Mume wangu hapendi ndugu zangu

HakiKwanza_2015

JF-Expert Member
Nov 16, 2022
345
505
Habari wakuu, nahitaji ushauri,

Mimi ni binti nimeolewa naishi na familia, mume wangu pamoja na mdogo wangu wa kike. Tatizo ni kwamba mume wangu amekuwa na kisirani sana juu ya huyu mdogo wangu wa kike. Kila anachofanya lazima mwanaume alalamike.

Na wala sijawahi kuwa na mawazo labda anamtaka, ndiyo maana anafanya hivi visirani vyote. Mazingira niliyomlea mdogo wangu namjua na ana tabia njema sana.

Mume wangu pia siwezi kumuhukumu kwa uhuni, hajanipa sababu ya kufanya hivyo. Kwahiyo kinachonichanganya ni kwanini ananipa wakati mgumu wa kumfanya mdogo wangu aishi kama yuko kwa mtu baki wakati mimi ni dada yake wa kuzaliwa naye kabisa?

Kila kitu ni lazima aseme kana kwamba huyu mtoto anamkwaza. Kinachoniuma mimi ni kwamba kila siku namuuliza hivi kama angekuwa anaishi hapa ndugu yako halafu mimi namfanyia hivi
Ungejiskiaje? Si ningeonekana mimi ndiyo mbaya sipendi ndugu wa mume?

Na kinachonishangaza, kuna kijana tunaishi naye hapa siyo ndugu wa damu wa mume wangu lakini anatusaidia kazi za hapa nyumbani, ametokea kijijini kwao. Sasa huyu hata akosee vipi mume wangu ukimwambia huyu kakosea hiki na hiki wala hutomuona akijigusa kwenda kumfokea wala kumsema.

Sana sana atajibaraguza tu ili uone ame 'react' na hii siyo mara ya kwanza. Chochote kinachomuhusu mtu wa kwao hutomuona mume wangu amekasirika, lakini ikiwa ni swala la kuhusu ndugu yangu atafoka haswa.

Inafika hatua anamnyima hadi vitu vya kutumia ndani ambavyo hata yeye anavitumia. Hiyo siyo shida, naumia kwasababu mimi huyu mtoto namchukulia kama mwanangu wa kumzaa, nimelichukua hilo jukumu kwa mama yangu tangu mdogo na kwa sasa mama haishi Dar na hatujawa na mahusiano mazuri sana na baba yetu kwa sababu ya mambo ambayo amekuwa akifanya kwetu sisi kama familia.

Kwahiyo najitahidi sana mdogo wangu asijihisi mpweke wala asione kuna pengo la kuumizwa kimalezi na baba yetu.

Na kuna siku ilikuwa sikukuu, nilimwambia mume ndugu zangu wanakuja kwasababu wazazi wetu hawaishi hapa Dar naomba sisi hapa tuwafanyie kitu kama kuwaalika wale hata chakula cha kawaida tu, akasema yeye hana hela.

Wala sikukasirika, nikajikokota nikanunua vyakula nikapika nioneshe kama mume wangu ndiyo amewaalika na wao waone wana kaka hapa mjini. Mume wangu wala hakuonesha ule ushirikiano ambao mimi huwa nautoa wakija ndugu zake, maana huwa napika haswa hadi kwenye kuni.

Nahangaika, napanga, naandaa, nikijua ndugu wa mume wangu wanakuja ila siku wamekuja wadogo zangu sikupata ushirikiano huo. Nilisema acha tu nivumilie kwasababu namheshimisha mume wangu mwenyewe.

Mara nyingine aliniliza na nikamwambia mimi huwa silii lakini unanitenda kama vile sisi kwetu ni masikini, yaani wadogo zangu walipita kutusalimia wakawa sebuleni akaniita chumbani akaniambia nataka kuja kukaa sebleni, naomba nikute siti ya kukaa. Kanakwamba wadogo zangu wamejaa pale maana walikuja kusalimia.

Kinachoniuma ni kwamba, sisi katika kukua kwetu hatujawahi kulelewa na ndugu, kama wadogo zangu wanakaa nje ya kwa baba na mama basi kwangu ndiyo pa kwanza, kwahiyo nikiona wanatendewa hivi naona kama ni mimi ndiyo napitia, sitamani wajione watu baki.

