Naibu Waziri Mahundi: Zaidi ya Watu 233,000 Kunufaika na Mradi wa Maji wa Mugango - Kiabakari - Butiama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945

NAIBU WAZIRI ENG. MAHUNDI: ZAIDI YA WATU 233,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MUGANGO- KIABAKARI-BUTIAMA.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wakandarasi wa mradi wa maji wa Mugango - Kiabakari - Butiama waweze kukamilisha utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo ili wananchi zaidi ya 233,000 waweze kunufaika na huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Mhandisi Mahundi ameyasema hayo Desemba 11.2023 wilayani Butiama, mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Mugango - Kiabakari - Butiama na mradi wa maji wa kjiji cha Kyankoma - Kiagata.

Katika ziara hiyo, Mahundi amewasisitiza wakandarasi hao kukamilisha utekelezaji wa ujenzi wa mradi husika ili wananchi wapate huduma ya maji safi na salama.

"Mwishoni mwa mwezi Desemba 2023 mradi huu, uwe umekamilika kulingana na mkataba wa nyongeza, pia namuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mugango/Kiabakari kuweza kusimamia utekelezaji wa mradi huu" -Mhandisi Mahundi

Kadhalika Mhandisi Mahundi amezindua mradi wa maji wa Kijiji cha Kyankoma - Kiagata ambao umetekelezwa na fedha za P for R kwa gharama ya shilingi millioni 609.2 ambapo inaelezwa kuwa kukamilika kwa mradi huo utaweza kunufaisha wakazi zaidi ya 5,200

Kwa upande wake Mbunge wa Butiama Jumanne Sagini ambaye pia ni Naibu waziri wa wambo ya ndani ya nchi ameishukru serikali kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Mugango – Kiabakari – Butiama ambao unatumia chanzo cha maji cha uhakika cha ziwa Viktoria akisema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza kero ya ukosefu wa maji katika eneo hilo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.45.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.45.jpeg
    47.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.46.jpeg
    38.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.47.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.47.jpeg
    45 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.47(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.47(1).jpeg
    34.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.48.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-12 at 16.18.48.jpeg
    40.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom