Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Mmmmh......niseme tu nashukuru kwa ushauri japo hilo somo bado ni gumu na sina utayari nalo!

Avemaria mpenzi yaani hiyo hasira na uchungu ulionao ndo mateso yenyewe,wewe waweza kuona kama hujitesi lakini unateseka sana,embu achia hili jambo tangaza msamaha,embu chukua hatua kama Tized alivyosema chagua njia yoyote ambayo utaona yafaa.

Jambo la pili muhimu kamwe kamwe usijiingize kwenye swala la kulipiza kisasi utajiingiza kwenye shida kuu na matatizo mengi,Mungu kasema kisasi ni chake na yeye ni Bwana wa vita,embu liachie jambo hili uone jinsi Mungu atakavyokupigania. Mwachie Mungu yeye ndo muhukumu wa wote.
 
Last edited by a moderator:
Stori za shigongo mshazibadili zenu.... siamin kama mtu na masterz bila experience anaweza anza kuwa mkurugenzi... nirudishie chenji plzzz
 
Mmmmh......niseme tu nashukuru kwa ushauri japo hilo somo bado ni gumu na sina utayari nalo!

Si lazima sasahivi lakini jipe muda kidogo,mwambie Mungu peke yangu siwezi naomba uniwezeshe katika hili.
 
Stori za shigongo mshazibadili zenu.... siamin kama mtu na masterz bila experience anaweza anza kuwa mkurugenzi... nirudishie chenji plzzz

Eti ndani ya miezi 6 ya kazi kajenga ghorofa. Atakuwa analipwa shingapi kwa mwezi duh!!..Akuzidishie chenji huyo
 
kwel mkuu tunaambiwa forgive and forget
 
Unajua Mapenzi ni kitu flani ambacho ni kigumu sana kudeal nacho.

Kwenye thread iliyopita yale watu waliocomment ,
kwa kiasi kikubwa ndio uhalisia wa jinsi watu wanavyoyatatua matatizo yao,

Niseme tu leo nimejaribu kumalizia utafiti nilioufanya kuanzia mitaani mpaka kwenye mitandao ya kijamii (ikihusisha familia,marafiki na wapenzi),

Nimegundua ukweli mchungu sana ambao wanaume lazima tukubaliane nao tu.

Kusema kweli wanaume bado tupo nyuma sana kwenye suala la kuyafanyia utabibu na kuyaponya mahusiano yetu yaliyovunjika(au yanayosuasua)

Na ndomana unakuta mwanamke akikukosea ni rahisi sana mahusiano yenu kurudi kwenye mstari kwasababu ni wepesi wa kutaka usuluhisho
lakini sisi vidume vya mbegu ndio tunajifanya kukaza usoni lakini moyoni tunateketea zaidi ya moto wa mabua!

Jambo hilo ni baya sana kwa afya kwasababu inasababisha wanaume tunaishi maisha mafupi sana.

Sijui kwa upande wa wanawake wanalichukuliaje hili suala ila

Naomba nieleweke kwamba hapa sizungumzii 'manungayembe' bali nazungumzia yale mahusiano yaliyokuwa serious au wale walio ndoani.

Hebu tuambie wewe kwa upande wako unalichukuliaje suala la kuomba msamaha kuanzia kwenye ngazi ya familia, marafiki mpaka kwa wapenzi.

'Je, ni watu gani ambao hutokuja kuwaomba msamaha?'
 
mimi Kwa upande wangu nadhani kuomba msamaha sio kigezo cha udhaifu kwa mwanaume,
bali ni hatua moja wapo ya kulilinda penzi lenu,
tena hasahasa kwenye mahusiano machanga ambayo yanachipukia,
Sema katika jamii zetu watu wanachukulia kwa mawazo hasi,...
Alafu hiki kitu cha kuomba msamaha pia inategemea na mahusiano na mahusiano,
mfano kuna yale mahusiano hit&run,
au yale ambayo watu hawana malengo ya kudumu muda mrefu sasa nadhani mahusiano ya namna hiyo hayana hata haja ya kuombana msamaha, labda itokee tu.
 
Kuomba msamaha ni jambo la heri kbs ila shida Moja kubwa,wanaume wengi hawapendi kufanya hivyo.
 
When you are at fault, you might fear that admitting an error is admitting weakness. On the contrary, apologies are a sign of STRENGTH.
 

Attachments

  • _20170512_191641.JPG
    _20170512_191641.JPG
    84.1 KB · Views: 31
Kuomba msamaha ni ishara ya kustaarabika na kujitambua Hasa kama unakuwa unaomba msamaha huo kwa dhati ya moyo wako na sio kushinikizwa.

Mimi mwenyewe na utata wangu wote ila kuna muda huwa ninaomba msamaha Hasa nikitambua kuwa nilichemka kwenye jambo husika (kiwe la kifamilia, mahusiano ya mapenzi, kikazi au la kisela tu na wana)

Hii huwa ina kufanya nijisikie mwepesi na mwenye jamani tele moyoni mwangu , na maisha kuyaona mswano kama kawa. Life goes on as usual as planned.

Hii huwa ni tiba s
 
Tumejijengea ivo,kuomba msamah ni ishara ya udhaifu,lakin ukweli upo tofauti,MTU akiomba msamah ni ishara ya ukomavu kiakili,..unamsadia yule ulimkosea kukusamee na wewe kujifunza kutoka katika lile kosa,..
 
Back
Top Bottom