Neno La Leo: Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

Neno La Leo: Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

Acid ndugu yangu,

Kama huna hoja tumalize malumbano haya. Nisingependa kutumia jukwaa hili kuzungumzia masuala ya ujira wangu, hayo ni ya binafsi. Nitafute tupate kikombe cha chai tuongee hayo. Mimi niko Iringa. Karibu sana ndugu yangu.

Ahhh, mijitu mingine bwana, ushaambiwa yeye sio ndugu yako unalazisha, by the way sijuhi kama ACID anashida ya chai! unata mgawane kidogo ulichopewa ili akufichie UJINGA WAKO? wewe tulia umeingia cha KIKE LEO!
LAZIMA UMKOME NYANI GULABU! tetehetehee!
 
hana lolote huyo acid

watanzania tumefunzwa ustaarabu na kuaminisshwa sote ni ndugu kinyume cha uadui ambao anautaka huyo acid, upenzi wake kwenye vyama umempofua mpaka anatamani uadui kuliko udugu loh hasara yake.

tukija kwenye mada, kuna ya kujifunza mengi tu, chama au kikundi chochote imara si mtu mmoja peke yake, maana sawa na sehemu yenye chemni moja tu na watu wote wanategemea kuona kupitia chemni hio, sasa ikizima watu wote wako gizani, hilo ndio alilomaanisha

na nnachofahamu yeye amenukuu maneno ya mandela na nnataraji vyama vina haki ya kujifunza na kujikosoa ikiwemo chama changu CCM kujipanga na kuwanoa makada wake vyema kuelewa misingi ya chama na kujipanga iwapo yeyote anaondoka mapambano yanaendelea tena yanaendelea kwa kufata misingi ya chama husika sio kila mtu anakuja na umaarufu wake pasipo kuelewa misingi ya chama husika

tuwe watu ambao kweli ni wasomi na sio wapumbavu, chadema kwa mfano ina watu wachache ambao ni vinara na nnamini wengi wao wanatumia umaarufu wao na huenda nata ili misingi ya chama chenyewe hawakijui.

tujadili mada badala ya mtu.
 
I guess you are talking about CCM kwamba kinamtegemea Kikwete tu kwa ajili ya ushindi wake. Maana Makamba alisema Kikwete ni maarufu kuliko CCM. Its no wonder kwamba hapa unamaanisha kwamba umaarufu wa Kikwete hautoshi kujenga msingi imara wa chama. In this view, I congratulate you, you have said it well.
Tena napendekeza umpelekee makala hii Makamba, kumkumbusha kwamab umaarufu wa Kikwete na familia yake hauwezi kujenga chama imara na uongozi imara wa chama.
He is talking about Chadema; he has a motive!! Tatizo kubwa la Majidi ni ule uwezo wa kuelewa kipi anaandika. Mara nyingi hujijibu mwenyewe. hapa angalia: Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. sasa hapa CUF na Chadema wapo wapi?
 
Na Maggid Mjengwa,
" One tall tree does not make a jungle"- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.
Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.
Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejindaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake. Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba, kitaangukia kaburini.
Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid,
Msamvu, Morogoro

PUMBA TUPUUUU! Kibarua cha uandishi ndiyo kinachokuweka mjini leo unakikataa kibarua hicho eti wewe si muandishi kwi kwi kwi kwi basi ujiite msanii wa chama filisi cha mafisadi.
 
Na Maggid Mjengwa,
" One tall tree does not make a jungle"- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.
Kweli one natural tall tree can not make a jungle lakini that natural tall tree can be a sign that a jugle can be created in that area. Lakini kumbuka vile vile many tall trees sio sign of jungle they can be "artificial" trees. Dubai huko wana mifano ya kutengenza

Na ukisema chama cha kisiasa cheny nguvu ni nguvu gani??? Nguvu za kifisadi, nguvu za kiadilifu, nguvu za kizalendo au ..... fafanua mkubwa.

Binafsi naona hata lama chama kina mtu moja wa kumtegemea ambaye muadilifu ni bora kuliko chama kinachoongozwa chenye nguvu, kinachohubiri uadilifu lakini matendo yake kwa miaka 40 ni tofauti. Nguvu za chama limojawapo ambacho hujapenda kukitaja badla yake umetumia TANU ni za kiutawala sio za nguvu za kiuongozi.

