Mabasi matano yazuiliwa kuendelea na safari Mbeya kutokana na changamoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988

bc331811-56e1-4cd9-a87f-4c3fd2a02ed3.jpeg
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Kikosi cha usalama barabarani limeyazuia mabasi matano ya abiria katika Stendi kuu Jijini Mbeya kuendelea na safari baada ya kukutwa na changamoto katika mifumo mbalimbali.

Akizungumza mapema Desemba 26, 2023 Mwanasheria Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Deus Sokoni baada ya kuendesha zoezi la ukaguzi wa magari, upimaji wa kilevi na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abiria katika Stendi hiyo amesema, jumla ya mabasi 58 yamekaguliwa ambapo kati ya hayo mabasi matano yalikutwa na changamoto katika mifumo hivyo kuzuiliwa.

Ameyataja mabasi hayo kuwa ni, Kampuni ya Turu Best, Isamilo Express, Arusha Express, Msigwa na Ahmed yanayofanya safari za masafa marefu kwenda mikoa mbalimbali nchini.
94275aca-db64-434a-885c-d4652617e98f.jpeg

4f0e69f3-6bba-4da5-a81b-971e8adab08f.jpeg
"Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kama vile mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) limepewa mamlaka ya kuzuia chombo cha moto kuendelea na safari pindi linapofanya ukaguzi na kubaini changamoto ikiwemo ubovu na hitilafu katika mifumo ya chombo hicho" alisema Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Sokoni.

Aidha, Afisa leseni kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) ndugu Amani Masuwe amesema kuwa, wamefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha abiria waliokuwa wanasafiri na mabasi yaliyozuiliwa wanapata usafiri mwingine na wengine kurudishiwa nauli zao ili kufanya utaratibu wa safari kwa siku nyingine.

Naye, Balozi wa usalama barabarani Mkoa wa Mbeya ndugu Yonna Mleka amepongeza zoezi la ukaguzi wa mabasi unaofanywa na Jeshi la Polisi na kuwataka madereva kujenga utamaduni wa kufanya ukaguzi wa magari yao ili kuepuka usumbufu kwao na kwa abiria pamoja kuepuka madhara mengine yanayoweza kuwapata kutokana na kutofanya ukaguzi.
 
Kwanini polisi na LATRA wasianzishe mabasi yao tuone watakavyokuwa njema?

Mwendokasi si hao hapo na ukiritimba wote? Kumbe iko vipi? Mengine yao haya ni uonevu tu.
 
Back
Top Bottom