Neno La Leo: Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

Nyie watu, mbona mnabishana Mdomo uko wapi wakati pua mnaiona?

HIVI KATIBA INASEMAJE kuhusu kesi kama hii ya Rais wa nchi anafariki / Kufa?

Je ni kweli Mbunge wa Chama (Mbowe) atakuwa RAIS? Si huyu Mbowe Watz walimkataa?

Au hata awe PM, katiba inamsema PM awe Rais wa nchi? Labda awe SPIKER wa bunge na hata hivyo itabidi Rais na Makamu wake wote wawe wamekufa. Na hata hivyo, spiker inabidi tu aitishe Uchaguzi haraka na si kuwa yeye ndiyo awe Rais. Kwenye uchaguzi hakuna uhakika kama atashinda. Kama watu wanataka kumuondoa Kikwete, sembuse Mbowe kama Acting President kwa nguzo ya Spiker?

Ingelikuwa BUSARA zaidi, Maggid akaaanza kukubaliana na Dr Slaa ili katiba kwenye hili swala iwekwe wazi zaidi na kama kuna utata unaweza kuleta nchi kuyumba basi na huo pia uondolewe.

Kwa kifupi hapa ni SWALA la KATIBA na si MTI MMOJA. Kama Chadema hakijajiandaa na Rais wao janga limemkuta, basi wataondolewa na CCM kama siyo CUF. Vita yao ni furaha ya Kunguru. Mbaya kama wakipatana, hapo tunaumia sisi Wananchi. Hebu ona kicheko cha CUF wakikutana na CCM leo, unategemea Mzenji atafaidika kweli hapo? CCM Zenji wanapeta tu wala hawana Wasiwasi.
 

- Tukisimamia hoja hii thread ina mengi mazuri, lakini tatizo linaletwa na ushabiki, unashia kuiharibu kabisaa hii thread halafu inaudhi kweli!

Es!
 

- Bob mkuu wangu huu ni mtizamo wako tu na ni moja ya mitizamo mingi over the Mada, hujakosea wala anything na wengine pia ila mitizamo mingi ndio hasa Demokrasia na upanuzi wa elimu kwetu wengi at large, right on the track bro!

Es!
 
Mkuu sioni kabisa Usahihi wa lolote lile kwani huwezi fananisha binadamu na mti au misitu ambayo haina mahusiano baina yake labda tu ktk concept ya mchumia tumbo kwani kila mti ktk msitu mzima hujitegemea..hakuna mahusiano baina ya mti mmoja kwenda mwingine zaidi ya kuona msitu mkubwa hali miti yote inategemea kulishwa mvua na rutuba iliyopo..
 
Sasa mkuu umesema Slaa na Lipumba wana same shot kwenye presidency,lakini mbona hujasema Dr Slaa na yeye ana nguvu ukanda gani?kama ulivyotolea mfano wa umaaruf wa Lipumba huko kanda ya kusini?Ama ni ukanda wa kaskazini?
Naombatueleweshane.
 
JF ni "The Home of Great Thinkers" japo pia ni kaya " Where we Dare to Talk Openly!"

Tusiifanye JF uwanja wa uzalisha, ulea na kueneza "hate propaganda"!
 
- Tukisimamia hoja hii thread ina mengi mazuri, lakini tatizo linaletwa na ushabiki, unashia kuiharibu kabisaa hii thread halafu inaudhi kweli!

Es!
Sasa ile agenda ya Independent Candiates ambayo wengi wameililia sana hadi mahakama ya rufaa inakuwa irrevant hapa? Mie naungana kabisa na yule asemaye msitu basi uwe wananchi; otherwise tukubali kuwa agenda ya Independent Candidates haitakuwepo katika demokrasia yetu!
 
