New Songs:Wakuu mnasemaje hapa?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
i251_FACTSCASEno.12001Page1.jpg

i252_FACTSCASEno.12001Page2.jpg

i253_FACTSCASEno.12001Page3.jpg

i254_FACTSCASEno.12001Page4.jpg

i255_FACTSCASEno.12001Page5.jpg


Naongeza Bonus hapa:

i256_Kagoda1.jpg

i257_Kagoda2.jpg
 
Last edited by a moderator:
Swadakta, Mkuu Invi, umelete maneno mazito sana kwa kweli. Sasa swali ni, "Je hawa jamaa wataendelea kufanya ngonjera na ushahidi wote huu???"
 
Tatizo ni kuwa watuhumiwa wanajifanya hawaoni wala hawatambui hata kukiwa na ushahidi wa nyaraka!
 
Mkuu Invisible asante kwa Doc hiyo....Hii Kagoda bado inakuwa siri kubwa,na kinachosumbua kuliko vyote ni hayo majina 1; John Kyomuhendo 2;Francis William.Imechukua miaka miwili sasa hawa watu hawafahamiki ni akina nani?Inawezekana kabisa ni watu tunaowafahamu wametumia majina mengine?
 
Thanks mkuu invisible na kwa kumbukumbu kipindi hiki ndiyo haswa bei ya US dollar ilipoanza kupaa kama kale kandege ka EL
 
Heshima mbele mkuu usiyeonekana......! thanks a million times man!

Hivi hawa kina Mramba, Yona, Mgonja hicho kiburi cha kutosikia hata ushauri wa macollegues wao kilitoka wapi?---who else is benind all these? Kuna watendaji wazuri tu kama Mh. Abdisalaam, Nyero, Mrindiko walitoa angalizo juu ya hawa Stewart na mwingine(Nyero) akasema kabisa hawa si washirika wazuri kupewa hiyo tender...lakini wapi! Na mbali na hiyo TRA ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha mapato ya serikali yanakusanywa ipasavyo na kusimamia sheria na taritibu za kodi, waka muonya waziri na bwana Mgonja....wapi wao wakatupilia mbali ushauri huo na kufanya walilo ona ni bora kwa maslahi yao binafsi!

On Kagoda.....ivi mabenki yetu (hasa hii CRDB) yanaplay role kuzuia ufisadi na Money loundering kwa ujumla? hivi inawezekanaje kupitisha multibillion transactions zote hizo hata kustukia na kufuatilia legitimacy ya fedha hiyo? Nafikiri hawa wenye bank wangetusaidia sana kupambana na ufisadi kama wangeamua kuwa wazalendo!
 
Heshima mbele mkuu usiyeonekana......! thanks a million times man!

In Kagoda.....ivi mabenki yetu (hasa hii CRDB) yanaplay role kuzuia ufisadi na Money loundering kwa ujumla? hivi inawezekanaje kupitisha multibillion transactions zote hizo hata kustukia na kufuatilia legitimacy ya fedha hiyo? Nafikiri hawa wenye bank wangetusaidia sana kupambana na ufisadi kama wangeamua kuwa wazalendo!

Mkuu NL, hapo umenena, hivi haya mabenki yetu yanajua yatendalo?? Wapi wale wakubwa wa BOT, hawa nao si wana wajibu wa kuhakiki shughuli za kibenki kwa benki zote Tz??? Au ndio ilikuwa amri ya wakulu so kila kitu ni kupeta wka kwenda mbele?? Jamani, hivi kweli jamani hawa watu wetu wana vitu kweli mule vichwani vyao au ndio mambo ya "kitu kidogo?". Ukienda kwabwela kufungua akaunti majiswali kibao mpaka unatamani kuweka pesa zako chini ya godoro lakini same banks wanapitisha maji transaction makubwa namna hii!!??
Sikubaliana persee na NN, lakini Mkuu NN ni hard kukataa kabisa, WaTanzania ndivyo................
 
Hawa Yona, Mgonja na Mramba lazima walipata 10% ndo maana wakchangamkia na kuruhusu tax excemption haraka haraka na tena kwa mda mrefu!

Ni corruption au kitu kidogo wandugu!
 
Mkuu tumekusikia, tumekusoma, tumekuona na asante sana kazi njema kabisa hii. JF tukiendelea hivi tutafanya Pesa za walipakodi ziwe za moto kuanzia rais hadi mjumbe.

Salaam kwa Kikwete si unaona kasi hii wewe jihadhari na matumizi ya pesa zetu hizo nyumba Bagamoyo ipo siku tutauliza pesa zilitoka wapi. Angalia sana mkuu hii ni kasi mpya na nguvu mpya ya kufichua maovu. kaa chonjo
 
Mkuu NL, hapo umenena, hivi haya mabenki yetu yanajua yatendalo?? Wapi wale wakubwa wa BOT, hawa nao si wana wajibu wa kuhakiki shughuli za kibenki kwa benki zote Tz??? Au ndio ilikuwa amri ya wakulu so kila kitu ni kupeta wka kwenda mbele?? Jamani, hivi kweli jamani hawa watu wetu wana vitu kweli mule vichwani vyao au ndio mambo ya "kitu kidogo?". Ukienda kwabwela kufungua akaunti majiswali kibao mpaka unatamani kuweka pesa zako chini ya godoro lakini same banks wanapitisha maji transaction makubwa namna hii!!??
Sikubaliana persee na NN, lakini Mkuu NN ni hard kukataa kabisa, WaTanzania ndivyo................

