Neno gani ambalo ulishawahi kuambiwa dhahiri likakukatisha tamaa?

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Jul 25, 2022
208
191
Ukweli ni kwamba kuna maneno mengi sana ambayo yanatumika na watu mbalimbali hususani pale wanapotaka kumkatisha tamaa mtu mwingine.

Binafsi, kuna neno "Sio kirahisi hivyo kama unavyodhani" Hili ni neno ambalo limeachisha mawazo ya watu wengi kuhusiana na kujihusisha na jambo fulani.

Mfano, unaweza kuwa umefikiria kuanzisha biashara katika eneo fulani, lakini watu wengi watasema kuwa "kwa hilo eneo sio rahisi kama unavyofikiria kufanya biashara hiyo" Lakini ukweli ni kwamba endapo utalianza jambo hilo utagundua sio kama lilivyokuwa likizungumziwa awali kwa maana linaweza kuonekana jepesi zaidi.

Je! Ni neno gani lingine mwana Jamii Forum umewahi kulisikia au kuambiwa ambalo dhahiri lilikurudisha nyuma katika kutekeleza jambo lako?

Hamza Nsiha ~
 
Mie niliambiwaga na mdada mmoja humu kwamba "ningekupea ila tatizo ni ile business unafanya ya kuuza coffins"
 
Kuna mwaka mzee wangu alifariki sasa kuna ishu nikawa nafuatilia kwenye ofisi moja ya serikali nikaambiwa nikamuone boss mmoja nakumbuka jina lake ni shirima....alichonijibu yule mzee sintosahau japo ni more than 20 years ago. Na nilishamlaani sintomsamehe..nilitamani nikajiunge alshabaab nirudi kumuonesha show kwa kauli ile ya kudharau kifo cha mzee wangu na kunifukuza kama mbwa. Ukizingatia jinsi tulivyomuuguza mzee kwa mda mrefu na alivyoteseka. Siku hiyo nilirudi home maza akaniuliza feedback sikumjibu nikaenda kwanza kujifungia geto...badae nikamwambia tu maza ningekua na uwezo wa kupata bunduki leo ningetafuta...na hapo nilikua o level tu. Sometimes nikiona madogo wameingia kwenye makundi ya kigaidi siwalaumu sana. Life pushes them to the limit na hawaoni option sababu kila mtu kama kawatenga
 
Kuna mwaka mzee wangu alifariki sasa kuna ishu nikawa nafuatilia kwenye ofisi moja ya serikali nikaambiwa nikamuona boss mmoja nakumbuka jina lake ni shirima....alichonijibu yule mzee sintosahau japo ni 20 years ago. Na nilishamlaani sintomsamehe..nilitamani nikajiunge alshabaab nirudi kumuonesha show kwa kauli ile ya kudharau kifo cha mzee wangu
Leta story nzima Kaka.
 
"Hivi nelly ukipaangalia kwenu na kwetu unaweza kuwa na girl kama mimi"

Ilipelekea nika-fail mtihani muhimu sana shule ila mungu sio massawe demu ameolewa ila mimi ndio kama mume vile.

Kuna siku aliwahi kuniambia ile kauli anaijutia sanaa hata kama nilishamsamehe na kuahidi kunipenda mpaka kufa
 
Noma Sana!

Ungemjibu Ile ni nyumba yetu sio yangu. Na Ile ni nyumba yenu sio yako.

Subiri uone nyumba YANGU
 
Kuna kazi ya online nilikuwa naifanya, nina shoot short video namtumia client alafu nalipwa, sasa my GF akaniona, yeye akahisi kama ni upuuzi au nafanya comedy za TikTok tu kumbe mi nimetega mingo ya kupiga kama dollar 10 ivi chap chap.

Aliniambia kauli moja tu "UKIKUA UTAACHA", lile neno linanikera mpaka leo hii na baada ya hapo nilimuapia mbele yake hawezi jua ninafanya kazi gani, as long as anacho kitaka anapewa basi asitake kujua mishe zangu na hata akitaka hato kaa asikie nikimuambia kamwe.
 
Apo uliupiga mwingi mzeee kila mtu ashinde mech zakeee
 
Kuna mtu wangu wa karibu sana ilikuwa kila nikimshirikisha ninachotaka kufanya, ananiambia hutaweza, achana nalo.

Nilichoamua ni kuacha kumshirikisha. Na nilikuwa nafanikiwa. Tangu wakati huo nilijifunza kufanya kile ninachoamini binafsi kinawezekana bila kutegemea sana mawazo ya watu wengine.

Wengine utasikia wakisema hakuna aliyewahi kufanya hilo jambo,sidhani kama utaweza. Sasa unajiuliza wale walianzisha mambo ambayo leo tunawatumia kama mfano walianzaje? Akina newton, nyerere nk.
Ukitaka kufanya jambo unaloamini, wewe fanya bila kutegemea sana mawazo ya watu wengine!
 
Ukweli ni kwamba kuna maneno mengi sana ambayo yanatumika na watu mbalimbali hususani pale wanapotaka kumkatisha tamaa mtu mwingine.

Binafsi, kuna neno "Sio kirahisi hivyo kama unavyodhani" Hili ni neno ambalo limeachisha mawazo ya watu wengi kuhusiana na kujihusisha na jambo fulani.

