Biashara ya Jenga Uza ni nzuri, inakupa faida ya uhakika

Jun 10, 2023
54
76
Habari za muda huu wana jamvi,

Leo nawaletea faida na hasara za biashara ya kujenga nyumba na kuuza almaarufu kama “JENGA UZA”

Hii ni biashara nzuri sana kwa wawekezaji ambao hawataki stress kuubwaa ya uwekezaji na changamoto nyingi sana za uwekezaji. Kama tunavyojua changamoto za biashara za sasaivi unaweza ukanunua mazao kwa bei hii wakati wa kuvuna ukitegemea baada ya miezi mitano au sita bei ipande uuze then unakuta bei haijapanda kiasi cha kupata faida ya kutosha au ulioitegemea.

Lakini hii Biashara ya nyumba ni uhakika kabisa faida ni ya uhakika kama utazingatia mambo yafuatayo;

1. ENEO SAHIHI
Tunaposema eneo sahihi hapa namaanisha ni lazima uchangue ni sehemu gani ununue eneo kwaajili ya mteja wako. Huwezi ukachagua eneo sehemu ya changanyikeni wakati mteja wako utamuuzia nyumba ya milioni 150. Chagua location yakishua kweli.

2. UMILIKI WA ENEO
Lazima uhakikishe unanunua eneo lenye uhakika wa umiliki.

Hakikisha hununui eneo lenye mgogoro au usiuziwe eneo ambalo tayari kauziwa mtu mwengine. Nunua eneo ukiwa na uhakika wa umiliki wa eneo ili usipate hasara ya kusumbuana mahakamani na watu.

3. TRENDING YA ENEO
Jambo jengine ni kuzingatia status ya eneo.

Kuna status ya maeneo sasa hivi, Ndio mfano Goba sasa hivi kunaitwa ushuani. Kuna sehemu kuna mijengo mikali tuu. Maeneo kama mbweni, Bunju, Salasala.

Nunua eneo ambalo wanakaa watu wa hadhi fulani nzuri jenga nyumba utauza kwa urahisi.

5. BARABARA IPITIKE MUDA WOTE
Mtu akiacha lami basi barabara iwe fresh na iwe inapitika bila shida vipindi vyote vya mwaka. Mtu hawezi kulipa milioni 150 afu barabara wakati wa mvua inamlazimu kutumia bodaboda au hata wakati wa kiangazi kunakuwa na mashimo makubwa na yahatari kwa chombo chake cha usafiri.

6. KUFIKIKA KWA URAHISI MJINI
Tukumbuke hapa hatujui wateja wetu ni wapi.

Lakini cha msingi ni kuhakikisha unanunua eneo ambalo ni rahisi kufika mjini maana wateja wengi tunaassume wanafanya kazi mjini iwe Mbeya, Njombe, Mwanza, Dar nk.

Wateja wetu wengi watafanya kazi mjini na kuhitaji mahitaji.

7. NYUMBA NZURI KWA GHARAMA NAFUU
Hapa sasa ndio kwenye mzizi mkuu wa faida.

Tayari tushazingatia mambo muhimu yote kwenye ununuzi wa kiwanja, Sasa tunaanza ujenzi.

Lazima uhakikishe unajenga nyumba bora sana na yakisasa lakini lazima iwe ya gharama nafuu kabisa. Usije ukajenga nyumba kwa gharama kubwa ikakulazimu uuze kwa gharama kubwa zaidi.

Pia lazima uhakikishe jengo linakuwa bora kwasababu mteja anatoa pesa ya kutosha kwahyo epuka tamaa za kujenga jengo lisilo bora ili upate faida kubwa.

Kwa kufanya hivyo unaweza kupoteza wateja wengi sana maana biashara za jenga uza wateja wake huwa ni wakujirudia sana.

6. USIJENGE GHOROFA
Ehee usijenge ghorofa kama unataka kuuza.

Ghorofa ni kwaajili ya kupangisha tuu. Kuuza ni ngumu sana kwasababu maranyingi ghorofa ni dream house kwahyo dream house kilamtu huwa anataka iwe vile atakavyopenda yeye na pale atakapopenda yeye. Ghorofa huwa tunajenga kwa Oder maalum tuu.

7. FAIDA
Makadirio ya faida ya chini kabisa wakati unaanza kujenga mpaka unauza (ndani ya miezi minne unaanza msingi mpaka unauza nyumba).

Makadirio yake ni faida ya milioni 3 mpaka 5, Lakini ukikitana na watu makini na wazoefu faida yake ni sio chini ya milioni 10 kwa mwezi na kwa miezi minne ni milioni 40 (yaani nyumba unajenga na kuiuza ndani ya miezi minne na utakuwa na faida isiopungua milioni 40).

NB: Hakikisha unaweka vitu bora tuu kwenye nyumba yako.

Wateja wa kuanzia 150M wanachozingatia zaidi ni ubora na sio urembo tuu. Kwahyo hakikisha unaweka vitu bora kwanza.

Hivyo ni vichache sana kati ya vingi. Lakini hivyo ndivyo vya msingi kabisa. Kama uko interested nipigie au nifate whatsapp tuzungumze kwa kina faida na hasara za hii biashara.

Uweze kuwekeza kwenye biashara hii na hakika utaifurahia zaidi kama utapata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

+255 714 122 011
Tupo Goba Dar es salaam
Popote tunakufikia
Karibuni sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom