Neno La Leo: Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

Maggid anashindwa kuelewa CHADEMA kinaendelea kukuwa kwa kasi ya ajabu, mijini pamoja na vijijini. CHADEMA ni chama makini, na ndio maana watu kama kina Maggid hawazungumzii vyama vingine kabisa, wao ni kumshambulia Dokta kila kukicha. Maggid lazima utambue ya kuwa CHADEMA kilikuwapo kabla ya Dokta na kitaendelea kuwapo kwa sababu ya SERA zake bora lengo la kumkomboa mtanzania.
 
Na Maggid Mjengwa,

" One tall tree does not make a jungle"- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.
Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.
Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejindaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake. Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba, kitaangukia kaburini.
Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid,
Msamvu, Morogoro

Brother Maggid, article nzuri sana mkuu!!! Nakubaliana 100% na yote uliyoyaandika hapa juu. Najua watu wameandika maneno mengi ya kejeli, lakini hilo lisikukatishe tamaa.
 
Kitu kikubwa ninachojifunza ndani ya hizi debate/discussions ni kuwa soon or later watu tutaanza kufikiri na kutenda nje ya mazoea. Fikra zinapojengwa na kutumiwa kwa usahihi zinaleta mabadiliko makubwa sana. Kule tulikotoka tulijisahau, tukawaacha watu wachache wawe wanafikiria mambo yote kwa ajiri yetu. Sasa hivi tumetengeneza matatizo makubwa kiasi kwamba hatuendi mbele kama Taifa. Ninafurahi kuona mwanga unaanza kuonekana taratibu. Siku za kudanganyana zimebaki chache na zinakaribia kikomo. Mwenye macho haambiwi ona!!

Ndahani,

Nakubaliana nawe, na uliyoyaandika yanatutaka sio tu tuanze kufikiri, bali tufikiri kwa bidii. Ahsante sana.
 
jmushi1,

..nimesoma kwamba kampeni za CUF na Prof.Lipumba zimepokelewa vizuri sana ukanda wote wa kusini mwa Tanzania.

..kwa upande mwingine, Prof makes a lot of sense katika mambo mengi anayoyazungumzia. he would have helped himself kama angeamua kujijenga kwanza kama mbunge kabla ya 2010.

..sasa, ukiweka mapenzi ya chama pembeni, ukasikiliza hoja kwa hoja, baina ya JK,Prof.Lipumba,na Dr.Slaa, naamini kabisa you will end up with a toss up btn Lipumba and Slaa.

..kwa upande wangu nadhani kura za Uraisi hazitatofautiana sana baina ya vyama vitatu CCM,CUF,na Chadema.

- Strong point bro! na ndio hasa Great Thinking!

Es!
 
Maggid anashindwa kuelewa CHADEMA kinaendelea kukuwa kwa kasi ya ajabu, mijini pamoja na vijijini. CHADEMA ni chama makini, na ndio maana watu kama kina Maggid hawazungumzii vyama vingine kabisa, wao ni kumshambulia Dokta kila kukicha. Maggid lazima utambue ya kuwa CHADEMA kilikuwapo kabla ya Dokta na kitaendelea kuwapo kwa sababu ya SERA zake bora lengo la kumkomboa mtanzania.

- Mkuu wangu strong, hoja nzito sana na ndio exactly tunayooiita Great Thinking.

Respect.

Es!
 
Ndahani,

Nakubaliana nawe, na uliyoyaandika yanatutaka sio tu tuanze kufikiri, bali tufikiri kwa bidii. Ahsante sana.

Mkuu huu ni ukweli uliowazi. Ukiangalia utaweza kutambua kuwa majority of Tanzanians hatufikirii kwa bidii(sio wote). Ingawa wakati BWM alisema watanzania ni wavivu wa kufikiri tuliona tumetukanwa, ukichakata aliyosema unaweza kufahamu kuwa BWM alikuwa sahihi. Mfano mmoja ni kuwa, pamoja na kuwa Lipumba ni asset kubwa sana kwa Tanzania, kuna mentality kuwa amelaaniwa kwa kuwa yeye ni mgombea wa CUF. Kuna mentality kuwa ukiwa CCM bila kujali wewe ni mbaya au mwizi kiasi gani, tayari umebarikiwa (japo hali hii inaanza kubadilika).

Ukiangalia utaweza kuona kuna elements za udini, uchama na udugu....utanzania unakuja mwishoni sana. Ukiangalia personalities za JK, Slaa na Profesa unaweza kuona profesa is there at the top, lakini kwa mentality ya kuwa yeye ni CUF, basi tayari amejiwekea doa. Pamoja na kuwa Slaa ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa Tanzania, still unaweza kuona baadhi hawaafikiani naye.

Kila mtu ameona perfomance ya serikali ya awamu ya nne, na kila mtu ameona perfomance ya CCM kwenye miaka hii mitano, i can not expect anything different from that hata kama wakipewa miaka mingine mitano. Unless there is a serious overhall in the leadership, kitu ambacho wanaokishikilia chama hawatakubali. Tena wakipewa mingine mitano itakuwa worse kwa kuwa they will have nothing to lose. Ingekuwa kwenye nchi ambazo majority wanafikiria kwa bidii sasa hivi hali ingekuwa tofauti sana. Tutakuwa tunajidanganya kama tukisema CCM imefanya kazi nzuri, tumeona hali ya sheria katika miaka mitano, tumeona mismanagement ya uchumi, inflation kwenda juu, hakuna kitu chochote significant ambacho tunaweza kusema tumekifanya katika miaka mitano iliyopita hakuna.. Chama kiko kwenye shambles, serikali ndio usiseme. Ukitaka kujua kama kweli tunafikiri kwa bidii au la, subiri matokeo ua uchaguzi.
 
Makubwa haya mimi ningemuomba Maggid atuletee kipande cha hotuba ya Mandela aliposema hivyo!.. maanake haiingii akilini kabisa. I can bet Mandela hakuwahi kusema hivyo....

Kaka umesema kweli nimejaribu kuu google Nelson Mandela Qutes zilozpo kwenye kumbu kumbuku sijafanikiwa kuipata hiyo aliyonukuu Maggid. Naamin mtu kama mandela quites zake na quotes alizoquotes watu wengine zinapatikana kirahisi
A good head and a good heart are always a formidable combination.

After climbing a great hill, one only finds that there are many more hills to climb.

Communists have always played an active role in the fight by colonial countries for their freedom, because the short-term objects of Communism would always correspond with the long-term objects of freedom movements.

Does anybody really think that they didn't get what they had because they didn't have the talent or the strength or the endurance or the commitment?

Education is the most powerful weapon which you can use to change the world.

For one to be free is not merely to cast off one's chains, but to live in a way that respects and enhances the freedom of others.

I cannot conceive of Israel withdrawing if Arab states do not recognize Israel, within secure borders.

I detest racialism, because I regard it as a barbaric thing, whether it comes from a black man or a white man.

I dream of an Africa which is in peace with itself.

I dream of the realization of the unity of Africa, whereby its leaders combine in their efforts to solve the problems of this continent. I dream of our vast deserts, of our forests, of all our great wildernesses.

I learned that courage was not the absence of fear, but the triumph over it. The brave man is not he who does not feel afraid, but he who conquers that fear.

If the United States of America or Britain is having elections, they don't ask for observers from Africa or from Asia. But when we have elections, they want observers.

If there are dreams about a beautiful South Africa, there are also roads that lead to their goal. Two of these roads could be named Goodness and Forgiveness.

If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart.

If you want to make peace with your enemy, you have to work with your enemy. Then he becomes your partner.

In my country we go to prison first and then become President.

It always seems impossible until its done.

It is better to lead from behind and to put others in front, especially when you celebrate victory when nice things occur. You take the front line when there is danger. Then people will appreciate your leadership.

Let freedom reign. The sun never set on so glorious a human achievement.

Let there be work, bread, water and salt for all.