Mfano, unaweza kuwa umefikiria kuanzisha biashara katika eneo fulani, lakini watu wengi watasema kuwa "kwa hilo eneo sio rahisi kama unavyofikiria kufanya biashara hiyo" Lakini ukweli ni kwamba endapo utalianza jambo hilo utagundua sio kama lilivyokuwa likizungumziwa awali kwa maana linaweza kuonekana jepesi zaidi.

Je! Ni neno gani lingine mwana Jamii Forum umewahi kulisikia au kuambiwa ambalo dhahiri lilikurudisha nyuma katika kutekeleza jambo lako?

Hamza Nsiha ~
Mimi sikumbuki ila nakumbuka Harmonize aliambiwa hajui kuimba arudi kijijini akalime na mpaka leo anatamba...so we shouldn't care au siyoo??
 
Ukweli ni kwamba kuna maneno mengi sana ambayo yanatumika na watu mbalimbali hususani pale wanapotaka kumkatisha tamaa mtu mwingine.

Binafsi, kuna neno "Sio kirahisi hivyo kama unavyodhani" Hili ni neno ambalo limeachisha mawazo ya watu wengi kuhusiana na kujihusisha na jambo fulani.

Mfano, unaweza kuwa umefikiria kuanzisha biashara katika eneo fulani, lakini watu wengi watasema kuwa "kwa hilo eneo sio rahisi kama unavyofikiria kufanya biashara hiyo" Lakini ukweli ni kwamba endapo utalianza jambo hilo utagundua sio kama lilivyokuwa likizungumziwa awali kwa maana linaweza kuonekana jepesi zaidi.

Je! Ni neno gani lingine mwana Jamii Forum umewahi kulisikia au kuambiwa ambalo dhahiri lilikurudisha nyuma katika kutekeleza jambo lako?

Hamza Nsiha ~
Nilikuwa nasoma FTC wakati huo, halafu kuna jirani yetu home, yeye alikuwa anasoma pale chuo cha ardhi Dar. Sasa wakati wa likizo tukakutana kitaa, mwana alikuwa third year pale ardhi na mimi ndo first year. Si akaniuliza nasoma kupata leve gani pale chuo ninaposoma. Nikamjibu FTC..!! AKANIAMBIA DAH..!! WATU SAA HII WANASOMA ADVANCED DIPLOMA NA DEGREE WEWE UNANGÁNGÁNA NA FTC..!! Aisee, alinipa hasira. Nikapambana mpaka nikamaliza FTC na kuingia FoE na kufanikiwa kupata BSc in Eng.

Wakati mwingine maneno makali tunayoambiwa na wanaotuzunguka, yanatutia nguvu ya kusonga, kwa maana ya kuwa-pruvu wrong walioyatamka
 
Nilienda interview fulani we acha Kuna jamaa alinicheka tukiwa kweny foleni jamaa alimaliza mwaka mmoja kunizidi mimi .... Sasa wakati tunaingia ananicheka kwa vile kaumbo kadogo then sina time na mtu kumbe yeye alikuwa na connection tayar ila huwezi amini leo niko nae ofisi moja .

Siku tunasaini mkataba dah!! Ananiangalia kwa chuki mi sina time nae roho mbaya tu.

Ila roho yangu imegoma kuwa na shobo nae mwaka wa pili na nusu hata namba nimefuta alinionyesha dharau sana kisa yeye ni bonge bong ivi.
 
" huna akili upeo wako mdogo...ndio maana mnafeli "

Maneno haya aliniambia class monta kwa sauti huku wadada rafiki zake pembeni wakicheka baada ya kuwa ktk mazungumzo na wana na yeye akiwepo baada ya mimibkusema mimi GS haina faida kwangu napambana nipate credit mbili tu niende chuo

Wakati huo ktk comb yangu ni yeye pekee aliyekuwa akifaulu na baadhi ya wadada wahuni wote chalii

Nikaja kumuonyesha kwanzia pre national respect ilikuja na necta nikwanyoosha Kombi nzima hadi hiyo gs niliyoidharau nikaifaulu yeye alikosa credit za chuo
 
'Kwa nini unaning'ang'ania wakati wanawake wapo wengi au wewe domo zege '

Siwezi sahau kashazalishwa watoto wawili sasa hivi yeye ndo anaisoma namba analalamika sijibu text Zake kwa wakati na simu zake sipokei maisha haya acha tu.
 
Kuna mwaka mzee wangu alifariki sasa kuna ishu nikawa nafuatilia kwenye ofisi moja ya serikali nikaambiwa nikamuone boss mmoja nakumbuka jina lake ni shirima....alichonijibu yule mzee sintosahau japo ni more than 20 years ago. Na nilishamlaani sintomsamehe..nilitamani nikajiunge alshabaab nirudi kumuonesha show kwa kauli ile ya kudharau kifo cha mzee wangu na kunifukuza kama mbwa. Ukizingatia jinsi tulivyomuuguza mzee kwa mda mrefu na alivyoteseka. Siku hiyo nilirudi home maza akaniuliza feedback sikumjibu nikaenda kwanza kujifungia geto...badae nikamwambia tu maza ningekua na uwezo wa kupata bunduki leo ningetafuta...na hapo nilikua o level tu. Sometimes nikiona madogo wameingia kwenye makundi ya kigaidi siwalaumu sana. Life pushes them to the limit na hawaoni option sababu kila mtu kama kawatenga
Nisamehe Sana kijana wangu
 
Back
Top Bottom