NEMC ingieni mtaani mfanye jambo, kuna watu binafsi wanapiga kelele kuliko hata huko kwenye kumbi za starehe

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Uchafuzi wa mazingira wa kelele ni moja ya kero kubwa ambazo zipo mitaani kiasi kwamba imeonekana kama ni sehemu ya maisha hasa ya wale wananchi wa kawaida mitaani.

Nitoe histori kidogo, mtu anaposema kelele nina uzoefu wa kuwahi kupitia ker kama hiyo sitaisahau.

Nilikuwa naishi mitaa ya Sinza nikiwa bachela, kuna mwamba mmoja akahamia jirani na nyumba ninayokaa mimi, madirisha ya vyumba vyetu yalikuwa karibu, sasa jamaa ilikuwa ikifka wikiendi au usiku anaporudi anafungulia muziki kwa sauti ya juu kama yupo disco.
Snapinsta.app_346044414_220538504025963_1530617249642071483_n_1080.jpg

Ilikuwa ni kero hasa, yaani jamaa alikuwa hajali kama kuja mgonjwa ndani a muda wa kupumzika, yeye anakita muziki tu kwa sauti ya juu tena alikuwa na spika kubwa kiasi.

Majirani wote walimlalamikia lakini mwamba hakujali, na kibaya zaidi mwenye nyumba hakuwa anaishi mitaa hiyo, hivyo hakuwa sehemu ya watu waliokuwa wakipata kero ya kelele.

Mimi ambaye nilikuwa jirani yake nilikuwa napata tabu sana kuna wakati hata muvi ililazimika niangalie kwa kutumia earphone.

Kuna siku nadhani alikuwa na mgeni mtu mzima, sikumbuki kama ni mama yake au bosi wake au ndugu yake flani hizi, ilikuwa Jumamosi ametembelewa, walikuwa wageni wawili na walionekana ni watu ambao alikuwa anaheshimiana nao.

Hatukusikia mziki wowote wala kelele walipowasili watu hao.

Nilichofanya nikachukua Spika zangu mbili ambazo nazo zilikuwa kubwa ila siyo kama zake, nikazibana dirishani kwangu, sehemu ambayo inapakana na dirisha la kwake.

Nakumbuka niliweka CD ambayo ilikuwa zile zenye nyimbo nyingi (MP3) kisha nikafungulia muziki kwa sauti ya juu kabisa, kiasi kwamba nikajua lazima iwe kero kwa wale wageni wake kwa kuwa hawajazoea.

Ilikuw ani mida ya saa tano asubuhi, baada ya hapo nikafunga mlango na kuondoka nikiacha muziki unaendelea kwa sauti ya juu.

Taarifa nilizozipata baada ya kurudi ni kuwa nasikia jamaa alikuja kugonga akaambiwa sipo, sijui alitaka nini hilo sijui na nilirudi usikuu.

Niishie hapo, lengo ni kuonesha kuwa NEMC inatakiwa kuingia hata mtaani pia, kuna binafsi ambao wao hawamiliki kumbi za starehe wala nini lakini wanachafua mazingira mtaani kwa kiwango cha juu.

NEMC fanyeni kitu mtaani, inawezekana kelele za mtaani zinawaumiza wngi zaidi kuliko hata hizo za kwenye kumbi za starehe.
 
Sheria zipo ila kama zikifuatwa mbona watu watashika adabu
Tatizo la mwafrika anafanya kitu kwa kukomoa halafu baada ya kumalizana na adui wanatulia tena

Hawa kama wanafuata sheria wangezifanya kila siku ila wana lao tu na usikia zoezi limesitishwa

Si unaona Bungeni Msukuma kaanza kupinga akiwa anajua fika sheria Bunge ndio lilipitisha ila kwa kuwa wana maslahi na hizo Bar wameanza kunyanyua midomo


Sheria zetu huwa ni za siku mbili tu
 
Japan mtu simu yake ikiita kwa nguvu (kwa bahati mbaya tena) kwenye eneo la watu wengi, atainuka na kumuomba msamaha kila mtu

Njoo huku sasa 🤣
 
Na hasa saluni za kike" yaani huko ni umbea tu wanachoongea ni vikoba na mizagamuo,Kwa tafiti tu nlivyofanya hata sabufa hawaweki kama saluni za kiume ili umbea waupige vizuri.Na hili pia mkalitazame
 
Back
Top Bottom