Neno La Leo: Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,

“ One tall tree does not make a jungle”- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.
Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.
Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejindaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake. Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba, kitaangukia kaburini.
Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid,
Msamvu, Morogoro
 
neno la leo halikupaswa kuwa na makala ndeeefu kama hii

halafu umepanga vibaya sana kazi yako umepaste eehh!

by the way pole na mafuriko yaliyokukuta.......
 
Maggid . you have tried to post the same for five time today only
 
Maggid... you have tried to post the same for five time today only

Acid,
Nawe ni kielelezo cha tatizo la baadhi yetu Watanzania, badala ya kuchangia hoja kwa kuikubali au kuikataa kwa maelezo, unamshambulia mtoa hoja! Nyie mpo na mtaendelea kuwapo. Ni sehemu ya jamii.
 
I guess you are talking about CCM kwamba kinamtegemea Kikwete tu kwa ajili ya ushindi wake. Maana Makamba alisema Kikwete ni maarufu kuliko CCM.

It's no wonder kwamba hapa unamaanisha kwamba umaarufu wa Kikwete hautoshi kujenga msingi imara wa chama. In this view, I congratulate you, you have said it well.

Tena napendekeza umpelekee makala hii Makamba, kumkumbusha kwamab umaarufu wa Kikwete na familia yake hauwezi kujenga chama imara na uongozi imara wa chama.
 
na wewe pia ni sehemu yajamii

tofauti yangu na wewe ni upupu uliokujaa ukidhani a wewe ni mwandihsi wa habari simply because they gave you a column

huna chochote kwenye fani na unatia huruma kwa kudhani wewe pia u-mmoja wa waandishi

maggid, nisamehe lakini nakuangalia kihuruma zaidi,

pole mnafiki
 
msamehe maggid... hana data za due diligence kuelewa asemayo

he is just trying to win a few sympathetic hearts
 
na wewe pia ni sehemu yajamii

tofauti yangu na wewe ni upupu uliokujaa ukidhani a wewe ni mwandihsi wa habari simply because they gave you a column

huna chochote kwenye fani na unatia huruma kwa kudhani wewe pia u-mmoja wa waandishi

maggid, nisamehe lakini nakuangalia kihuruma zaidi,

pole mnafiki

Acid ndugu yangu,

Ni nani alikwambia kuwa mimi ni mwandishi wa habari?
Au ni wapi nilipowahi kuandika kuwa mimi ni mwandishi wa habari?
Kama huna majibu ni vema ukapima mwenyewe kama uendelee na malumbano au la.
 
Huyu jamaa naona anakuja ki MS karibu tutamdharau na kuanza kumpambia mapambo kwa sababu hana jipya anarudia yale yale yaliyopuuzwa jana na juzi.
 
Acid ndugu yangu,

Ni nani alikwambia kuwa mimi ni mwandishi wa habari?
Au ni wapi nilipowahi kuandika kuwa mimi ni mwandishi wa habari?
Kama huna majibu ni vema ukapima mwenyewe kama uendelee na malumbano au la.

Maggid... hii kweli kali ya leo... atowae tiba si tabibu??

na aandikaye habari si mwandishi wa habari??? mbona unakimbi akivuli chako mwenywe kikupachopesa ya kula????

rudi kamwambie aliekutuma kwamba kazi ni ngumu na akuongezee 50%

remember, politics are momentarily encounters but we (Tanzanians) are here for life

You are a puppet
 
absolutly crap... CCM ni chama cha uongozi? miaka 50 ya uhuru bado twawatwisha akinamama ndoo za maji na kujisifu ati Rais wetu ni rafiki wa watu!!! Mfumo mzima wa Utawala wa CCM ni upupu mtupu... kwa taarifa yako ni mtu mmoja tu ndiye anayeweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa jamii yake na wewe mwenyewe umeweza hata kuwataja so hoja yako ya mti na miti ni nadharia ambayo unajaribu kuipindua iwasaidie ninyi mafisadi ambao mnafiri mmeiteka nchi yetu... penda msi pende mabadiliko ni lazima...
 
Maggid... hii kweli kali ya leo... atowae tiba si tabibu??

na aandikaye habari si mwandishi wa habari??? mbona unakimbi akivuli chako mwenywe kikupachopesa ya kula????

rudi kamwambie aliekutuma kwamba kazi ni ngumu na akuongezee 50%

remember, politics are momentarily encounters but we (Tanzanians) are here for life

You are a puppet

Acid ndugu yangu,
Umefeli kujibu maswali yangu. Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kuandika vitabu na makala, hajawahi kutambulishwa wala kujitambulisha kama mwandishi wa habari. Unaelekea kuwa ni mwenye msongo na kujawa chuki. Hilo ni tatizo lako. Zangu ni pole tu.
 
swali moja tu!!!

unapata ujira kwa kazi ya kuandika au kuongoza?? (maana nyerere ujira wake ulijulikana unatoka wapi... na wewe je?

mimi si ndugu yako by the way
 
Mtazamo huu wa Maggid unaweza kuwa na ukweli ndani yake, lakini ni too simplistic. Mfano, ushindi wa National Rainbow Coalition Kenya kwa namna moja au nyingine ulitegemea kwa kiasi kikubwa infuence na sheer personality ya Raila Odinga kuhamasisha Umma, na siyo makada au mfumo wa uongozi wa NRC.
 
proper mkuu... je maggid ana upeo huo?
 
swali moja tu!!!

unapata ujira kwa kazi ya kuandika au kuongoza?? (maana nyerere ujira wake ulijulikana unatoka wapi... na wewe je?

mimi si ndugu yako by the way

Acid ndugu yangu,

Kama huna hoja tumalize malumbano haya. Nisingependa kutumia jukwaa hili kuzungumzia masuala ya ujira wangu, hayo ni ya binafsi. Nitafute tupate kikombe cha chai tuongee hayo. Mimi niko Iringa. Karibu sana ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom