Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,495
Waziri Maua Daftari atiwa hatiani kwa utapeli
na Irene Mark, Dodoma (tanzania daima)
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imemtia hatiani Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Maua Daftari kwa kosa la utapeli na kumwamuru kulipa sh milioni 100.7.
Uamuzi huo ulitolewa jana na aliyekuwa Jaji wa mahakama hiyo, ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Laurean Kalegeya na kumtaka Naibu Waziri huyo kumlipa fedha hizo, Fatma Salmin ambaye alikuwa mlalamikaji katika kesi hiyo ya madai.
Naibu Waziri huyo alifikishwa mahakamani hapo mwaka 1999 kwa kesi ya madai ya kujipatia fedha kwa nja ya udanganyifu kutoka kwa Fatma.
Katika madai hayo, ilielezwa kuwa Naibu Waziri huyo alishindwa kulipa sh milioni 39.5 kwa ajili ya malipo ya shamba lenye thamani ya sh milioni 40 alilouziwa eneo la Kibaha, mkoani Pwani.
Aidha, mlalamikaji huyo alidai kumuuzia Dk. Daftari mtambo wa kusindika matunda wenye thamani ya sh milioni 100.
Hata hivyo, madai ya mlalamikaji ni kulipwa sh milioni 400 alizotapeliwa na Naibu Waziri huyo aliyedai kuwa rafiki yake waliokuwa wakishirikiana katika biashara mbalimbali.
Akizungumzia hukumu hiyo, Naibu Waziri, alisema hakubaliani na uamuzi huo, hivyo amemwagiza wakili wake, Peter Swai kukata rufaa haraka.
Alisema hana imani na mazingira ya usomwaji wa hukumu hiyo kutokana na ukweli kuwa wakili wake hakupelekewa taarifa mapema.
Sina imani na mazingira ya hukumu hiyo na sina imani nayo hata kidogo kwa sababu wakili wangu amepewa taarifa za hukumu muda mfupi kabla ya kusomwa, tena kwa njia ya ujumbe kwenye simu yake ya mkononi na karani wa mahakama.
Baada ya hukumu hiyo ilinayonitaka mimi kumlipa Fatma sh milioni 100 nimemwamuru wakili wangu kukata rufaa mara moja... naamini huko haki itapatikana, lakini sikubaliani na hukumu hiyo kabisa, alisema Dk. Daftari.
Aidha, alisisitiza kuwa hajawahi kumkopa wala kufanya biashara na mdai, hivyo haoni sababu ya mahakama kumtia hatiani. Hivyo anapigania haki yake na atafanya hivyo hadi atakapokata kauli.
Nilisema mahakamani kuwa sijawahi kumkopa mdai hata siku moja, nimekata rufaa kuhakikisha napigania haki yangu hadi nitakapokata kauli... sidaiwi wala sijawahi kumkopa yule mama, alisisitiza.