Ndugu zangu watanzania,
Nadhani imefikia wakati tuukubali ukweli na kuuishi. Tunavyomuita Rais wetu majina ya ajabu ajabu na kumpa majina yashushayo, ndivyo hivyo atakavyokuwa.
As long As hatuwezi kumuondoa hapo alipokuwa kwa mujibu wa katiba, basi inatupasa Kutii Mamlaka iliyopo (kama maandiko yanavyotuambia).
Hebu tuache kumshusha na kumsemea mabaya siku zote, Hebu tuanze Kumuinua, Na kumpa Baraka ili abarikiwe na kuliongoza taifa letu.
Hivi unajua kama maneno yanaumba?
Hebu angalia mzazi ambaye anamuita ajina mabaya mtoto wake na kumuwazia mabaya, e.g hili toto jinga sana, wewe mbwa, litazame kwanza sura kama ng'ombe, we mtoto ndio maana hauna akili, Asilimia 95 ya watoto hao wanaishia kuwa na tabia za mbwa, majinga na yote ambayo watoto wao wamewawazia na kuwanenea.
Hebu tuache kumsema vibaya raisi wetu na kutoa mawazo ya kuendeleza nchi kuliko kulaumu, Mungu atasikia huko aliko na kutusaidia, kulaumu hakutosaidia chochote zaidi ya kuwa na hasira vichwani mwetu zinazopunguza siku za kuishi.
Ee Mungu, Tunaomba mkono wako wenye nguvu umguse Rais wetu na kuweza kuliongoza taifa letu katika nchi ya asali na maziwa.