Mkuu Morani,

kama gavana wa benki kuu (BOT) ambaye anatakiwa asimamie maadili yautendaji wa benki zetu ndiye mtekelezaji wa ulipaji wa mapesa haya,

na Waziri wa fedha anayesimamia BOT ndiye muamrishaji pesa ziibiwe

na Katibu mkuu wa wizara ya fedha ndiye aliizinisha ulipaji wa mapesa haya

ulitegemea nini kwa mabenki yetu? Wizi mtupu.
 
Mkuu mimekukubali!!!! Bado kazi ipo kuikomboa nchi yetu kutoka katika mikono ya mafisadi wachache. Ni vita ngumu kuliko ile ya kumng'oa mkoloni, tukiungana pamoja tutafanikiwa.
 
Kweli wizi ni izi tu hivi kweli a central bank governor unaweza kuapprove barua cheap namna hiyo kama hiyo ya kagoda??????? No headed paper, no profesionalism. Yaani basi ubabaishaji tu! Mabilioni yote hayo kwa kiratasi hicho tu!
 
Nadhani tuiachie Mahakama kutekeleza wajibu wake.

I guess na Kikwete tumuachie kuongoza nchi, tusi comment chochote kile, au?

By the way, hii affidavit inasema "As a consequence...The accused were thus arrested and charged with the offences contained in the charge sheet." Tungepata hiyo charge sheet tungeelewa zaidi ni specific offences gani, vipengele vya sheria gani vimevunjwa. Tujue hiyo sheria ya "kusababisha hasara" wametumia ipi hiyo.

Tunaambiwa makosa ya "kusababisha hasara," hawa wadau, especially Yona (na mipango yake na Mkapa), hawakufanya uzembe uzembe kwa bahati mbaya na kusababisha hasara; walinuia kujinufaisha kwa kupanga. Tuseme ni wezi, sio wazembe. Vinginevyo waachiwe huru mapema, tusifanyiwe usanii.

Sheria aliyoharibu Mramba, kwa mfano, ya misamaha ya kodi, inasema wazi kwamba maofisa wakifanya madudu pasipo nia mbaya hawana hatia, vipengele 4, 12, Invesment Act, 1997: A member, officer or other staff of the Tanzania Investment Centre shall not in his personal capacity be liable in civil or criminal proceedings, in respect of any act or omission done in good faith in the exercise of his functions under this Act ...The Centre shall be an Agency of the Government and shall be under the general supervision of the Minister.

Sasa hapo Mramba kama msimamizi mkuu wa hii investment center anaweza kujaribu kujitetea kuwa na yeye analindwa na hii "good faith" exception. Kwamba alisamehe kodi sio kujinufaisha bali kuvutia wawekezaji.

Kama wamejinufaisha tuseme wamekwiba, sio wazembe.
 
Ahsante mkuu.

Hawa jamaa BM, Yona na Mgonja pamoja na washirika wengine ambao labda hatujawajua kweli ni axis of evils!

Hata hivyo haya mambo wakulu wanayajua ila wanatuzuga tu! Kuna jamaa yangu mmoja alinidokeza kuwa anamfahamu sana Mkurugenzi wa UWT (Bw. Othman) na kwamba haya yote yanayofanyika ni usanii tu na wajinga (mabwege - WaTz) tunazugwa tu! Inasemekana yanachongwa na UWT

Kagoda nadhani hadi sasa kila kitu kiko wazi kabisa. Saed Kubenea amesema wazi kwenye Mwanahalisi ya jana kwamba Dowans na Kagoda ni RA. Nilitegemea hadi sasa RA angeshatoa vitisho vyake vya kwenda mahakamani na mahubiri yake ya kila mara kuwa yeye ni mfanyabiashara msafi sana (Mr Clean businessman) lakini sijasikia kitu. Kwa maana hiyo story ya Mwanahalisi ni kweli. Swali linalonisumbua na labda wengine wengi ni kuwa nani achukue hatua? Hivi sisi kama raia hatuwezi kufanya kitu mahali ambapo ushahidi tele uko mikononi mwetu (hapa JF, Kubenea etc)?

Au sote tumetiwa kiwewe?? Nimesikia kwenye taarifa ya TBC Taifa mchana leo kuwa hakimu Mwankenja anaumwa na kesi ya hao mafisadi imeahiriswa hadi tarehe 9 Aprili!
 
Last edited:
Halafu kila siku kuna watu wanakuja kutuambia kwamba Tanzania hatuna wataalam. Wataalam wapo sana, tatizo ni kwamba wana siasa wetu ndo wamegeuka kuwa watalaam na wao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. Matokeo yake maamuzi hayo ya mwisho wamekuwa wakiyatumia vibaya kwa kuwa wanajua kwamba hakuna chochote ambacho kitafanyika.

Ukifunua ma-file huko kwenye hizi ofisi za serikali unaweza kukuta madudu mengi sana na kuanza kujiuliza kwanini huyu mtu mpaka leo bado yuko huru wakati alisababisha madudu na hasara kubwa sana?
 
Back
Top Bottom