Vile vile elewa hata mti una shina na mizizi, familia ina chanzo, mto una chanzo na vyama vya siasa vina waaasisi. I mean before having many you start with one.

Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.
Je vipi nikisema tanzania bado hatujakombolewa?Je vipi nikiwakwambia kama ni kweli unayosema si sawa CCM kujiita chama chacha kiuongozi. Ni kweli kazi ya ukombozi iliisha. Je wanachi wameshakombolewa na matatizo ya msingi kama afya, elimu, nishati miundombinu?

Kimtazamo mwingine naweza kusema kazi ya ukombozi hata hao TANU hawakuikamilisha waliishia njiani wakaanza mikakati ya chama kumiliki dola.

Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Sasa tupe mfano kwa Tanzania kwa mazingira ya sasa. Kuwa muwazi vyama tllivyonavyo ni CCM, CHADEMA , CUF, NCCR TLP. etc Ni ipi unaona ni chama cha mtu 1ja ?Umri wa vyama unajulikana. advantage, postion na operating enviroment ya hivi vyote tunavijua.Weka factor zote in consideartion. sasa kipi ni chama bora? Binafsi naweka CCM cha mwisho. tumewapa usukani lakini sio tu hatufiki bali hatujui tunaenda wapi lakini gari linakwenda. sijui unasemaje ka hilo

Kuna usemi pia ni bora uwe na jeshi la mtu 1ja mwenye uzalendo na ari kuliko kuwa na jeshi la askari ambao hawana ari wala nia ya dhati na uzalendo wa kupigana vita.

Vile vile usisahu wataalmu wanakwambia QUALITY should be of more priority na sio QUANTITY.

Kuna chama kina makada wengi wanaielewa itikadi malengo na shabaha ya chama chao. lakini matendo yao ni tofauti na uelewa wao. risk ya Umeme wa mgao ukija mwaka kesho watasema ni changamoto.

Mfano mdogo chama hichi chenye makada wengi kiko madarakani.kwa miaka kama 10 umeme mijini kimekuwa tatizo.Wao wanasema kila mwaka tatizo la umeme ni changamoto. Mimi nasema mgao wa umeme sio changamoto ni Failure. Changamoto inakuja mara moja tu ikija mara 10 ukashindwa kuikabili ni failure. Mgao wa umeme sio kimbunga au mafuriko. Usisahu Makada hawa wengine wana PHD, na degree mbili mbili.

...............
 
Maggig is a messenger of bad news and simply paid to convey it. To me is nothing but a nuisance
 
'Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake'.

Interesting, CCM haiunganishwi na itikadi bali maslahi. Kinachofanya mpaka leo chama kinaexist ni maslahi tu. Ndio maana huwa nnasema si vema kukiita CCM chama cha kisiasa, hiyo ni kutuzuga tu, hilo ni kundi la criminals, na kuthibitisha hilo angalia EPA, RICHMOND, RADAR, NDEGE YA RAIS, KILIMO KWANZA, MEREMETA.

Ni mpaka watanzania tutakaposhtuka kuwa tunaongozwa na MAFIA ndio hapo tutakaposalimika, the good news is tumeshtuka already na wao wanajua sasa kuwa tumeshtuka, so wameanza kuandaa majeshi kwa mapambano ili waendelee kutunyonya.

History reminds me kwamba governments dhalimu zote duniani siku moja zinaondoka tu.
 
proper mkuu... je maggid ana upeo huo?

Acid
user-offline.png
Banned
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Sat Apr 2008Location Dar - TzPosts 6,721Thanks 2,842Thanked 2,959 Times in 1,701 Posts
 
'Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake'.

Interesting, CCM haiunganishwi na itikadi bali maslahi. Kinachofanya mpaka leo chama kinaexist ni maslahi tu. Ndio maana huwa nnasema si vema kukiita CCM chama cha kisiasa, hiyo ni kutuzuga tu, hilo ni kundi la criminals, na kuthibitisha hilo angalia EPA, RICHMOND, RADAR, NDEGE YA RAIS, KILIMO KWANZA, MEREMETA.

Ni mpaka watanzania tutakaposhtuka kuwa tunaongozwa na MAFIA ndio hapo tutakaposalimika, the good news is tumeshtuka already na wao wanajua sasa kuwa tumeshtuka, so wameanza kuandaa majeshi kwa mapambano ili waendelee kutunyonya.

