NEC ya dharura Dodoma kishindo gani?

Kwahiyo raisi anaweza kuahirisha ziara kwaajili ya chama/ kukiwa na emergence issue kwenye chama na hawezi kuhairisha safari/ziara kukiwa na emergence issue inayowagusa watanzania ? (refer mafuriko, mgomo wa madaktari etc)

Usiulize makonzi polisi.
Sisiemu siku zote wanaweka maslahi ya chama mbele, ya Watanzania wote nyuma. Ona hata bungeni, suala la posho zao wanataka lushughulikiwe kwa dharua, mjadala wa kuokoa mgomo wa madaktari hawataki kuusikia. Zero kabisa
 
hakuna cha katiba hapo bro. ni kujipanga sawa kwani huoni kuwa sasa wabunge wa kujivua gamba wameanza kuasi? wanapinga hoja za wakubwa wao, wanataka kuweka mikakati ya kujifanya si wa TZ kumbe hakuna kitu-ni wafamaji hao hawaishi-----
 
Tanzania itaendelea bila ce-ce-m, kwani hawana jipya wako tayari kumwaga damu ili wapate kuishi na kuendelea kuwepo madarakani
 
Rais jk, ameitisha mkutano wa dharura wa nec mjini dodoma utakaofanyika tar 12 feb, naye nape amekiri uwepo wa mkutano huo na kusema lengo ni kujadili katiba mpya ya ccm.

hele ya hewa sio nzuri mkuu
 
Good observation. Hilo suala la katiba halina udharura wowote, kwa nini ameliitishia NEC ya dharura? Kuna dharura zilizopo, lakini amenyamaza kimya

Mkuu hiyo issue ya Katiba ni pana sana. Kwanza ujue hata uvuaji gamba ulielezwa utatelelezwa kwa Katiba mpya kwa maana Kamati ya Usalama na Maadili inapewa nguvu zaidi za kufanya maamuzi bila kupitia vikao vya CC na NEC mradi tu viwe na ushahidi wa kutosha na wa kisheria. Lakini pia, ni lini CCM wakawa na ajenda nzito wakaiweka hadharani kama si kuiweka kwenye "mengineyo", ama kwenye "hali ya kisiasa" na hapo sasa wewe kabla ya kikao utajuaje hayo "mengineyo" ya Mwenyekiti na timu yake ama "hali ya kisiasa" ina mipaka gani!!! Kwa ujumla tusubiri tuone maana hii ngonjera ya maamuzi ya NEC na mafisadi ilianzia Butiama, na sote tukakimbilia huko, lakini tukarudi na porojo kibao, sasa leo tuone kitakachotokea. Butiama walijadili Richmond na Meremeta, lakini iliishia wapi? Tusubiri tuone.
 
Hi Friends, habari toka ndani ya Chama ni hizi:Hakuna lolote, hakuna chochote - ni maandalizi ya Valentine day na Harusi ya Arumeru! Mkutano wa dharura ni tarehe 12 - 13 Feb, then siku yenyewe ya rangi nyekundu. Watu kujinafasi bwana!
 
Karibu JF, Lakini mkuu amaisharudi from Finland?
 
Kiukweli lengo la kikao hicho sio kujadili katiba ya CCM, hoja ya kujadili katiba ya CCM sio hoja ya kidharura kihivyo!.

Lengo la kikao hicho ni ku practice Party Supremacy over the government!. Baada ya ile kanuni ya chama kushika hatamu kufutwa, kwa sasa taifa liko katika hali tete ya mgomo wa madaktari, JK ambaye ndiye mkuu wa the executive alitakiwa awe amesha intervene tangu hajaenda Davos!. Akiwa Dovos akatoa maelekezo kwa Pinda kufanya alichokifanya, aliporudi tuu hii ndio ingekuwa priority no.1 kudeal nayo ikiwemo kufanya maamuzi magumu lakini due to his weakness hakufanya lolote!.

The weak are always scared, hivyo anaitisha NEC ya CCM ili kupata baraka za maamuzi makubwa anayopanga kuyafanya ikiwemo kulivunja baraza la mawaziri au kufanya mabadiliko makubwa!.

Mkuu siku zote nasema tuna weakness kubwa Tanzania, na tunazidi kuireinforce. NI kwanini Rais ashughulikie mgogo wa madaktari wakati kuna katibu Mkuu wizara ya afya, waziri wa afya, waziri Mkuu na wengine wengi kabla ya rais? What if inatokea migomo 30, madereva, manesi, walimu, wanafunzi, polisi, wanajeshi etc etc?? Kwanini tusiwe na mechanism ya kudea na issues kama hizi?

Kuna maamuzi gani magumu na yenye maana ambayo JK anaweza kuyafanya at this point of his presidency?Unajua style ya JK kuendelea kudivert attention ni kucreate migawanyo ndani ya NEC, na yeye kuwa part ya makundi yote. Make up ya NEC si nzuri, kuna wachovu wengi ambao hawawezi kumchallenge rais na kukichallenge chama kiwezie kuongoza vizuri zaidi.

Kimsingi Rais, na Waziri Mkuu wanatakiwa kushughulikia mambo makubwa zaidi na sio mambo ya migimo, kuna issues kubwa zaidi hapa Tanzania zaidi ya mgomo.
 
Nimelitazama sana baraza la mawaziri na utendaji kazi wake, maajabu manaibu waziri ndio wenye uwezo mkubwa sana kuliko mawaziri wenyewe sielewi kwa nini JK kafanya hivi. Halafu kama walivyosema waliotangulia Aggrey Mwanri huyu jamaa nilimpitisha siku nyingi sana ni mchakazi lakini kafungwa miguu yake. Nadhani yeye anafaa sana kuchukua nafasi ya PM ili aweze kulitumikia taifa ipaswavyo lakini najua haitawezekana kwa sababu tu yeye na EL picha haziendi..
 
Nakubaliana na wewe juu ya Mwanri kuwa waziri mkuu. Lakini si inabidi awe waziri kamili kwanza au? Kwani Waziri Mkuu anatokana na wabunge wa majimbo lakini pia ni lazima awe na uzoefu, at least in practice katika siasa za Tanzania, atokane miongoni mwa wajumbe wa baraza la mawaziri; manaibu mawaziri sio wajumbe wa baraza la mawaziri. Nje ya Nyerere pengine na kawawa, hakuna waziri mkuu mwingine aliyetokana na ubunge peke yake au ubunge na unaibu waziri.
Otherwise miongoni mwa waziri waliopo sasa, magufuli angefaa sana katika hiyo nafasi lakini wakubwa hawampendi huyu mtu for some reasons. Sitta nae angeimudu nafasi hiyo vizuri. Wengine waliobakia kwa kweli sioni kama wataleta jipya. Hata kwenye nafasi zao za uwaziri, wengi wanapwaya kama ulivyosema. Sijui kwanini JK katika miaka yake saba ya Urais amekuwa na tabia ya kuteua watu wa ajabu kabisa katika nafasi za uwaziri na kuacha wabunge wengi tu wenye uwezo mzuri wa kumudu nafasi hizo. Rais ana uwezo wa kuteua watu kumi kuwa wabunge, na maana ya sheria hiyo ni kumpa rais nafasi ya kuteua watu anaodhania wanaweza kuwa mawaziri wazuri wa kumsaidia lakini kwa bahati mbaya hawakupata nafasi ya kuwa wabunge. Kuna watu wengi wenye experience huko private sector, na pia makatibu wakuu ambao angeweza kabisa kuwaondoa huko na kuwapa uwaziri, ambao wangefanya kazi nzuri sana.
 
Mwanri anafaa sana,,

Kweli ninyi magamba,uwezo wenu wa kusoma uwezo wa mtu ni zero,au ni sura anayoji mascarade akijibu pale bungeni,yule msanii tu,mjaja mjaja kwa sababu hata wanaomuuliza maswali ni mapimbi tu wa akili,fuatilia vizuri anafanya maigizo tu anapojibu,hayupo katika vichwa
 
Mara kadhaa Jk anatumia fursa ya viongozi wengi wa CCM kuwa Dodoma kufanya vikao vya chama. Sidhani kama ni mkutano wa dharura.

inawezekana.....

nadhani ni jitihada za kupunguza gharama za kuwakusanya hao watu na kuwalipa posho za usafiri na mengineyo...hapo anakuwa ameua ndege wawili kwa jiwe moja.......very clever!!!!!
 
Nakubaliana na wewe juu ya Mwanri kuwa waziri mkuu. Lakini si inabidi awe waziri kamili kwanza au? Kwani Waziri Mkuu anatokana na wabunge wa majimbo lakini pia ni lazima awe na uzoefu, at least in practice katika siasa za Tanzania, atokane miongoni mwa wajumbe wa baraza la mawaziri; manaibu mawaziri sio wajumbe wa baraza la mawaziri. Nje ya Nyerere pengine na kawawa, hakuna waziri mkuu mwingine aliyetokana na ubunge peke yake au ubunge na unaibu waziri.
Otherwise miongoni mwa waziri waliopo sasa, magufuli angefaa sana katika hiyo nafasi lakini wakubwa hawampendi huyu mtu for some reasons. Sitta nae angeimudu nafasi hiyo vizuri. Wengine waliobakia kwa kweli sioni kama wataleta jipya. Hata kwenye nafasi zao za uwaziri, wengi wanapwaya kama ulivyosema. Sijui kwanini JK katika miaka yake saba ya Urais amekuwa na tabia ya kuteua watu wa ajabu kabisa katika nafasi za uwaziri na kuacha wabunge wengi tu wenye uwezo mzuri wa kumudu nafasi hizo. Rais ana uwezo wa kuteua watu kumi kuwa wabunge, na maana ya sheria hiyo ni kumpa rais nafasi ya kuteua watu anaodhania wanaweza kuwa mawaziri wazuri wa kumsaidia lakini kwa bahati mbaya hawakupata nafasi ya kuwa wabunge. Kuna watu wengi wenye experience huko private sector, na pia makatibu wakuu ambao angeweza kabisa kuwaondoa huko na kuwapa uwaziri, ambao wangefanya kazi nzuri sana.

Kama wewe ni weak ukichagua mtu strong utaonekana weak zaidi. Ili kuonesha kuwa wewe ni strong kati ya ma-weak inabidi uchague the weakest. Tuna tatizo kubwa sana na katiba hapa Tanzania, za vyama vyetu vya siasa(CCM,CHADEMA, CUF , TLP etc) na mbovu zaidi ni ile ya Jamhuri.

Kimsingi rais anaweza kumchagua mtu anayempenda au anayetaka awe mkuu wa mkoa, mkuu wa Wilaya, waziri, naibu waziri au mkurugenzi kwa sababu anazopenda na asiulizwe au asipingwe. Hakuna system inayochagua mtu anayefaa na anayestahili. Kama mtu akifaa basi ni bahati tu, na sio kutokjana na kutaka iwe hivyo. Hatuna system inayochagua watu kwa merit, isipokuwa tuna mtu anayechagua watu kwa preferances zake mwenyewe, at least in Practical.

Tunatakiwa tuwe na guidelines za kisheria za kufanya teuzi ziwe based on merit, na zisiwe solely or mainly based on politics and technical know who. Kwa sasa kuna watanzania wenegi sana wenye uwezo wa kufanya kazi amabazo zamani zilikuwa ngumu. Wengine hawataki kuingia kwenye ujinga wa kudhalilishana na wahuni wakati wa kugombea ubunge au nafasi za kisiasa, hawataki ujinga kama uliopo sasa hivi kwenye siasa zetu. Tunatakiwa tuwe na proper mechanisim ya kuaccomodate watu kama hawa. (sio kusema Rais ana nafasi kumi za kuteua wabunge).

Ukiangalia chaguzi zetu zilizopita utaona kuwa kuna mtu smart, visionary, capable na energetic, lakini ameachwa na kuchukuliwa corrupt, mwizi, mbabaishaji na useless kwa Tanzania. System kama hii inawakimbiza baadhi ya watu wanaofaa.

The point here is, our system is broken, we need a smart person to start fixing it. So far we do not have this person.
 
Fukuza mafisadi CCM ifufuke kwani tunakoelekea wizi wa kura ni mgumu, samawani JK ni ushauri wangu wa bure tu.
 
Fukuza mafisadi CCM ifufuke kwani tunakoelekea wizi wa kura ni mgumu, samawani JK ni ushauri wangu wa bure tu.

ndio mawazo na ushauri wa wengi, vinginevyo hakuna haja ya kuendelea kuimba wimbo wa mafisadi na *******. Tulianza na Butiama na Dodoma mara kibao, lakini hakuna mpya. Hii ni nafasi ya mwisho.

Kulikoni la jana limeandika:

Kikwete kuwabana

waasi CCM Dodoma

.Mafisadi washitukiwa kutaka Uenyekiti Taifa

.Wastaafu wataka hatua za haraka zichukuliwe

CHAMA cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wakie Rais Jakaya Kikwete, kinajipanga kuzima uasi unaopangwa kufanywa na baadhi ya wanachama wake wenye uchu wa madaraka, imefahamika.

Habari za ndani ya serikali na CCM zinaeleza kwamba, tayari Rais Kikwete ameshajulishwa kuhusu kuwapo kwa mkakati mzito wa kukivuruga chama hicho tawala na amejipanga kuchukua hatua.

Kwa mujibu wa habari hizo, kikao cha dharura Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho mwishoni mwa wiki hii, pamoja na mambo mengine nyeti kinaweza kujulishwa kuhusu hali hiyo.

Ofisa Mmoja Mwandamizi wa Serikali ameliambia KULIKONI kwamba viongozi wawili wastaafu wamemkabili Rais Kikwete na kumshauri kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo.

"Wazee (anawataja majina) wamemuendea Rais na kumwambia achukue hatua maana nchi sasa inayumbushwa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka, vinginevyo hali itazidi kuwa mbaya na hata kuweza kufanya uasi ndani ya chama," anasema mtoa habari wetu huyo.

Taarifa zinaeleza kwamba, baadhi ya wanasiasa wanahusishwa moja kwa moja na matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa ikiwamo migomo na kukwama kwa baadhi ya huduma muhimu, ikiwa ni mbinu za kumhujumu moja kwa moja Rais Kikwete.

"Wamekuwa wakiwatumia watendaji ndani ya serikali na ndani ya chama na hata vyama vya upinzani kumhujumu Kikwete na ajenda yao ya kwanza ni kuibua mjadala kwamba ameshindwa na kuanza na kutaka kutenganisha kofia za Uenyekiti na Urais, hoja ambayo wameanza mkuda mrefu kuijenga na kutaka kuiingiza kwenye vikao vya CCM vya mwaka huu," anaeleza na kuendelea;

"Wakajifanya ni wajanja na kujificha nyuma ya wazee, ambao waliwaendea na kuwaomba wachukue nafasi ya Uenyekiti, na ndipo wakaona sasa Rais Kikwete amezidi kuwa mpole, hali ambayo waliona si njema kwa mustakabali wa Taifa," anaeleza mtoa habari wetu.

Hata hivyo, vikao cha Kamati Kuu ya CCM na NEC vinaelezwa kujadili mabadiliko ya Katiba ya CCM, lakini pia vinatarajiwa kujadili hali ya nchi ikiwamo mgogoro wa madaktari na serikali na ule wa wabunge na serikali, na yote ikihusiana na masuala ya posho na misuguano kati yao na serikali ambayo inakabiliwa na hali mbaya ya kifedha.

Wabunge wanapigania kupanda kwa posho kutoka Sh 70,000 hadi Sh 200,000, wakati madaktari wanataka kupandishiwa kutoka Sh 10,000 wanazolipwa sasa na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi. Wabunge wameingilia kati mgogoro wa madaktari na wamekutana nao jijini Dar es Salaam, katika vikao ambavyo wabunge hulipwa posho na gharama za kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam.

Vyombo vya habari vimemnukuu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisema kwamba vikao vya sasa ni vya kujadili mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya chama hicho, mabadiliko ambayo yanalenga kukirudisha chama hicho kikongwe kwa wananchi badala ya sasa kuwa mikononi mwa wenye fedha.

Nape alisema leo kutakuwa na kikao cha Sekretarieti ya chama hicho itakayokutana mjini Dodoma na baadae kikao cha Kamati ya Maadili kabla ya kikao cha Kamati Kuu, vikao vitakavyofanyika mwishoni mwa wiki hii kabla ya NEC.

CCM inatarajia kufanya chaguzi katika ngazi zote mwaka huu na mabadiliko hayo ya Katiba yatahusu pia mchakato mzima wa chaguzi hizo, lakini pia yatahusu udhibiti wa maadili ya wanachama wanaotarajiwa kuwania nafasi mbali mbali ndani ya chama hicho na watakaowakilisha chama katika chaguzi za dola.

Katika sherehe za kuadhimisha miaka 35 ya CCM jijini Mwanza, Rais Kikwete, alisisitiza uamuzi wa chama hicho kujisafisha katika ngazi zote, kwa nia ya kurudisha hadhi ya chama mbele ya jamii.

Alisema katika vikao vya NEC vilivyopita, chama hicho kiliazimia kujisafisha katika utaratibu uliofahamika kama 'kujivua gamba' na kwamba uamuzi huo hauhusu viongozi wa taifa pekee bali hata ngazi ya chini kabisa ambako alisema nako kuna uchafu.
[h=1]CCM usanii mtupu[/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 17 February 2010

