NEC ya dharura Dodoma kishindo gani?

NEC ya dharura Dodoma kishindo gani?

Muhi2 ya vigogo (Appolo) hawajagoma so hiyo ya walalahoi haiwahusu!!
 
Bila kumpa Agrey mwanri uwaziri mkuu basi iyo post ifutwe,ila we pasco unafanya utetezi kwa jk,hakuna jipya.KWA TAARIFA YENU ULIMBOKA AMEWAMALIZA NA MGAYA NAYE YU NJIANI.arusha tunaandaa mgomo wa daladala kushinikiza uchaguzi kata ya daraja mbili

Kidogo Agrey anafaha faha kwa sasa kwa kuwa anonyesha kuwa ni kiongozi mwenye kudare na pia mara zote nimeona uwa anakubali kosa au kukili kosa na uomba msaada kuunga nguvu kutibu tatizo.Uwa nachukia sana viongozi walio wengi ndani ya ccm na serikali kutokukubali makosa na kuafikiana na waele wote wanaotafautiana nao mitizamao.Ina niuma sana sana kuona wanakuwa allogant kwa kila jambo muhimu kwa Taifa.Yani kwa ujumla ni ile tabia ya umuch knowa wa viongozi wetu,as if kama ni gari basi wao ndio watu pekee wanaojua kuliendesha na kulitengeneza pekee na wengine wote ni vilaza na hawana chochote cha kujadili kuhusu gari ilo.
Kwa kiwango fulani kama yatatokea mabadiliko basi waziri mkuu kuwa huyo jamaa nami nakubaliana nawe,ila aongeze kasi ya ufuatiliaji baada ya maamuzi yake,manake swala la kuamua juu ya utatuzi ni swala moja na kufuatilia kuwa tatizo limetibika ni jambo jingine.

Japo watu watajiuliza magaufuli ni vipi,ukweli kasi ya magufuli na JK na waziri wake mkuu zimepishana sana,kwani magufuli anaonekana kuwa na kasi zaidi ya JK na waziri wake mkuu hivyo kutofautina sana nao kwa kasi na hasa waizri wake mkuu anaeonekana ni mtu wa kusubilia kauri za wakuu wake.Hivyo nafilkilia ingekuwa vyema magufuli akapigwa chini ili kumuandaa kwa safari ya kagame wetu ajae kuipaisha Tanzania.Tumeshajua uwezo wa utendaji lilobaki ni kumuandaa kisaikolijia na kisiasa kwa kuwa yeye ni msomi wa masomo ya sayansi [Science] yani yuko katika hard system thinking na style ya uendeshaji wa Taifa hili unaegemea zaidi kwenye soft system thinking.Ni vyema wakamuweka pembeni ili kuandaliwa kuwa hata Rais au waziri mkuu pindi tutakapokuwa na kagame wetu hapa bongo.
 
dawa piga chini baba tunu weka magofuli au mwanri hapo! Acha na hao mashemeji zake mama riz wanakukosta rais watu!
 
Mh Rais kama umefuatilia sakata la mgomo wa madaktari utakubaliana nami kuwa viongozi wa wizara ya afya ndio wametufikisha hapa tulipo kwa kufanya maamuzi mabovu ya visasi na hasira dhidi madaktari wa intern. Sasa Mh jk ulikua huna mda wa kupoteza zaidi ya kuwafukuza kwa haraka waziri, naibu wake na katibu wa afya na kuwaomba msamaha madaktari. Sasa haka kamchezo ka kuwalinda watu wachache wateule kwako unauona moto wake unavyoliunguza taifa? Hivyo bomu lako ulilotega mwenyewe linakulipukia, sasa ni wakati wa kuwafukuza wateule wako waliotuletea janga hili na baadae ukae na madaktari na kuwaomba msamaha kwa waliyotendewa. JK funguka! Kabla nchi haijawaka moto.
 
Boniface Meena, Dar
Midraj Ibrahim, Dodoma
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), inatarajiwa kukutana kwa dharura mjini Dodoma Februari 12 mwaka huu.Kikao hicho cha Nec kinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa ndani ya chama hicho tawala umekuwa ukivuma vibaya, kufuatia wabunge wake kuingia katika vita ya chini chini na Serikali yao inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa zilizopaatikana jana kutoka ndani ya CCM, zilisema tayari wajumbe wa Nec wamekwishafahamishwa kuwapo kwa kikao hicho cha dharura.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, pamoja na mambo mengine, kikao hicho cha Nec kitajadili masuala ya mchakato wa Katiba ya chama hicho.

Taarifa hizo zilifafanua zaidi kwamba, wajumbe watajadili jinsi ya kuwapata wajumbe wa Nec upande wa Zanzibar, baada ya katiba ya chama hicho kufanyiwa marekebisho kuhusu taratibu za kuwapata wajumbe hao.

Kauli Nape

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alithibitisha kuwapo kwa kikao hicho cha Nec na vingine vya chama hicho tawala lakini, akisema si vya dharura.

Nape alisema leo kutakuwa na kikao cha Sekretarieti ya chama hicho itakayokutana mjini Dodoma.
Kamati ya Maadili

Alitoa ratiba ya vikao hivyo akisema, Februari ya 11 mwaka huu kutakuwa na kikao cha Kamati ya Maadili asubuhi na kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) baadaye mchana.

Katibu huyo aliongeza kwamba, Febrauri 12 kutakuwa na kikao cha Nec huku ajenda kuu ikiwa ni kupitia mabadiliko ya katiba ya chama ili kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi.

"Tunafanya hivyo kwakuwa kuna watu walikuwa wanahoji uchaguzi
utafanyikaje wakati Nec haijakaa, kwa hiyo hiki ni kikao maalumu cha mabadiliko ya katiba ili uchaguzi ufanyike, " alisema Nape.

CCM imeanza mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama hicho ambao uchukuaji wake wa fomu ulianza Februari 4 mwaka huu huku uchaguzi ukitarajiwa kuendelea awamu kwa awamu, kuanzia jumuiya na chama hadi Juni.

Vikao hivyo vya juu vya chama vinafanyika wakati pia chama hicho kikiwa bado hakijatekeleza mpango wa kujivua gamba ambao kwa sasa ulirudishwa CC kwa ajili ya maamuzi ya mwisho.


JK alivyowalainisha

Hata hivyo, juzi Rais Kikwete alifanikiwa kuwalainisha wabunge hao wa CCM, ambao walikuwa wameweka msimamo wa kukataa Muswada wa Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wabunge wachache, walikubali kupitisha muswada huo ambao unatarajiwa kuwasilishwa bungeni leo.

Baadhi ya wabunge waliohudhuria kikao hicho ni Jenister Mhagama (Peramiho), Peter Selukamba (Kigoma Mjini), Angela Kairuki (Viti Maalumu), Anna Kiliango (Same Mashariki), Saidi Nkumba (Sikonge), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro) na Muhammad Amour Chomboh (Magomeni).

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, wabunge hao walifikia uamuzi huo baada ya Rais Kikwete kuwaeleza kwamba bado wanayo nafasi ya kufanya marekebisho wanayoona yanafaa, kwa sababu yaliyopelekwa na Serikali ni mapendekezo.

“Kwa kweli tumemwelewa Rais, mwanzo kuna vitu ambavyo vilikuwa hatujaelezwa vizuri. Rais alichotwambia ni kwamba sisi ndiyo waamuzi wa mwisho, Serikali imeleta mapendekezo tuna haki ya kufanya marekebisho kwa sababu hiyo ndiyo kazi yetu,” alisema mmoja wa wabunge hao na kuongeza:

“Rais ametwambia hakuwa na makosa kukutana na Chadema, amekutana nao kama alivyofanya kwa makundi mengine, na mapendekezo yao amatuletea sisi ndiyo waamuzi tupime wenyewe.”:A S 465:
 
Sijui kwa nini Jakaya yupo kimya kiasi hiki, sasa anamwongoza nani? Inauma sana Jakaya watu wanakufa kisa mgomo na wewe umeshidwa kuutatua kisa siasa. Ok naona kama kwako hii inakupa usingizi. Tupo pamoja madakitari
 
Rais jk, ameitisha mkutano wa dharura wa nec mjini dodoma utakaofanyika tar 12 feb, naye nape amekiri uwepo wa mkutano huo na kusema lengo ni kujadili katiba mpya ya ccm.

Nnape anamaanisha Katiba mpya ya CCM au Katiba mpya ya Taifa?

Maana tunachokijua ni kwamba Wabunge wa CCM wamekataa kukutana na Rais wao Kiwete kwa madai kwamba amewasaliti kwa kukubaliana na maoni ya CHADEMA yaliyopelekea kurudishwa kwa mswada wa Katiba mpya kufanyiwa marekebisho.

Yawezekana kabisa hapa Nnape na M/kiti wake hawataki kusema ukweli kuhusiana na kikao hicho cha NEC.
 
mbona bado hawasemi ukweli nape na jk wake......kikao si cha kuhusu katiba ya ccm ni kuhusu hali halisi ilivyo huko ndani ya ccm hasa baadaya wabunge wake kumtunishia misuli
 
Mkuu, kuna thread nyingine ipo kama hii na wadau wameichangia!
 
Mh Rais kama umefuatilia sakata la mgomo wa madaktari utakubaliana nami kuwa viongozi wa wizara ya afya ndio wametufikisha hapa tulipo kwa kufanya maamuzi mabovu ya visasi na hasira dhidi madaktari wa intern. Sasa Mh jk ulikua huna mda wa kupoteza zaidi ya kuwafukuza kwa haraka waziri, naibu wake na katibu wa afya na kuwaomba msamaha madaktari. Sasa haka kamchezo ka kuwalinda watu wachache wateule kwako unauona moto wake unavyoliunguza taifa? Hivyo bomu lako ulilotega mwenyewe linakulipukia, sasa ni wakati wa kuwafukuza wateule wako waliotuletea janga hili na baadae ukae na madaktari na kuwaomba msamaha kwa waliotendewa. JK funguka! Kabla nchi haijawaka moto.

Sio hao tu pia Waziri mkuu kwani ndo aliyefanya jazba kwa kutoa vitisho kwa watu waliokuwa na madai halali. Huyu ndiye aliyeharibu kila kitu kwa kuusikiliza uongo wa wizara ya afya bila kuuchuja.

Madaktari mkumbuke kuwa katika mgomo huu mnahitaji kuwa pamoja. Inabidi sasa kuongeza madai ya kuwa baada ya matakwa yenu yote kutimia, wote mnarudishwa kazini na hakuna hata mmoja atakayehamishwa toka kwenye kituo chake cha kazi bila ridhaa yake na pinda afute aombe radhi na akiri kuwa alidandia treni kwa mbele.
 
Sio hao tu pia Waziri mkuu kwani ndo aliyefanya jazba kwa kutoa vitisho kwa watu waliokuwa na madai halali. Huyu ndiye aliyeharibu kila kitu kwa kuusikiliza uongo wa wizara ya afya bila kuuchuja.

Madaktari mkumbuke kuwa katika mgomo huu mnahitaji kuwa pamoja. Inabidi sasa kuongeza madai ya kuwa baada ya matakwa yenu yote kutimia, wote mnarudishwa kazini na hakuna hata mmoja atakayehamishwa toka kwenye kituo chake cha kazi bila ridhaa yake na pinda afute aombe radhi na akiri kuwa alidandia treni kwa mbele.

Kweli ndugu kama unavyo sema Pinda naye anahusika moja kwa moja.Asante kwa kunikumbusha hilo
 
Rais jk, ameitisha mkutano wa dharura wa nec mjini dodoma utakaofanyika tar 12 feb, naye nape amekiri uwepo wa mkutano huo na kusema lengo ni kujadili katiba mpya ya ccm.


Toka lini suala la katiba likawa ni suala la dharura? Kwa sasa dharura ni Afya ya watanzania, ombwe la uongozi na mfumuko wa bei! Achana na mambo ya katiba.
 
Ndugu wana JF,
Habari nilizozinasa hivi punde ni kwamba, mheshimiwa Rais Kikwete ameahirisha ghafla ziara yake ya kikazi katika nchi za Nordic (Denmark, Norway, Sweden, Finland) na Uholanzi, ambayo ilitakiwa aianze wiki ijayo. Sababu zilizotolewa na serikali ni kwamba JK ameahirisha ziara hiyo ili kutatua mzozo wa ndani ya chama chake ambao unafukuta sasa, ukizingatia kwamba mwaka huu chama chake kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu. Hizi ni habari za ndani kabisa toka kwa waandaaji wa ziara hiyo.:A S 465:
Nawasilisha
 
tetesi zimezidi hapa JF mods peleka thread hii hoja mchanganyiko hapa inatuchanganya tu.
 
Kwani maamuzi magumu yanaanzia kwenye chama!
Hiyo katiba... Hiyo katiba.... Hiyo katibaaaa......
 
Mara kadhaa Jk anatumia fursa ya viongozi wengi wa CCM kuwa Dodoma kufanya vikao vya chama. Sidhani kama ni mkutano wa dharura.
 
Back
Top Bottom