History reminds me kwamba governments dhalimu zote duniani siku moja zinaondoka tu.

Sawia mdau.

Hapa naona lengo la Mjengwa ni kuishambulia CHADEMA, kama kawaida ya ule usemi wa mti wenye matunda mazuri kutupiwa mawe..lakini hata hivyo hoja yake haina nguvu kwa sababu sote tunajua Chadema ina 'father figures' wengi tu wa kuaminika.

Pili kama ulivyosema CCM haiunganishwi na sera wala muono wowote wa sayansi ya siasa, bali maslahi. Wangekuwa walau na muono mmoja wasingejiita wajamaa huku wakifanya tofauti na ujamaa. Hata hizo sera na ilani (manual za kuwachakaza watz kwa umaskini) zinaeleweka kwa makada wote, OUTPUT I WAPI?

Jibu kila mtu analifahamu.
 
Unajua Maggid inawezekana anafikiri CCM ina msitu simply kwa sababu viongozi wake wanajulikana na wananchi, lakini anasahau kujulikana kwa viongozi hawa kumetokana na CCM kushika dola hivyo basi wengi wao wamekuwamo serikalini kama mawaziri, wakuu wa mikoa,wilaya, viongozi wa mbio za mwenge etc. As such ana kutokana na historia ya nchi yetu wamekuwa maarufu na wamepewea umaarufu na vyombo vya umma vilivyokuwa ndiyo the only source of information those days. Lakini tukija wamefanya nini individually na kama group hapo ndiyo kwenye utata.

Maggid anashindwa kuelewa kwamba CHADEMA mfano kama chama kimeweza kuexist toka mfumo wa vyama vingi uanze kikiwa na wabunge, in every term. Majidd anafikiri ili chanma kionekane kinaweza basi kiwe na mabalozi makatibu kata, na wenyeviti nchi nzima. Anasahau kwamba huu ni mfumo wa CCM ulioistawisha CCM na kuwaacha the rest of Tanzanians hapo walipo in 50 years. Muda si mrefu Maggid anaweza kuanza kuuliza barabara iliyojengwa na CHADEMA iko wapi?
 
tuwe watu ambao kweli ni wasomi na sio wapumbavu, chadema kwa mfano ina watu wachache ambao ni vinara na nnamini wengi wao wanatumia umaarufu wao na huenda nata ili misingi ya chama chenyewe hawakijui.

tujadili mada badala ya mtu.
Naam!
 
Naomba nimweleweshe Bw. Majid,kuwa kila kitu huanzia kwa mtu mmoja,na kutoka kwake ndio tunakuwa na wafuasi.Mfano huenda wewe ni muislamu au mkristo,muanzilishi wa ukristo ni mtu mmoja hali kadhalika uislamu.From there ndio tunakuwa na wewe na mimi.Taifa huanza na mtu mmoja na ndio maana kila Taifa yupo mtu anaitwa Baba wa Taifa.Hivyo basi kwa leo hii Mkombozi wetu lazima awe ni mtu mmoja anayeungwa mkono na watu,na si kikundi cha watu kama unavyohoji.Je nini kianze Bwana Majid,oganaizesheni au ukombozi?Na Bwana Majid wakati wa kutafuta ukombozi hutapata watu wengi maana ni waoga kama wewe ila baada ya kupata,watakuja wengi kila mmoja na utaalamu wake ili mradi aonekane naye ni mkereketwa.Kama kweli Tanzania tunataka ukombozi wa kweli tuamue,tumpe yule tuliyemwona anaweza kutukomboa.Hivyo usiogope na kuulizia organiztion

MPE DR.SLAA KWA MAENDELEO YA KWELI
 
Maggid amenunuliwa na ccm kazi aliyopewa ni kuharibu vichwa vya wana jf lkn amechemka.
 
maggid mbona umegeuza hapa jamvini kama mahali pakupigia debe cha cha mafisadi kwanini usiendeleze mchakato majimboni live kwenye majukwaa
 
Na Maggid Mjengwa,

“ One tall tree does not make a jungle”- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.
Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.
Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejindaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake. Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba, kitaangukia kaburini.
Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid,
Msamvu, Morogoro

Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.