Na kuna muda huwa nawaza, ningekuwa na uwezo ningejenga nyumba yangu niwaweke wadogo zangu hadi watakapokuja kuolewa. Atakae tawanyika sawa, ila kwakuwa mzazi wetu ana uwezo ataona nampokonya wanae. Ila natamani sana wadogo zangu waishi maisha niliyotamani kuishi.


Ushauri unaohitajika;

1. Ni kosa mimi kumtetea mdogo wangu? Kwasababu ninapo jaribu kuuliza kwani tatizo lipo wapi hadi ufoke juu ya jambo dogo hivi, naonekana mkorofi au nataka kumpanda mume kichwani?!

2. Kiubinadamu, huyu mdogo wangu amekosea kuja kuishi kwangu? Nimemlea na hana tabia mbovu kwahiyo namjua, na kila siku namwambia mdogo wangu ikitokea leo dada yako nimedondoka, watoto wangu hutowaacha naamini.

Nampenda sana huyu mtoto, Mungu pekee ndiyo anajua. Kuna muda namwambia mume wangu basi nisamehe mimi naomba vumilia kidogo huyu mtoto akipata kazi ataondoka.

Kwasababu siyo kwamba kwetu tuna shida ya kifedha na wala mume wangu hamgharamii chochote zaidi ya chakula ninachokula mimi ndiyo anachokula huyu mtoto. Ni anakaa kwangu kwasababu ni karibu na chuoni anaposoma yeye.

Kwa upande wa nauli na gharama za kujikimu anatoa mzazi na mimi nikipata huwa nampa kidogo, nashindwa hata kusema namuhudumia maana biashara niliyokuwanayo ilishavurugika baada ya kumuomba mume tusimamie wote ili asiwe na wivu na wateja (stori ndefu haihusiki na mada).

Kwahiyo sina uwezo wa kumgharamia mdogo wangu kwa asilimia mia ila nikipataga 20, 30 nampa ajisogeze. Na mdogo wangu najua ananijali sana, kuna vitu ananifanyiaga huwa nahisi kama nina binti wa kike kabisa.

Yaani kiufupi sipo tayari ndoa yangu iingie doa kwasababu ya mimi kumtetea mdogo wangu na sipo tayari kugombana na mdogo wangu kwasababu yoyote, sijui kama nimeeleweka hapa?

3. Nifanyeje ili mume wangu awe na amani, mdogo wangu pia awe na amani na asijue kwamba shemeji yake huwa analalamika? Kwasababu kila ambacho mume huwa analalama mimi huwa natafuta namna ya kumuelekeza mdogo wangu kama vile mimi ndiyo nataka iwe hivyo, namwelekeza ili asije akafanya tena mume asione tunamdharau.

Na kibaya ni kwamba kuna siku mdogo wangu alisikia nikilalamika sana kwamba hii hali ya yeye mume wangu kukosa amani inaninyima raha, nataka anisaidie mawazo nifanyeje ili awe na furaha na nimuelewe ili niwe namrekebisha mdogo wangu na mimi niwe na amani, hakunijibu! Kesho yake mdogo wangu alikosa raha na sikutaka tena kuibua hiyo mada.

Kiukweli ndoa yetu haina miaka mingi lakini naumia, nilitamani sana mume wangu amlee mdogo wangu kama ambavyo mimi ningelea wa kwake. Lakini inanipa wakati mgumu sana kwamba isije ukatokea mtafaruku kati yao. Nitakae kuwa kwenye wakati mgumu ni mimi.

Uadui huwa hauishi ikiwa mmoja akijua mwengine anamchukia. Na kuna muda huwa namwambia mume, natamani hata na wewe aje ndugu yako hapa akae nikuoneshe jinsi inavyokua kuishi na familia, kuna vitu unavichukulia kama ni mwanao kafanya. Na mume kwangu ana upendo, anajitahidi sana kwakweli, kama kuna makosa ni madogo ya kiubinadamu, ndiyo maana nafukia mengine yoote.

Ninachotamani ni ushauri tu wa kumfanya mume wangu amuone mdogo wangu kama mdogo wake. Niwe na amani pia.

Naombeni ushauri.
 
Pole sn mkuu ,,Hilo ni tatizo tena ni kubwa sn.

Nakushauri mtoe mdogo wake mrudishe nyumbani.

Pengine mumeo anaomba kugegeda mdogo wako.

Lakini ni ngumu kukueleza sababu ya kuvunja ndoa yako.
Hapo Kuna jambo,,

Chukuwa hatua.
Asante kwa ushauri,

naweza kuwapa benefit of doubt katika kugegedana, mdogo wangu amefata nyayo zangu na ananijua vizuri tu na kiukweli uhuni hana.

Mume wangu kusema anatembea nae naweza kumtetea kwa sasa, mimi ni mtu mfatiliaji sana wa hisia so kama kuna mahusiano kati yao ntakuwa wa kwanza kujua ila kwasasa ntakua natenda dhambi kumuhukumu mume wangu siku akinipa
Hiyo sababu ntajua tu.

Sababu ambayo nahisi ni kwamba mume wangu hajawahi kuishi na familia kubwa yenye ndugu mchanganyiko kama mimi nilivyokua wazazi wetu maisha yao yoye wamekua wakiishi na ndugu zao so nilijifunza huko kuwa kila mtu ni mwanadamu mwenye uwezo wa kukosea.

Kilichonileta natamani mume wangu awe na amani na mdogo wangu naumia kuwa katika position ya kumfukuza mdogo wangu wakati mimi ndo nilishadadia aje hapa ili awe karibu na chuo. Leo namwambiaje nenda nyumbani? Ni mbali sana kutokea nyumbani kwenda chuoni kwao. So kwa hapa kwangu anarahisisha.
 
Huyo ni mbinafsi aliyepitiliza,
Ukishamjua mtu hakusumbui Tena,
Anza kutomchukulia serious kweye hayo mambo yake ya uselfish, mpuuze na usiruhusu moyo wako uumie simply umeshamjua, act matured and normal anapokupa changamoto kama hii.

Akiona haujali atabadilika mwenyewe na kuacha ubinafsi japo itachukua muda ila matunda utayaona.
 
Huwezi kumbadilisha huyo mwamba, tabia zake ni ngumu mno, hata wewe itafikia mda atakuwa na visirani na wewe.

Maisha yetu haya ya kitanzania huwezi kukwepa kuishi na ndugu, awe wa upande wako au wa mke/mume kwa sababu tunategemeana.

Ongea na wazazi wenu, muone jinsi gani huyo binti ataishi nje ya hapo, wanaume wenye guru pia wapo.
 
Asante kwa ushauri,

naweza kuwapa benefit of doubt katika kugegedana, mdogo wangu amefata nyayo zangu na ananijua vizuri tu na kiukweli uhuni hana.

Mume wangu kusema anatembea nae naweza kumtetea kwa sasa, mimi ni mtu mfatiliaji sana wa hisia so kama kuna mahusiano kati yao ntakuwa wa kwanza kujua ila kwasasa ntakua natenda dhambi kumuhukumu mume wangu siku akinipa
Hiyo sababu ntajua tu.

Sababu ambayo nahisi ni kwamba mume wangu hajawahi kuishi na familia kubwa yenye ndugu mchanganyiko kama mimi nilivyokua wazazi wetu maisha yao yoye wamekua wakiishi na ndugu zao so nilijifunza huko kuwa kila mtu ni mwanadamu mwenye uwezo wa kukosea.

Kilichonileta natamani mume wangu awe na amani na mdogo wangu naumia kuwa katika position ya kumfukuza mdogo wangu wakati mimi ndo nilishadadia aje hapa ili awe karibu na chuo. Leo namwambiaje nenda nyumbani? Ni mbali sana kutokea nyumbani kwenda chuoni kwao. So kwa hapa kwangu anarahisisha.

Mkuu, amini maneno yangu. Ikitokea siku mumeo na mdogo wako wakaja kupatana na kucheka pamoja.

Elewa umeshachelewa. Ameshapigwa mtu tako 3000.

Mimi ni mwanaume na nimeshapitia yote hayo. Kuanzia kutongoza mashemeji na hata marafiki wa mke.
Hapo mumeo katoswa na mdogo wako hilo ndy tatizo. Hamisha mdogo wako, au kubali kushare mapenzi.

Ukweli mchungu.
 
Habari wakuu. Nahitaji ushauri,

Mimi ni binti nimeolewa naishi na familia, mume wangu pamoja na mdogo wangu wa kike. Tatizo ni kwamba mume wangu amekua na kisirani sana juu ya huyu mdogo wangu wa kike. Kila anachofanya lazima mwanaume alalamike. Na wala
au unambania haki yake ya ndoa? maana wanaume hasa wasio wagomvi na malaya, wife akikubania huwa tuna visirani sana. Kama unambania acha, jiachie ale ashibe utanifuata inbox kunishukuru.
 
Hapo umeongelea sana madhaifu ya upande mmoja, kwa upande wako hatujui japo utasema unawapenda ndugu wa mume ..........
Kweli kila binadamu ana mapungufu hata yeye mume wangu ukimuuliza atasema mke wangu ana moja mbili tatu. Lakini kilichonileta hapa sio mapungufu ya mume wangu nnachotamani ni kujua au kuelewa nifanyeje ili amuone mdogo wangu kama mwanae.

Haitokua sawa kama akimfanyia mdogo wangu ubaya kwa kuwa mimi ni mbaya japo huwa napenda sana kumuuliza mume wangu kama kuna lolote nimemkosea nirekebishe. So asiposema naona naenda sawa tu
 
Ukisema hanipendi nanyong’onyea maana ananijali yani kuna vitu ananifanyia naridhika so nikimuhukumu kwa hili ntakua nakosea. Roho ya kimaskini siwezi Kupinga ila naikemea tu kwa jina la Muumba. Na ntafanyeje sasa ndo mume wangu wa ndoa

Mrs Fulani...
Tofautisha kati ya upendo na kujali, unaweza kumjali mtu na haumpendi ndio maana huko njiani tunawajali wasiojiweza lakini haina maana kwamba tunawapenda.

Waswahili waliposema ukipenda boga na penda na ua lake walikuwa na maana pana na ndio hii ninayoimaanisha hapa.

Mtu mwenye roho ya kimasikini huwa ana vitabia lukuki kama uchoyo, ubinafsi, kisirani n.k, uusikute anamchukia mdogo wako sababu haoni pia mkiwasaidia nduguze.
 
Mkuu, amini maneno yangu. Ikitokea siku mumeo na mdogo wako wakaja kupatana na kucheka pamoja.

Elewa umeshachelewa. Ameshapigwa mtu tako 3000.

Mimi ni mwanaume na nimeshapitia yote hayo. Kuanzia kutongoza mashemeji na hata marafiki wa mke.
Hapo mumeo katoswa na mdogo wako hilo ndy tatizo. Hamisha mdogo wako, au kubali kushare mapenzi.

Ukweli mchungu.
Vipi kuhusu hao ndugu wengine wanaokuja hapo kusalimia na anawatosa? Mimi siamini kwamba binti kamkataa, hapo issue ni gubu la mwamba, hataki ndugu wa mke waishi hapo.
 
Umemtumia mdogo wako wa kike kama kinga ila kifupi mmerundikana mpo ndugu zaidi ya wawili... Waambie ndugu zako kuwa maisha ni magumu wabaki uko uko kijijini. Mfumo wa ujamaa umeshakufa sasa hivi tunaishi kibepari
Tupo ndugu zaidi ya wawili wapi sasa? Mimi na mdogo wangu mmoja anaeenda chuo anarudi jioni, ndo kurundikana? Soma vizuri maelezo. Mtoto ambae humlipii ada, humpi nauli, mara moja moja hata chakula ananunua yeye mdogo wangu akijibana chuo anatuletea vizawadi maskini.

Kwetu hatuna shida na nyumba dar ipo lakini nauli mtoto anaweza kutumia hata elfu 10 kutoka nyumbani kwenda chuo. So sio kwamba kwetu ni kijijini lakini nyumba ya hapa dar ilipo ni mbali na chuo. Nimeshaelezea sana.
 
Back
Top Bottom