Omarlyas,
Mkuu wangu nadhani unajibu maswala mengi kimkato sana kiasi kwamba sikuwezi kukuelewa vizuri.
Kwanza kabisa umesema haya
Angalao Kikwete ana guts za kuuacha Lowassa ajiingize kitanzini...vipi Dr Slaa ni lini ameweza kusimama mbele ya maslahi binafsi ya Mbowe????
Second, Kuhusu ujuvi ama uledi wa masuala ya Utawala nina uhakika asilimia 100 kuwa Kikwete anamzidi Dr Slaa. Ofcourse Kikwete ana advantage ya kupewa nafasi ndani ya mfumo kujifunza kwa muda mrefu lakini ukiangalia mapambano na sasa majigambo, vikwerombwezo na mikwara ya Dr Slaa, kimoja kiancho onekana ni kuwa hajatumia muda wake kujifunza vya kutosha namna serikali ama utawala unavyofanya kazi...]
Maana ya hoja zangu ni kuweka mstari baina ya watu hawa wawili kwani JK ni rais na Lowassa alikuwa waziri mkuu aloteuliwa na JK tofauti na Dr.Slaa ambaye ni katibu wa chama na Mbowe ni Mwenyekiti wake hivyo wadhifa wa Dr.Slaa haulingani na ule wa JK ktk dhamana na majukumu walokuwa nayo..
Kisha si lazima Dr.Slaa apingane na Mbowe ili aonekane kiongozi mzuri ikiwa swala ni maamuzi ya Mbowe kuhusiana na Zitto au mwanachama mwingine yeyote, na hasa pale Zitto anapotaka kugombea kiti cha Mbowe mwenyewe. Mtu yeyote anaweza chukua side kulingana na katiba ya chama au jinsi mtu huyo anavyoona uhalali wa kitendo hicho. Kwa hiyo sioni kabisa udhaifu wa DR.Slaa akiwa rais kuhusishwa na nidhamu alokuwa nayo leo kwa kiongozi wake na wala haina maana Dr.Slaa haelewi mapungufu ya Mbowe. Mbona kina Kitwete wote hawa bado ni royal kwa Mzee Kitwana Kondo mkorofi lakini wanaheshimu mchango wake kwa chama na hata siku moja hawatadiriki kumtia kidole cha singi!.
Hivyo sina sababu kubwa ya kujua katibu mkuu anapatikanaje ili kukubaliana na hoja ya Loyality ya Dr.Slaa kwa Mbowe unless unataka kuhnambia kwamba hata nafasi hiyo hakutakiwa kupewa isipokuwa kwa hisani ya Mbowe. Na hakika mkuu wangu najua kwamba unajua vizuri kwamba namfahamu Mbowe kwani waswahili wanasema tumempokea mjini. Na kwa njia hiyo kubali kwamba namfahamu Mbowe kwa mengi mabaya na mazuri, lakini inapofikia swala la Uongozi ni muhimu sana tukubali sote kwamba siku zote dereva ni mmoja na tumwache dereva aifanye kazi yake kama dereva..
najua fika umewahi kuendesha ukampakia mtu kisha kila unalofanya atakurekebisha, funga brake, usifanye hivi ama vile mara nyingi safari kama hii huishia pabaya zaidi na ndicho nachokiona zaidi kwa Wapinzani wa Mbowe.. Zitto, is a good fella and he means well for the party lakini muhimu pia tufahamu kwamba ndani ya chama kuna watu wenye ambition..Hizi ndio siasa za nchi za kiafrika yaani upinzani ni baina ya watu badala ya vision ya mtu kwa wananchi na taifa. Zitto na Mbowe kama picha haziendi haziendi hata aje mtume haitasaidia...
Na pengine hujawekea maanani sana maswala ya Chadema na jinsi Dr.Slaa alivyocheza kwani kama Dr.Slaa angefanya unavyofikiria kuwa bora basi leo hii Chadema kisingekuwa chama kilichopo leo na kimeweza kusimamisha mgombea mmoja anayependwa na wananchi. Chadema ingemeguka vibaya sana na pengine kufa kabisa kutokana na kashfa ndogo sana na za kipuuzi.
Hili ndio lilikuwa lengo la CCM kuisambaratisha Chadema kwa kupitia Mbowe na hakika kidogo sana wafanikiwe lakini chama kimeweza kusimama imara. Kama hukuliona hilo basi mkuu wangu ndio nakueleza kwamba CCM walitaka Chadema ife kwa kupitia Mbowe na hakika Zitto aliupanda mkenge ingawa kikatiba hakuona ubaya wake kuweka Upinzani kwa mwenyekiti..
Na mwisho mkuu wangu mimi sii mjumbe wa Chadema wala sina ushabiki na Mbowe kwa sababu namfahamu vizuri zaidi ya misukosuko mlokuwa nayo leo ndani ya Chadema, na najua fika wala sii Zitto pekee wanaolalamika na Mbowe wapo wengi na wenye wadhifa ndani ya chama lakini wote hawa wamekuwa royal na uongozi wa Mbowe kwa sababu lengo halikuwa kumchafua Mbowe bali kukisambaratisha chama cha Chadema..Na Mbowe mwenye kachangia sana kuendeleza azma ya CCM anapoweka kisasi au chuki na baadhi ya wanaChadema..