Majjid Mjengwa- Nimekuwa nikifatilia post zako nyingi hapa JF lakini unaonekana kutoa post zako zikiionesha kuwa una mission flani you need to accomplish, sitaki kukukatisha tamaa juu ya mission yako lakini style unayoitumia haijificchi kwani unapo andika kuhusu jambo flani jaribu to PUT ALL FACTORS IN PERSPECTIVE kwani umekuwa ukilazimisha watu waamini unacho amini bila kufanya analysis ya kina na inayohitaji kupata facts zilizojaa hoja zilizojitosheleza.

Katika kuonesha huo upungufu wako mfano ulio utoa wa SPLM na JOHN GARANG sio hai kwani JOHN GARANG alikuwa na wasaidizi wengi sana na ambao walikuwa mstari wa mbele kuendeleza mapambano ya kijeshi na GARANG alikuwa symbol ya movement na kuwakilisha movement nje ya nchi na kisiasa zaidi, hata mazungumzo yaliyokuwa yanafanyika kuleta amani SUDAN YA KUSINI hayakuwa yanawakilishwa na JOHN GARANG PEKEE BALI JOPO LA wanaharakati kutoka SUDAN YA KUSINI, na hata baada ya Kifo cha John Garang hakuwa tabu kupata mlithi wake ambae ni SALVA KIIR, na akina Dr. Ann Itto, Gen. Dominic Dim Deng na hawa hapa chini ndo makamanda wa SPLA wanaoendeleza mapambano mpaka leo hii.

Current leaders of the Sudan People's Liberation Army:
  1. Gen. Salva Kiir Mayardit, Commander-in-Chief of SPLA
  2. Lt. Gen. Paulino Matip Nhial, Deputy Commander-in-Chief of SPLA
  3. Lt. Lt Gen. Nhial Deng Nhial, Minister for SPLA Affairs
  4. Lt Gen. James Hoth, Chief of General Staff
Hivyo sijakuelewa ulikuwwa na maana gani kutoa mfano huo, inawezekana huna facts za kutosha au una INSULT OUR INTELLIGENCY!

Na kwa Taarifa yako SALVA KIR amefanikiwa zaidi kuliko hata JOHN GARANG kwani muda si mrefu SUDAN YA KUSIN WATAPIGA KURA YA MAONI ITAKAYOAMUA HATMA YAO YA KUUNDA JAMHURI INAYO JITEGEMEA YA SUDAN YA KUSINI. Nadhani ulihitaji kufanya reseach kidogo tu kabla ya kutaka kuwalisha watu uongo ambao haujazingatia all facts na mfano usiokuwa hai.

Ningependa sana uwe unazingatia facts sio kuchakachua mifano ili tu uweze kuhalalisha unachotaka kuwasilisha, kwa hizo facts hapo juu ningekuomba uwe muungwani kwa kutuomba radhi au ku recycle your post.

Natanguliza shukrani zangu kwa kutujali.
 
hali kadhalika kila chama lazima kiwe na political icon au party flag bearer ambaye ana mvuto mkubwa wa kisiasa kuuliko mtu yoyote ndani ya chama chake, that was true kwa nelson mandela na anc, kenyata na kanu, ccm na nyerere, democrats na obama and still true now kwa chadema na dr slaa, sio kwambo umaarufu wa viongozi hao ulichochea utawala wa totalitarian bali kulikuwa na watu makini nyuma yao ambao walikuwa sio maarufu wanaofanya kazi kubwa ya kumpa support ili aendelee kubeba maudhui na ujumbe uliokusudiwa! So hilo ni swala la kawaida katika siasa za nchi mbalimbali duniani kijana wangu.
 
- Mti mmoja mrefu haufanyi msitu, ana maana Dr. Slaa peke yake hawezi kuongoza nchi anahitaji msaada ambao hana maana hana wengine, akiwa Mwanza Chadema nzima inakua huko, ndio maana ninasema waungane Wapinzani kama kweli nia yao ni moja yaani kutukomboa wa-Tanzania, na time ni sasa!

Es!
 
Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown
 
Mi sijaona tall tree wala jungle katika context hii Tanzania. Si chama twawala wala upinzani.

Those who can lead do not, those who do cannot.
 
Back
Top Bottom