......
endelea ksoma nyingine @ Nelson Mandela Quotes

quotes nyingine ya muhimu ni

No one is born hating another person because of the color of his skin, or his background, or his religion. People must learn to hate, and if they can learn to hate, they can be taught to love, for love comes more naturally to the human heart than its opposite.-Long Walk to Freedom

bado naitafuta hiyo quote tujue context yake kama mleta mada aliilewa vizuri .Isije akawa imetumika kama wanafunzi wa kiume tulivyokuwa tunatumia kifungu cha wakoritho 7 ktongoza wasichana shuleni . kifungu kinasema hivi
Peaneni msinyimane. Mwanamke hana amri juu ya mwili wake ....Iwapo mmekubaliana kwa faragha . .....
Sasa bila kuelewa context nzima unaweza kuwapotosha watu
 
Maggid, Jibu la hoja yako hakika umeiweka wewe mwenyewe uliposema haya:-

Ndugu zangu, Hii ni nchi yetu. Ni nchi yetu sote, kama Watanzania sisi ni ndugu. Nchi ni kama mama, hatuwezi kuchagua mama. Ndio maana tunaipenda nchi yetu. Inahusu Watanzania zaidi ya milioni 40. Kumchagua Mtanzania atakayepewa jukumu la kushika dhamana ya watu milioni 40 si sawa na kucheza ' ngoma ya lelemama'. Tuwe makini, na wakati mwingine si vibaya tukagombana kwa hoja.

Sasa kama ulikuwa na maana kwamba tufikirie kwa makini sana tunapomchagua mgombea kwani yeye ni sehemu tu ya msitu mzima (Watanzania) labda ningekuelewa lakini baada ya kusoma mfululizo wa mawazo yako hakika nilishindwa kabisa kuanisha mtiririko mzima.

Haya mawazo ya kufikiria kwamba Dr.Slaa anaweza kufa na Chadema wasiwe na mtu baada yake haihusu kabisa kwani ukikata mti mmoja ktk msitu hujaumaliza msitu bado utabakia msitu kwa maana ya Mti mmoja si msitu. Hivyo swala la kiongozi mmoja kati ya watu millioni 40 sii hoja kabisa ya kuzungumzia kwa mifano hiyo.
Na kibaya zaidi CCM wamesimama vibaya zaidi ya vyama vyote Kiukweli...

Yaani unayoyaombea yanawezekana kabisa kutokea CCM kwani hapa tulipo watu wanaomba dua kila siku ya MUngu..JK mgonjwa, Bilal Mgonjwa, Spika wa Bunge tunaambiwa Mzee Sitta hatarudi sasa - Hatuelewi hayo unayoyaombea kwa Chadema mbona yanatisha zaidi kwa CCM - Harufu ya Lowassa imetapakaa kila kona hata utabiri wa Mwanakijiji kuwa 2015 unaandaliwa kwa Lowassa kuchua madaraka inaonekana wazi kwamba unatengenezwa leo..Hivyo umakini unaoutaka kwa nini usizungumzie hili ambalo lipo kwa uhakika kabisa?
 
na mimi nimejaribu kuipitia hii mada kuanzia mwanzo mpaka mwisho, lakini kwa kifupi niseme dunia imebadilika kisiasa na siasa ya nchi moja haiwezi kabisa kulingna na ya nchi nyingine, huwezi kulinganisha Kenya ama South Africa na Tanzania, kila nchi inakuwa na siasa zake kulingana na mahitaji yao kwa sasa, tukizungumzia vyama kama TANU,KANU, ANC, zANU FRELIMO na vingine kama hivyo vilikuwa na ajenda, mifumo, misimamo na malengo yanayofanana AMABAYO NI UKOMBOZi, lakini sasa vyama vimebadilika majority wa ANC walingangania lazima sasa Raisi awe MZULU, kwa hiyo hapa ile itikadi ya chama cha ANC kuwa mtu wa kabila lolote anaweza kuwa raisi waliipindisha kwa maslahi ya hao Majority

KWa matatizo ya Tanzania sasa hayahitaji chama zaidi, yanahitaji MTU, system ya TAnzania ya vyama almost vyote zinafanana kimuundo na kimfumo kwa sababu labda vinatoka kwenye msingi mmoja (TANU, Nyerere, CCM)
nasema tunahitaji mtu kwa sababu Tanzania ni nchi iliyoweka kila kitu chake kwenye system, kinachokosekana ni usimamizi uliosahihi na uwezo binafsi wa kiongozi kujua lipi lianze na lipi lifuate, Tuchukulie mfano mdogo tu wa BW Magufuli, ni kwa nini huyu bwana akiwekwa kwenye wizara yoyote anaperfom tofauti na wengine, jibu ni kuwa yeye anafuata kilichokwepo kwenye miongozo ya wizara na katiba ya nchi bila nonsense yoyote

Tanzania sasa inahitaji Mtu ambaye atairudisha hii nchi kwenye utawala unaofuata sheria nakuweza kusimamia rasilimali za nchi ili kila mtanzania aweze kunufaika na kupata unafuu wa maisha, na hapa kwa kweli sio chama cha siasa chenye uwezo wa kufanya hivyo, bali ni MTU

SASA TUKIANGALIA TATHMINI RAHISI TU YA SASA, UTAONA CHADEMA NA CUF WANA SERA ZINAZOMLENGA MWANACHI MOJA KWA MOJA NA ZA CCM NI ZILE ZILE ZINAZOJULIKANA, LAKINI TUNAKUJA KUANGALIA NI NANI ATAKAYEENDA KUTEKELEZA HIZO SERA? (mTI MMOJA MREFU)

KWA MTAZAMO WANGU (niko tayari kurekebishwa)
1) CCM imekosa msimamizi na mtekelezaji wa sera zake, JK alipewa nafasi ya miaka mitano na ndio kingekuwa kipimo kizuri cha kupima uwezo wake wa kusimamia sera za chama chake na katiba ya nchi ikiwemo na utawala bora Kwa ujumla, hii nguvu yote anayotumia sasa kurudi madarakani ni alama anuwahi inayoonyesha kutokubalika kwake kwa kile alichokifanya kwa miaka mitanio iliyopita (tofauti na Mkapa ambaye hakukubaliaka sana mwanzo lakini alikuja kushinda kwa kishindo awamu ya pili), HAPA NAOMBA NISEME HIVI KISICHOKUBALIKA SASA SI CCM BALI NI MTU (JK), LAKINI KAMA WANGEsIMAMISHA MTU MAKINI TUNGEKUWA TUNAONGEA MENGINE
2) Pamoja na Matatizo yasiyo rasmi ya CUF ambayo kwa kiasi kikubwa yanaongelewa Chadema pia, Lipumba amekosa CV ya kiuongozi, ni msomi wa kweli, ni mtu anayejenga hoja za mantiki na ni mtu anayeongea kwa kufikiria, Tatizo kubwa ni kuwa Watanzania hawajaona impact yake kwenye siasa za Tanzania, hajawahi kuwa mbunge wala kuwa sehemu yoyote ambayo angeweza kusema na kuitetemesha serikali, kwa hiyo Lipumba amekuwa ni mgombea wa urasi wa CUF na wala sio wa Watanzania, namaanisha anaweza kupata kura nyingi za wanachama wa CUF , lakini chache sana za wasio wanachama wa CUF na sababu sio sana Chama bali ni kutofahamika kiutendaji.
3) Kwa upande wa Slaa, watu wamefunika yote ya Chadema, wanachoangalia ni MTU, Dk ategemei kura za wana Chadema pekeyake bali za hata wasio wanachama wa Chadema na sababu kubwa yeye ameonyesha misimamo na uthubutu wa hali ya juu ambao hata mgombea wa CCM (Raisi aliyemaliza muda wake) hana, na kwa sababu Watanzania sasa wanahitaji MTU wa kuwaongoza na kuwatetea ndio watu wapo tayari kwa lolote ili mradi waone mabadiliko

kwa hiyo ningependa kuweka wazi kwa ndugu Mjengwa kuwa siasa ya nchi moja haiwezi kuwa sawa na nchi nyingine yoyote kwa miaka hii , hatuna tena influence ya East na West, kila nchi inatengeneza siasa zake kutokana na matatizo yaliyopo, SIASA YA TANZANIA SASA NI MTU WALA SIO CHAMA
 
CHADEMA ni chama makini, na ndio maana watu kama kina Maggid hawazungumzii vyama vingine kabisa, wao ni kumshambulia Dokta kila kukicha. .

U realy do believe this??? Now I can understand makada wa CCM na vikorombwezo vyao.......
 
Omarilyas,

..sasa hiyo ni worst case scenario, tueleze basi na best case ikoje.

..ikiwezekana tueleze na 50-50 case scenario ikoje.

NB:

..second in charge wa Chadema anaweza kuwa rafiki yako Zitto Kabwe. why not??

