Weka fungu fulani maalum la kusaidia watu kila mwezi, kwa mujibu wa uwezo wako.
Hili fungu kwangu mimi ni muhimu kuliko sadaka.
Halafu jipe sheria kwamba, mtu unayemuamini mwenye sababu nzuri atakayewahi kukuomba, umsaidie. Kwa kadiri ya uwezo wako na fungu hilo.
Ukilimaliza, akija mtu kukuomba, mwambie huna uwezo wa kumsaidia, fungu la kusaidia watu limekwisha.
Ukishindwa kufanya hivyo, lawama ni juu yako.
Kuombaomba ni jambo la aibu.
Tatizo tunaendekeza sana Ujamaa, tunasahau Kujitegemea.
Pia, tuna matatizo makubwa sana ya kimsingi ya kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa yaliyotufikisha hapa, hivyo sipendi sana kulaumu wanaoomba msaada.