilimsamehe rafiki yangu nikaachia machungu yote na kuishi kwa amani, nimemsamehe na kovu limeshaisha kwa msaada wa mungu, maana peke yangu ningeshindwa , alinifanyia mambo magumu sana, ila mungu alinisaidia😭😭
 
Mungu anisaidie tuu kwakweli maana mmgh!

Ameen,atakuwezesha tu,si kitendo cha haraka ila kinakuja taratibu,badilisha mtizamo wako ule uovu alioutenda uweke pembeni,anza kumuona kama mzazi,mtu anayehitajika kupendwa na kusamehewa,uchungu ulionao juu yake anza kuuachia achia tunda la amani listawi moyoni mwako. Mungu mfalme wa amani akuwezeshe kwenye hili.
 
Sijui kwa nini, ila story yako imenipa bonge la simanzi...i just feel bad, I might have wronged a few people na wala sikumbuki, au niliona ni kawaida.
 
Mda mwingine ni ngumu sana kusamehe, nilishawahi kukaa na kinyongo kwa miaka mitatu mfululizo, rafiki yangu niliyemwamini na kumpa siri zangu alinijeruhi sana, kila nikimuona moyo unadunda sana na kukosa amani, kuna siku nikaja kusoma kitabu kimoja ivi kinaitwa MOYO ULIOJERUHIWA, kile kitabu kilinisaidia sana , nikawa nasoma uku nalia kwa uchungu, karibia kila kitu kilichokuwa kikiongelewa kwenye kitabu kilinihusu mimi na maisha yangu, kile kitabu kilibadilisha maisha yangu, toka siku hyo nilimsamehe rafiki yangu nikaachia machungu yote na kuishi kwa amani, nimemsamehe na kovu limeshaisha kwa msaada wa mungu, maana peke yangu ningeshindwa , alinifanyia mambo magumu sana, ila mungu alinisaidia����

Kweli kabisa kusamehe si kazi rahisi inahitaji moyo mkuu,inauma sana hasa pale unakuta mtu kakukosea na bado anaendelea kukuonyesha jeuri inaumiza mno,ila ukijifunza kuachilia unakuwa mtu mwenye furaha na amani mno,mimi binafsi hili limenisaidia sana katika maisha yangu ya ndoa,huwa natangaza msamaha hata kabla sijaombwa,najitahidi sana kumaliza tofauti inayojitokeza kabla jua halijazama,kinyongo huwa kinanitesa sana huwa siwezi hata kufanya kazi zangu ninapokuwa sina amani na mtu. Dhamira yangu huwa inanishitaki sana je mimi nmemkosea Mungu mangapi mpaka na mimi nisisamehe?
 
Sijui kwa nini, ila story yako imenipa bonge la simanzi...i just feel bad, I might have wronged a few people na wala sikumbuki, au niliona ni kawaida.

Pole sana,kama uko nao karibu ni vyema ukatangaza msamaha,kama wako mbali basi wasamehe tu na Muombe Mungu rehema juu ya hilo. Kama ni wewe uliwakosea waombe msamaha kama hawako tena Muombe Mungu juu ya hilo akusamehe.
 
Kweli kabisa kusamehe si kazi rahisi inahitaji moyo mkuu,inauma sana hasa pale unakuta mtu kakukosea na bado anaendelea kukuonyesha jeuri inaumiza mno,ila ukijifunza kuachilia unakuwa mtu mwenye furaha na amani mno,mimi binafsi hili limenisaidia sana katika maisha yangu ya ndoa,huwa natangaza msamaha hata kabla sijaombwa,najitahidi sana kumaliza tofauti inayojitokeza kabla jua halijazama,kinyongo huwa kinanitesa sana huwa siwezi hata kufanya kazi zangu ninapokuwa sina amani na mtu. Dhamira yangu huwa inanishitaki sana je mimi nmemkosea Mungu mangapi mpaka na mimi nisisamehe?

pia namshukuru mungu roho ya kisasi sina kabisa, nitendee ubaya wote kama ukipata tatizo nakusaidia tena kwa moyo mmoja, watu wananishangaaga sana maana mtu anaweza kunitukana matusi mazito ila ikitokea akawa na tatizo namsaidia tu kiroho safi, nikifanya wema kwa adui yangu uwa najisikia amani kwangu.

Nilifundishwaga siku moja, silaha kubwa dhidi ya adui yako ni kumtendea wema tu na sio kushindana nae, kutenda mema kwa maadui ni KISASI tosha
 
Kama maneno yote haya ni ya kweli, na msamaha una baraka zooote hizi, Hivi kwa nyinyi mlio kimyume na rasimu ya katiba iliyopitishwa "kidijitali" pale bungeni hivi karibuni, mko tayari kuwasamehe akina sita na timu yake kwa ajili ya kupata "mijibaraka" kama ya mwenzetu??

Nawaza tu kipuuzi puuzi, msinikasirikie, ikiend imeshaanza...!!!!
 
pia namshukuru mungu roho ya kisasi sina kabisa, nitendee ubaya wote kama ukipata tatizo nakusaidia tena kwa moyo mmoja, watu wananishangaaga sana maana mtu anaweza kunitukana matusi mazito ila ikitokea akawa na tatizo namsaidia tu kiroho safi, nikifanya wema kwa adui yangu uwa najisikia amani kwangu.

Nilifundishwaga siku moja, silaha kubwa dhidi ya adui yako ni kumtendea wema tu na sio kushindana nae, kutenda mema kwa maadui ni KISASI tosha

Haswaa tena ukitenda mema kwa adui yako unapalia makaa kichwani pake.
 
Back
Top Bottom