Kwani mjadala ukiwa hauna mwelekeo inakuwaje? Anageuziwa aliye uleta.
 
kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi. Ebu niambie kwenye kura za maoni ya sisi m si kulikuwa na side ya upinzani vile vile! hao walikuwa ni wakina nani? Maana, maana ya upinzani ni kuwa kuna side mbili zinapingana. Sasa ebu niambie kule Dodoma wapinzani kwenye kambi ya sisi m alikuwa nani na angeungana na nani? kwi kwi kwi kwi
 
I do think this is not the mjengwa we thought. i cant believe he is the one we used to know!
 
Kitu kikubwa ninachojifunza ndani ya hizi debate/discussions ni kuwa soon or later watu tutaanza kufikiri na kutenda nje ya mazoea. Fikra zinapojengwa na kutumiwa kwa usahihi zinaleta mabadiliko makubwa sana. Kule tulikotoka tulijisahau, tukawaacha watu wachache wawe wanafikiria mambo yote kwa ajiri yetu. Sasa hivi tumetengeneza matatizo makubwa kiasi kwamba hatuendi mbele kama Taifa. Ninafurahi kuona mwanga unaanza kuonekana taratibu. Siku za kudanganyana zimebaki chache na zinakaribia kikomo. Mwenye macho haambiwi ona!!
 
Maggid huyoooooooooooo kesha waacha mparurane macho. Yuko wapi kutetea hoja? Ngoja nimtafute acid

Ndugu Yangu Mchukia Fisadi,

Sijawaacha. Nimeanzisha mada hii na naifuatilia kwa makini sana. Nasoma kila kinachoingizwa. Haya tunayoyajadili hapa ni mambo mazito na ya muhimu sana kwa taifa letu. Kuyachukulia kwa wepesi wepesi na mzaha mzaha ni hatari sana. Maana, katika siku zisizozidi 21 Watanzania tunakwenda kufanya maamuzi magumu, makubwa na mazito yatakayoamua mustakabali wa nchi yetu.

Tukifanya makosa, tutasubiri miaka mingine mitano au hata kumi kurekebisha makosa hayo. Nilijiunga hapa JF baada ya kusikia sifa za mahali hapa, kwamba JF ni "The Home of Great Thinkers, Where People Dare to Talk Openly!"

Na kwa staili yangu nazileta hizi mada humu ili ' Great Thinkers' wazichambue, wazijadili, waje na mawazo na mengineyo yenye manufaa kwa taifa. Nilifahamu, kuwa ' Kwenye msafara wa mamba na kenge wamo ". Kwamba miongoni mwa 'Great Thinkers' wa JF kuna wasiofanana na jina hilo, na wakati mwingine hawafanani hata na kenge, bali mijusi.

Ndio hao, mara wanapoona hoja imewasilishwa, basi, wanakimbilia kumshambulia mtoa hoja. Ni wavivu wa kufikiri. Kufanya kazi ya kuisoma kwa makini hoja husika, kuikubali au kuikataa kwa hoja.

Katika mada hii nimeona hatua ya maana imeanza kupigwa. Watu wameanza kujadili "Urefu wa mti", hivyo basi, wanajadili hoja. Naona kuna ambao wamenielewa, tena vizuri sana. Kuna ambao hawajanielewa hadi sasa, naamini watakuja kunielewa vema mbele ya safari.

Ndugu zangu,
Hii ni nchi yetu. Ni nchi yetu sote, kama Watanzania sisi ni ndugu. Nchi ni kama mama, hatuwezi kuchagua mama. Ndio maana tunaipenda nchi yetu. Inahusu Watanzania zaidi ya milioni 40. Kumchagua Mtanzania atakayepewa jukumu la kushika dhamana ya watu milioni 40 si sawa na kucheza ' ngoma ya lelemama'. Tuwe makini, na wakati mwingine si vibaya tukagombana kwa hoja.

Kwangu mimi kutoka Jangwani peke yangu na kupandisha Magomeni ilihali nikijua nitakutana na umati wa watu usio na mtazamo kama wangu ni kazi ya kuutafuta umakini huo. Tuanze kujadili.

