NEMC yatoa angalizo tabia ya wenye mabasi 'kuchimba dawa' na kutupa taka Ovyo porini wakati wa safari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkurugenzi wa Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amezungumza na waandishi wa habari na kusema:
IMG-20230831-WA0012.jpg

Moja ya jambo ambalo limekuwa likifanyika mara kwa mara kama mazoezi ni mabasi ya abiria, malori na magari yanayofanya safari ndefu kuwa na kawaida ya kusimama porini kwa lengo la kujisaidia (kuchimba dawa).

Amesema tabia hiyo imechangia kuchafua mazingira na kuwa kero kwenye jamii, kwani hali hiyo imekuwa ikifanyika hata katika vyanzo vya maji na hivyo wakati wa mvua uchafu unasambaa na kuharibu mazingira.

“Mbali na hapo inadharirisha hasa kwa wenye jinsi ya kile, kwani mara nyingi maeneo wanayofanya hivyo si rafiki kwa binadamu kunaweza kuwa na wadudu au Wanyama wakali.
IMG-20230831-WA0015.jpg

“Hivyo ni muhimu kushirikiana na Halmashauri mbalimbali kuhakikisha vyoo vinajengwa kila baada ya mwendo fulani kwenye maeneo ambapo Barabara Kuu zinapita, pia nipongeze baadhi ya mabasi ambayo yana vyoo ndani.

“Kuna watu wengi wanapitia wakati mgumu katika kujizuia wanapokuwa njiani wakati wa safari, wapo wanaoogopa kunywa maji kwa kuwa wanajua inaweza kumsumbua anapobanwa haja.”

Ameongeza kuwa elimu itolewe kwa abiria wanaotupa takataka mbalimbali barabarani wakati wa safari.

Kuanzia Wiki ijayo NEMC itatoa elimu kwa muda wa mwezi mmoja, baada ya hapo basi litakalokamatwa, litapigwa faini ya Tsh. Milioni tano.
 
Wajitahidi kujenga vyoo vya umbali mfupi!!! Wasafiri wagonjwa wa sukari kukojoa mara kwa mara, wengine machafuko ya matumbo.

Ukiachana na watoto pia kuna walevi kujisaidia mara kwa mara
 
Kuna kipindi walisema hayahaya ya vyoo kujengwa barabarani lakini sijui iliishia wapi japo kuna vyoo baadhi ya maeneo watu walijenga ila hakuna basi zinazosimama,wakaja na utaratibu sijui kila baada ya muda fulani gari isimame dk ishirini ila watu 'wachimbe dawa' sijui kama nayo inatekelezwa.
 
Hatari sana,hilo la kutupa takataka barabarani kuna siku nilinunua mhindi nikawa nakula,safari yangu ulikuwa ya kutoka Dar kwenda Mwanza,muda wa saa tatu tatu hivi Ndo tunatoka Dar nikawa nimemaliza kula mhindi wangu hivyo nikaaamua kutupa gunzi nje ya gari,Bwana wewe ule mwendo wa basi ,kwa chini kulikuwa na canter unakuja upande wetu,lile gunzi liliangukia kwenye kioo cha canter kwa mbele ,nilisikia mlio mkubwa wa vioo,sijui hali ya wale waliokuwamo kwa gari,sitarudia tena
 
Mkurugenzi wa Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amezungumza na waandishi wa habari na kusema:
View attachment 2734498
Moja ya jambo ambalo limekuwa likifanyika mara kwa mara kama mazoezi ni mabasi ya abiria, malori na magari yanayofanya safari ndefu kuwa na kawaida ya kusimama porini kwa lengo la kujisaidia (kuchimba dawa).

Amesema tabia hiyo imechangia kuchafua mazingira na kuwa kero kwenye jamii, kwani hali hiyo imekuwa ikifanyika hata katika vyanzo vya maji na hivyo wakati wa mvua uchafu unasambaa na kuharibu mazingira.

“Mbali na hapo inadharirisha hasa kwa wenye jinsi ya kile, kwani mara nyingi maeneo wanayofanya hivyo si rafiki kwa binadamu kunaweza kuwa na wadudu au Wanyama wakali.
View attachment 2734502
“Hivyo ni muhimu kushirikiana na Halmashauri mbalimbali kuhakikisha vyoo vinajengwa kila baada ya mwendo fulani kwenye maeneo ambapo Barabara Kuu zinapita, pia nipongeze baadhi ya mabasi ambayo yana vyoo ndani.

