Mradi wa Maji wa Milioni 550 Watekelezwa Usinge Jimbo la Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
"Kaka yangu Aloyce Kwezi amekuwa akinielekeza tatizo la maji hapa Usinge. Sasa Kwezi asipoongea itakuwaje. Mnatakiwa kumshukuru na kumpongeza sana, Mbunge wenu ni katika wabunge walio makini sana ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehakikisha amesemea Usinge mpate mradi wa maji" - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Na baada ya sisi kuendelea kukung'uta vihenge ambavyo Dkt. Samia ametupatia miradi mikubwa inayokuja huku Kaliua tuna mradi wa Bilioni 143 lakini bila Mbunge Kwezi huu mradi wa Usinge haufiki tunafanyaje" - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Tumeendelea kunoa vichwa kama Wizara hadi tulipoweza kusanifu mradi wa shilingi milioni 550 padogo hapo usipoweza kukutana na Mbunge ambaye hawezi kutetea hoja yake utaweza kupata milioni 500." - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Nyie ni wafanyabiashara, milioni 500 sipafupi, niparefu na hapo hizo ni jitihada za Kwezi. Mna bahati na niwapongeze na niwasihi msifanye makosa tunapoelekea kwenye uchaguzi mwakani" - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Kwezi hebu simama cheki alivyo na nguvu ameenda hewani jibaba limeshiba linapiga kazi kama tingatinga, unataka nini tena Mungu akupe nini tena akupe kidonda cha pua ukose kufunga bandeji" - - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Huyo ndio kwezi wa Kaliua Mungu amewajalia Mhe. Rais akijua jitihada za Kwezi akawaleteeni jembe Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya "Bingwa" Wanausinge mpo" - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Mungu awape nini, huyu mrembo simmemuona kutoka kule Ulyankulu Mhe. Rehema simama wasije wakaona kama umenisindikaza yupo kazini jamani huyu ni mheshimiwa mbunge mmemuona huyu anatokea Ulyankulu ambapo wote mnasomeka ni Kaliua" - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Hawa wote wanashirikiana kuleta maendeleo Kaliua ndio maana hatupo katika jimbo lake lakini kwa makubaliano na mahusiano mema na Kwezi ndio maana Mbunge mwenzake yupo hapa, Kwezi wa mahusiano Oyeeeh, Kwezi mpigakazi Oyeeeh, Kwezi Wamaendeleo Oyeeeh,Kwezi msabisha mradi wa mkubwa wa maji kuja hapa Oyeeeh," - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Ndugu zangu kwa kuwa muda ni mfupi naamini ujumbe wangu nimeuweka katika maongezi mafupi na mmeuelewa vizuri na sitarajii hata swali maana nimesema kufikia mwezi wa pili mkandarasi anakuja kazini kuna swali hapo" - Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.00.42.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.00.42(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.00.42(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.00.43.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.00.43(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 13.00.44.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.44.17.jpeg
 
Back
Top Bottom