Ni bahati mbaya, kuwa kila unapotoa hoja, watu hukimbilia kukutafutia droo ya kabati la kukuingizia; CCM, CUF, CHADEMA, Dini, Kabila, Ufisadi na kadhalika. Wengi tumelisahau droo muhimu sana katika kabati letu; Droo la Tanzania.

Mimi nimo kwenye droo hilo. Katika kila nifanyalo; naangalia kwanza, kama lina maslahi kwa Tanzania. Wanaojihangaisha ni wale wanaonitafutia droo nyingine za kuniweka na kuliacha droo langu la Tanzania. Ni kwa vile hawanijui.
 
Sio tu uchambuzi wa kisiasa unakushinda kuandika bali hata makala zisizo za siasa....wewe si mwandishi mzuri kwani uwezo wako wa kufikiri uko chini ya unaojaribu kuwaandikia!!!!!
 
Sio tu uchambuzi wa kisiasa unakushinda kuandika bali hata makala zisizo za siasa....wewe si mwandishi mzuri kwani uwezo wako wa kufikiri uko chini ya unaojaribu kuwaandikia!!!!!

Kazi ipo mwaka huu!
 
we Majjid acha njaa zako katiba inamruhusu Dr Slaa hata kuchukua watu wa CCM kuunda serikali ili mradi anawasimamia yeye na rungu mkononi si ajabu watu kama Dr Mwakyembe na Dr Magufuri wakala shavu! halafu hivi ni wewe uliyesema ati umeandika kitabu cha Obama ati? Teh teh pumba zako weweee ndo maana magazeti yako hufa kila siku!
 
Joka Kuu said:
..kwa upande wangu nadhani kura za Uraisi hazitatofautiana sana baina ya vyama vitatu CCM,CUF,na Chadema.

Mh Joka Kuu,je una maana kila mgombea urais ana nguvu kwenye kanda flani pekee na kwamba hicho ndiyo kigezo cha kuwa kura zao hazitatofautiana sana?Nimekuomba unieleze kuwa Dr Slaa na yeye ana nguvu kanda gani?JK and so forth...Umeshaweka wazi kuwa Lipumba ana nguvu huko kanda ya kusini,na ukasema hiyo ndiyo sababu ama kigezo kuwa yeye na slaa wana nafasi sawa za kupata urais....hata hivyo haujataja upande ambao unaona chadema nao wan nguvu na hivyo kuwa sawa na cuf...

Kwamba nafasi zao za kupata urais ni sawa ie the probability of choosing Dr Slaa is the same as the one of choosing Lipumba?

je hayo ni kweli? Je ni kweli kuwa cuf na chadema wamegawana hizo kanda kwa kiasi kwamba wana nafsi sawa za uraisi? Vipi kuhusu hizo polls zinazotolewa?Mbona sioni ukaribu huo unaouzungumzia?Vigezo gani umetumia mkuu?

Je inawezekana habari za hapa JF ni za upotoshaji?Ukishaniwekea hapa sehemu/kanda ambazo chadema,ccm na cuf wana nguvu,then tunaweza kuanzia hapo....hii itasaidia sana kwasisi kuweza kubainisha kama uwezekano huo upo ama haupo....Je ni kanda zipi hizo ambazo Lipumba na cuf wana influence zaidi na pia ni zipi ambazo ccm na JK wana influence, zaidi?what about chadema na Slaa?

Kwa kuanzia,kanda ya kaskazini ni wazi chadema ina nguvu,ila sidhani kama ni kanda hiyo pekee...Tuwekeeni taarifa watu mlio karibu na matukio....Nimeona picha,video,habari nk za mikutano ya Dr Slaa huko Mbeya,Iringa,Rukwa nk....Vipi kuhusu Lipumba?
 
Nje ya mada, Nelson Mandela aliyasema hayo maneno kwenye hotuba gani au kwenye kitabu gani?
 

- Great Thinker ha! ha! ha! ah! ha! ha! inachekesha sana ha! ha!

Es!
 

- Majjid Great Thinking bro!

Es!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…