“Kuna watu wengi wanapitia wakati mgumu katika kujizuia wanapokuwa njiani wakati wa safari, wapo wanaoogopa kunywa maji kwa kuwa wanajua inaweza kumsumbua anapobanwa haja.”

Ameongeza kuwa elimu itolewe kwa abiria wanaotupa takataka mbalimbali barabarani wakati wa safari.

Kuanzia Wiki ijayo NEMC itatoa elimu kwa muda wa mwezi mmoja, baada ya hapo basi litakalokamatwa, litapigwa faini ya Tsh. Milioni tano.
Hao waandishi au wasanii wa bongo muvi? Mbona hawafanani na fani yao.
 
Screenshot_20230902-014721_Lite.jpg

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetangaza kuwachukulia hatua ikiwemo kuwapiga faini hadi ya shilingi milioni tano Madereva na Abiria watakaojisaidia maarufu kama ‘kuchimba dawa" kwenye maeneo yasiyo rasmi baada ya mwezi mmoja wa kutoa elimu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr. Samuel Gwamaka ambaye ameziomba Halmashauri na Wajasiriamali kutumia changamoto hiyo kama fursa ya ujenzi wa vyoo ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

"Tutaoa hii elimu kwa muda wa mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja tutaanza kuchukua hatua tutakapokuta kwamba kuna basi lipo porini Watu wanachimba dawa tutatoa motisha kwa yule ambaye atakuwa anatutumia picha, wewe piga picha namba za hilo basi, piga picha ya ushahidi angalau Watu wanachimba dawa halafu tuletee sisi kama Baraza huyo mwenye Basi tutashughulika naye kwanza kwa kumpiga faini isiyopungua milioni tano”.

“Pia inaweza kuhusisha kwa kumnyang'anya leseni ya kuendesha Mabasi lakini adhabu zinaweza kwenda kwa pamoja kwahiyo kuanzia Oktoba 2, 2023 hatutegemei kuona basi linachimba dawa” ——— Dr. Gwamaka. #MillardAyoUPDATES
 
Nakumbuka zamani kabla sijampokea Yesu, tulikuwa tunasafiri kwenda ziara ya kanda ya ziwa na rafiki yangu.

Akasema tukalale jirani na stand, basi tukapata Lodge mitaa ya Ubungo maziwa ina bar.

Ikawa ni pombe na kitimoto. Alfajiri safari, aisee niliumwa na tumbo, namshukuru Mungu sikuumbuka, ila tulipoingia Msamvu, nilipitilizia chooni.

Nilihara hadi basi likaniacha. Nikalifukuzia na bodaboda nikakuta wananingojea mizani.

Ila swala la kuchimba dawa tusizuiwe, hawa vigogo wanaotoa matamko wao wanasafiri na ndege, choo ndani na muda mfupi wa safari ndio maana wamesahau shida anazopata msafiri wa basi
 
View attachment 2736136

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetangaza kuwachukulia hatua ikiwemo kuwapiga faini hadi ya shilingi milioni tano Madereva na Abiria watakaojisaidia maarufu kama ‘kuchimba dawa" kwenye maeneo yasiyo rasmi baada ya mwezi mmoja wa kutoa elimu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr. Samuel Gwamaka ambaye ameziomba Halmashauri na Wajasiriamali kutumia changamoto hiyo kama fursa ya ujenzi wa vyoo ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

"Tutaoa hii elimu kwa muda wa mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja tutaanza kuchukua hatua tutakapokuta kwamba kuna basi lipo porini Watu wanachimba dawa tutatoa motisha kwa yule ambaye atakuwa anatutumia picha, wewe piga picha namba za hilo basi, piga picha ya ushahidi angalau Watu wanachimba dawa halafu tuletee sisi kama Baraza huyo mwenye Basi tutashughulika naye kwanza kwa kumpiga faini isiyopungua milioni tano”.

“Pia inaweza kuhusisha kwa kumnyang'anya leseni ya kuendesha Mabasi lakini adhabu zinaweza kwenda kwa pamoja kwahiyo kuanzia Oktoba 2, 2023 hatutegemei kuona basi linachimba dawa” ——— Dr. Gwamaka. #MillardAyoUPDATES
MKURUGENZI HOHEHAHE

La MASPIKA kwenye mabaa linekushinda umehamia huku....unataka watu WAJIHARISHIE..!!!!!!
 
Hawa viongozi wanatuchokonoa, wanatutafuta ubaya, hawajakoma tu kwenye bandari?

Abiria wa Kigoma uwanyimwe kuchimba dawa... ahahahahahhaaaaa

Patachimbikaa
 
Back
Top Bottom