Simple,

Another scenario:

President Dr Slaa, Vice President anaitwa nani vile? + Waziri Mkuu: Freeman Mbowe = Kikwete + Lowassa (Atleast these guys had more than atleast 30 years of understanding the politics of governance..and relevant education - economics and Development studies)

Scenario nyingine baadae kama ukihitaji
 
U realy do believe this??? Now I can understand makada wa CCM na vikorombwezo vyao.......
Mkuu wangu ebu nifahamishe kidogo..Najua fika vita yako na chama hiki cha Chadema ni Mbowe na wapambe zake, lakini itakuwa vizuri sana kama utaweza kunieleza udhaifu wa chama kizima kwani binafsi siamini kabisa kwamba matatizo ya Chadema ni Mbowe, mtu ambaye kakubali kuachia kiti cha Urais kumpisha Dr.Slaa anaye uzika kwa wananchi. Sasa kama una mapungufu ya Dr.Slaa twambie nasi tupate kujua lakini kama ni swala la Mbowe na Chadema hakika mimi siamini kabisa kama mtu mmoja anaweza kumiliki chama kizima ktk dunia ya leo.
 
Mkandara,

Wewe unampa benefit ya nini Omar, Jamaa kamlinganisha Slaa na Kikwete. Anamlinganisha Mbowe na Lowassa. Unadhani jamaa yuko serious? Omar kabadilika sana siku hizi. Alijificha kwenye kibanda cha ushauri wa kisiasa for a long lakini wachunguzi wa mambo tulimgundua zamani sana.

Omar ni kipenzi cha kudumu cha Kikwete. Alichukia sana kuona Slaa kakubali kugombea uraisi. Hizi chuki na matusi yote dhidi ya Slaa ni kwa vile Omar kaona kuwa Slaa ana nafasi kubwa ya kung'oa tonge toka kwa Kikwete.
 
Na Maggid Mjengwa,

" One tall tree does not make a jungle"- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.
Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.
Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejindaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake. Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba, kitaangukia kaburini.
Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid,
Msamvu, Morogoro

Maggid,

..kwanza hii mifano uliyotumia ina walakini kidogo.

..Frelimo hawakujua watafanya nini baada ya kifo cha Mondlane. kilichotokea baada ya hapo kilikuwa sawa na "mapinduzi baridi ya kijeshi." aliyekuwa makamu wa raisi wa Frelimo, Uria Simango, ndiye aliyepaswa kumrithi Mondlane, lakini aliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Samora Machel. Uria Simango alikuja kuuwawa pamoja na mkewe na mpaka leo haijulikani walipozikwa.

..kwa upande mwingine lazima tuwe makini sana na makada wa CCM wa miaka hii, pamoja na malengo yao ktk chama. naamini kwa dhati kwamba CCM imepoteza mwelekeo na kutekwa nyara na watu waliongia ktk siasa kwa nia ya kujitajirisha kwa njia zisizo halali.
 
Ha ha ha,

Yaani kabisa Omar unamlinganisha Slaa na Kikwete?

Angalao Kikwete ana guts za kuuacha Lowassa ajiingize kitanzini...vipi Dr Slaa ni lini ameweza kusimama mbele ya maslahi binafsi ya Mbowe????

Second, Kuhusu ujuvi ama uledi wa masuala ya Utawala nina uhakika asilimia 100 kuwa Kikwete anamzidi Dr Slaa. Ofcourse Kikwete ana advantage ya kupewa nafasi ndani ya mfumo kujifunza kwa muda mrefu lakini ukiangalia mapambano na sasa majigambo, vikwerombwezo na mikwara ya Dr Slaa, kimoja kiancho onekana ni kuwa hajatumia muda wake kujifunza vya kutosha namna serikali ama utawala unavyofanya kazi......Rejea suala la NUSU YA MAAFISA WA USALAMA WA TAIFA KU-REPORT KWAKE.....Ama lile la kuhusisha dili la matrekta kutoka India na kumhusisha Shimbo kama binafsi wakati ukweli ni kuwa ni shughuli waliyopewa jeshi ambalo miaka yote mnasema litumike katika maswala ya maandeleo haswa sasa wakati hakuna vita....Bado lile suala la mfumo wa kibenki wa TISS ambalo mlidai kuwa ni fedha zilizokuwa zikpelekwa Idara ya Usalama...na mengine mengi ambayo sitayataja hapa kwa maslahi ya maendeleo ya demokrasia nchi...
 
Back
Top Bottom