Ushauri kwa Waziri wa Ardhi na Makazi: Sikiliza pande zote mbili za mgogoro kabla ya kutoa maamuzi

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Tunakupongeza sana kwa juhudi zako katika kutatua migogoro ya ardhi katika nchi hii lakini ninakushauri uende pole pole na usikilize pande zote mbili yaani mlalamikaji na mlalamikiwa.

Juzi ulikuwa hapa Mwanza na uliamuru nyumba ya Wakili msomi kuvunjwa.

Wakati nyumba inavunjwa Wakili mwenyewe hakuwepo na kwahiyo ulisikiliza upande moja na hivyo nyumba ikavunwa.

Kuna maamuzi mengine inayohusu migogoro ya ardhi yalikwishaamuliwa na Mahakama lakini bado tunaona badala ya kuheshimu maamuzi ya mahakama nyumba zinavunjwa.

Mimi binafsi nakupongeza kwa juhudi zako za kutatua migogoro hii ya ardhi lakini nenda polepole na ukutanishe pande zote mbili ndipo utoe uamuzi.
 
kweli, maamuzi yafanyike kwa kuheshimu Mihimili mingine!
Otherwise naye ataonekana wale wale tu,alafu atajichumia dhambi sehemu ambayo kwania njema kabisa,kafanya maamuzi yasiyo ya haki.
 
Japo alivunja Pinda....

Anaendeshwa na mihemuko, halafu hata ukisikiliza pande zote, toa muda kwa ambaye haridhiki na uamuzi wako aende Mahakamani, kesi inaendeshwa na Silaa siku hiyo hiyo, siku hiyo hiyo anakuwa hakimu, siku hiyo hiyo anavunja, hatoi nafasi mtu aende hata kwa Waziri Mkuu au Rais, yeye ndio Alfa na Omega, amekuwa kero nyingine sekta ya ardhi.
 
Back
Top Bottom