Ndugu zangu walinidanganya nikasoma kozi isiyo na soko

Nashindwa kung'amua kwakweli.. Waliotuletea haya mambo wametupata sana..

Me nadhani tatizo lilianza hapo ulipojiaminisha kwamba kuna watu wana wajibu wa kukufanyisha kazi baadae wakulipe ujira (fedha) sasa umekuta sivyo ndio unaanza kuchanganyikiwa..


Anyway mkuu umesomea mambo ya biashara, hope umeiva kwenye maeneo hayo..

Ninachokushauri, tumia hiyo elimu ulionayo uweze kujikwamua kiuchumi..

"YOU ARE RESPONSIBLE OF YOUR LIFE"

Kumbuka hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kozi ambayo haina soko ni mtazamo wako tu na vile unavyoichukulia.
Watu kibao wako maofisini wanafanya kazi ambazo hawakuzisomea...Ninachoamini mimi kuna kazi nyingi ambazo unaweza fanya huku knowledge ya biashara ukaitumia kidogo sana.
Yawezekana pia CV yako umeitengeneza ki biashara so kwingine hau fit. Jaribu kutengeneza CV yako kwa namna ambayo unaweza ku accomodate kazi tofauti tofauti. Ukishapata kazi ndo unaweza kuamua career path ya kufuata.
Usiwalaumu nadhani walikushauri kwa mtazamo wao.
Best of Luck!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 4 siyo mingi kabsa rudi kasome degree uliyopenda wew mbona inawezekana tu mkuu!

By the way hakuna course isiyo na masirahi hizi ni perception zako tu. Vuta subra na jitofautishe na wenzako katika huo uhasibu wako. Kuna siku haya maneno yako yatakuja kukusuta sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom