Amemaliza chuo si miaka mingi sana, hajabahatika kuajiriwa bado.
Mungu alimuona na kumjaalia ajira ya muda mfupi ya sensa iliyofanyika hivi punde, si haba, kamilioni hivi alikashika na kwa hakika ilikuwa pesa nyingi sana kwake kwani alikuwa hajawahi kufanya dili lolote la kufikia kiwango hicho cha fedha.
Ebwana kumbe huyu mtu ni mfuasi mkubwa wa chama na kumbe alikuwa anafahamu vizuri ratiba za uchaguzi wa ndani wa chama.
Akahifadhi fedha zake vizuri tu hadi hapo juzi kati uchaguzi ulipofika na kujitosa mazima, wajumbe akawatafuta na, kama kawaida ya wajumbe, 'wakamhakikishia' kuwa ni mwenzao hivyo ka'm' kake kakaenda huko kwenye 'maji ya kunywa na nauli' za wajumbe, wote walimhakikishia ushindi wa 100% yaani wa kishindo. Kwa uhakikisho huo wa wajumbe, halikupenya masikioni mwake wazo todauti na hilo kutoka kwa yeyote.
Uchaguzi ulipofika hapa juzi, ndugu yangu ameshindwa, ameambulia vikura vichache mno ambavyo havifikii hata idadi idadi wajumbe waliotoka eneo lake.
Leo ni siku ya nne, ndugu yangu yupo ndani tu hatoki nje mpaka usiku na mimi, kwakuwa hakunishirikisha, nashindwa hata cha kufanya. Nimsaidie vipo huyu mtu wadau? Hawa vijana lini wataacha ukaidi?!!!!