jk1.jpg

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) ni "usanii mtupu." Kelele za kupambana na ufisadi zimeishia kwenye ndoa na watuhumiwa wakubwa.
"Wamefunika kombe mwanaharamu apite; badala ya kufunua kombe ili mwanahalali asimame," ameeleza mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho mjini hapa.
Kilichotarajiwa katika vikao vya chama hicho vilivyoanza Jumamosi iliyopita, ni watuhumiwa ama kuondolewa katika chama au kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Lakini kilichofanyika ni kuweka kando tuhuma za aina zote za ufisadi zinazokabili baadhi ya viongozi ndani ya NEC na wote kuonekana kama kwamba hakukuwepo tuhuma wala msutano.
Hali hii ya "muwafaka" na watuhumiwa wa ufisadi ilianza kuonekana Alhamisi iliyopita pale Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilipojinyenyekeza kwa serikali.
Kamati, kana kwamba kulikuwa na shinikizo, ilikubali karibu majibu yote ya serikali juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya bunge kuhusu mkataba kati ya serikali na kampuni feki ya Richmond.
Ni kashfa ya Richmond iliyomng'oa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili wa wizara ya nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.
Mwingine ambaye amekuwa akihusishwa na kashfa ya Richmond na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutumia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ni Rostam Aziz, mbunge wa Igunga.
Rostam amekuwa akitajwa mara kadhaa kuwa mmiliki wa Kagoda ambayo ilichota zaidi ya Sh. 40 bilioni; kughushi nyaraka na kumhusisha rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa ndiye aliyeruhusu ukwapuaji kufanyika.
"Sasa huwezi kuamini kuwa kulikuwa na mvutano kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wabunge waliokuwa wamejipambanua kama makamanda dhidi ya ufisadi. Ghafla wote wakawa kama wamepigwa pasi," ameeleza mjumbe huyo wa NEC.
Habari za ndani ya vikao zimeeleza kuwa aliyepigilia msumari wa mwisho kwenye uhasama uliokuwa umejengeka ni mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Imeelezwa kuwa Rais Kikwete, baada ya baadhi ya wajumbe kuonyesha kung'aka, wakitaka watuhumiwa wafukuzwe kwenye chama, alilalia upande wa Kamati ya Mwinyi na kusema ilihitaji muda zaidi kumalizia kazi yake.
CCM iliunda Septemba mwaka jana kamati ya viongozi watatu kuchunguza kiini cha mvutano ndani ya bunge na kati ya bunge na serikali, na ndani ya baraza la wawakilishi. Mwenyekiti wake alikuwa Ali Hassan Mwinyi.
Ilikuwa baada ya taarifa ya Kamati kujadiliwa ndani ya Kamati Kuu na baadaye kuwekwa wazi ndani ya NEC, baadhi ya wajumbe walipendekeza watuhumiwa wa ufisadi wafukuzwe kwenye chama.
Watuhumiwa hao ni pamoja na aliyekuwa waziri wa miundombinu, Andrew Chenge anayehusishwa na mlungula kwenye ununuzi wa rada na ambaye alikuwa na zaidi ya Sh. 1 bilioni katika akaunti ya benki nchini Uingereza.
Aidha, kuna taarifa kwamba mbunge wa Ukonga, Makongoro Mahanga alisimama kikaoni na kutaka NEC imsafishe Lowassa kwa madai kuwa "alituhumiwa bila kusikilizwa."
Makongoro alinukuliwa akisema kitendo kilichompata Lowassa kinafanana na kile kilichowahi kumkuta rais mstaafu Mwinyi ambaye alijiuzulu kwa makosa ya wengine.
Hata hivyo, hoja ya Makongoro ilijibiwa papo hapo na Mwinyi mwenyewe aliyenukuliwa akisema, "…lakini mimi sikusafishwa," kauli ambayo ilisababisha baadhi ya wajumbe waangue kicheko na kuzima kabisa mpango wa Lowassa na wapambe wake kutaka asafishwe.
Taarifa zinasema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Bernard Membe na John Chiligati walikuwa miongoni mwa wajumbe wa NEC waliotaka Chenge achukuliwe hatua kwa kilichoitwa "kuaibisha chama chao" kwa kuhusishwa na kashfa ya rada.
NEC iliambiwa na Kamati ya Mwinyi kuwa ilikuwa haijakamilisha kazi yake na hivyo ilihitaji muda zaidi. Taarifa za baadaye juzi zilisema iliongezewa miezi miwili.
Mjumbe wa NEC ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia MwanaHALISI kuwa alikuwa na maoni tofauti kuhusu kamati hiyo kuongezewa muda.
kwa maoni yake, alisema, kamati ya Mwinyi haina kazi nyingine ya kufanya isipokuwa "hiyo ni njia ya kupoteza muda tu" ili kuonekana kamati inashughulikia mapatano ya makundi.
"Ukiangalia kwa makini utaona kuwa hakuna muda zaidi wa kujadili masuala haya. Kuanzia Aprili chama kitakuwa katika pilikapilika za uchaguzi. Hapa ndipo kinafunga mjadala wa ufisadi. Tutakutana majimboni," ameeleza.
Wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema "muwafaka" na watuhumiwa wa ufisadi umeonyesha sura halisi ya CCM na mwelekeo wake katika siku za usoni.
"Kwa hatua hii, watuhumiwa wamepata mahali pa kupumulia. Watapata nguvu zaidi na kujiimarisha. Hapa ndipo watawashughulikia wale wanaowachukulia kuwa ni maadui zao," wameeleza.
Kumekuwa na madai kuwa Spika wa Bunge Samwel Sitta amekuwa akitumia "kivuli cha kupambana na ufisadi" ili kumuangamiza Lowassa kisiasa.
Pamoja na spika, walikuwa Dk. Harisson Mwakyembe, Anne Kilango Malecela, Fred Mpendazoe, William Shelukindo, Lucas Selelii, Christopher Sendeka, James Lembeli, Aloyce Kimaro, Injinia Stella Manyanya ambao sasa wamenywea.
Habari zisizorasmi zinasema wabunge hao wanaweza kuwa wameamua kuachana na malumbano ya wazi ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Katika hatua nyingine, NEC imekubali maridhiano kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad lakini kwa masharti magumu yanayoweza kuleta sura mpya ya maridhiano hayo.
"NEC imekubali maridhinao hayo lakini wamesema maazimio ya Butiama ndiyo yazingatiwe na utekelezaji wake utakuwa ni kura za wananchi wa Zanzibar. Kazi ya kutafuta maoni kwa mujibu wa kikao ni baada ya uchaguzi mkuu," kilieleza chanzo chetu.
"Baada ya uchaguzi serikali itaundwa. Kazi ya kwanza ya serikali hiyo itakuwa ni kuendesha kura ya maoni ya wananchi juu ya serikali hiyo ya kitaifa, baada ya hapo ndio mabadiliko yatafanywa kwenye serikali," ameeleza.

CCM usanii mtupu | Gazeti la MwanaHalisi
 
Nakubaliana na wewe juu ya Mwanri kuwa waziri mkuu. Lakini si inabidi awe waziri kamili kwanza au? Kwani Waziri Mkuu anatokana na wabunge wa majimbo lakini pia ni lazima awe na uzoefu, at least in practice katika siasa za Tanzania, atokane miongoni mwa wajumbe wa baraza la mawaziri; manaibu mawaziri sio wajumbe wa baraza la mawaziri. Nje ya Nyerere pengine na kawawa, hakuna waziri mkuu mwingine aliyetokana na ubunge peke yake au ubunge na unaibu waziri.
Otherwise miongoni mwa waziri waliopo sasa, magufuli angefaa sana katika hiyo nafasi lakini wakubwa hawampendi huyu mtu for some reasons. Sitta nae angeimudu nafasi hiyo vizuri. Wengine waliobakia kwa kweli sioni kama wataleta jipya. Hata kwenye nafasi zao za uwaziri, wengi wanapwaya kama ulivyosema. Sijui kwanini JK katika miaka yake saba ya Urais amekuwa na tabia ya kuteua watu wa ajabu kabisa katika nafasi za uwaziri na kuacha wabunge wengi tu wenye uwezo mzuri wa kumudu nafasi hizo. Rais ana uwezo wa kuteua watu kumi kuwa wabunge, na maana ya sheria hiyo ni kumpa rais nafasi ya kuteua watu anaodhania wanaweza kuwa mawaziri wazuri wa kumsaidia lakini kwa bahati mbaya hawakupata nafasi ya kuwa wabunge. Kuna watu wengi wenye experience huko private sector, na pia makatibu wakuu ambao angeweza kabisa kuwaondoa huko na kuwapa uwaziri, ambao wangefanya kazi nzuri sana.

Tatizo letu si watu, ni utamaduni na mfumo mzima.

Hata umuweke malaika gani kwenye mfumo na utamaduni mbovu hufanyi kitu.

Tuliona Mizengo Pinda akishangiliwa sana alivyotajwa kuwa PM baada ya Lowassa, kiko wapi sasa?

Kikwete alivyopata urais watu walifurahi sana, wakasema alibaniwa na Mkapa, wengine wakamuita "nabii", kiko wapi sasa?

Kwa kutumia hizi siasa za personalities za "fulani atafaa sana" wakati hatuna utamaduni wa kuangalia policies na meritorious ascendacy tutabadilisha wachezaji kumbe tatizo ni mfumo wa mchezo tunaocheza.

Bila kubadilisha mfumo na utamaduni wa siasa za kufuatilia mambo deeply na kujikita katika policies kuliko personalities, tutapiga mark time kwa miaka 50 mingine.
 
Back
Top Bottom