Joanah
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 26,554
- 97,968
Jensen salamone,
Hiyo ndiyo faida ya kuomba ada kila mtu.
Unafikiri wakati wanakutumia hela shuleni wao hawakuwa na shida?
😂😂😂😂
Yuko kwenye payback period!!
Jensen salamone,
Hiyo ndiyo faida ya kuomba ada kila mtu.
Unafikiri wakati wanakutumia hela shuleni wao hawakuwa na shida?
Hii ya kubadili namba huwa i work mi nilibadili namba maza akawa anaendelea kuniuza tu kwa watu sijui anatamba huko kijijini kuwa mwanangu mtu fulani utasikia nimempa namba yako mtu fulani ni ndugu yako atakupigia akipiga huyo ndugu ndani ya siku mbili anaanza mizinga yani kero juu ya kero niliisha mwambia lakini ikipita muda anagawa tena namba yanguBadili no zako zote za sm then wazijue wazazi wako pekee baada ya hapo wakanye kuwa siku wakigawa no yako utabadili na wao pia hutawapa so hawatakupata
So utabaki kusaidia wazazi wako tu kwa siri
Tumia 3-5 yrs kujipanga
Ukishakuwa sawa unaweza acha wajue no yako
Ndg yangu ukijifanya yesu mtoa misaada utakufa maskini
Wakat mwimgine roho mbaya ni nzur hata Bible inasema usitoe zaid ya uwezo wako
Unadhan ukiwanyima ndo utakuwa na dhambi?
Sasa endelea kuwa maskini
Wazazi wako walikua wanaomba misada mbali mbali kwaniaba yako hivo ndotunavo ishi hapa Africa, mkipata msiba au majanga ya namna yoyote ndungu wanakuja kukufariji kwa nauli zao lini mnarudisha hizo fadhira acha kulalamikia ndg wengine tunawatafuta hatunaHawajawahi kuchangia chochote kwenye elimu yangu ni wazazi wangu pekee walihusika kwa 100% tangu nimeanza chekechea mpaka nimemaliza
Hilo ni janga la kitaifa na kwa kiasi kikubwa hatuendelei kwa sababu hiyo kwa kuwa tunashirikiana kugawana umaskini.Hii ndio shida ya kutoka familia duni. Badala ya wao kukuongoza kwenda kwenye mafanikio wanazidi kukudidimiza kwa kukuona mkombozi wa ukoo wakati bado haujaota mizizi.
Kusema ni tenge fungu la msaada ni ngumu mno kumbuka mshahara wenyewe ni kiduchu bado nahitajika kutenga kiasi fulani kwa mwezi kinisaidie kuanzisha kimradi hapo baadae so kwa hilo kwangu haliwezekaniki kwa sasa huo uwezo sinaWeka fungu fulani maalum la kusaidia watu kila mwezi, kwa mujibu wa uwezo wako.
Hili fungu kwangu mimi ni muhimu kuliko sadaka.
Halafu jipe sheria kwamba, mtu unayemuamini mwenye sababu nzuri atakayewahi kukuomba, umsaidie. Kwa kadiri ya uwezo wako na fungu hilo.
Ukilimaliza, akija mtu kukuomba, mwambie huna uwezo wa kumsaidia, fungu la kusaidia watu limekwisha.
Ukishindwa kufanya hivyo, lawama ni juu yako.
Kuombaomba ni jambo la aibu.
Tatizo tunaendekeza sana Ujamaa, tunasahau Kujitegemea.
Pia, tuna matatizo makubwa sana ya kimsingi ya kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa yaliyotufikisha hapa, hivyo sipendi sana kulaumu wanaoomba msaada.
Tatizo hao unaowapa wakiombwa na wao wanatoaBadilisha namba ya simu, halafu hiyo namba wape watu wachache sana mfano wazazi.
Hahah. Unezibuka.Mkuu wakipiga simu sema da sasa hivi wamechelewa umetoka kumtumia mtu pesa so umefulia akipiga mwingine jibu liwe hilo hilo watachoka wenyewe msaidie mtu aliyekupa hela kipindi unasoma tu wengine piga chini. Wakizidi sema umetoka kulipa kodi ya nyumba so uko vibaya au sema kuna mtu ulimkopa ndio umetoka kumlipa so huna hata mia
Basi waambie huna uwezo.Kusema ni tenge fungu la msaada ni ngumu mno kumbuka mshahara wenyewe ni kiduchu bado nahitajika kutenga kiasi fulani kwa mwezi kinisaidie kuanzisha kimradi hapo baadae so kwa hilo kwangu haliwezekaniki kwa sasa huo uwezo sina
Nimeipenda sana hii approach nitaanza kuitumiaMkuu wakipiga simu sema da sasa hivi wamechelewa umetoka kumtumia mtu pesa so umefulia akipiga mwingine jibu liwe hilo hilo watachoka wenyewe msaidie mtu aliyekupa hela kipindi unasoma tu wengine piga chini. Wakizidi sema umetoka kulipa kodi ya nyumba so uko vibaya au sema kuna mtu ulimkopa ndio umetoka kumlipa so huna hata mia
Naendelea kuchota maarifa kutoka kwenu. Asante sana mzeeMzee inaonekana umewaendekeza siku wa actie una kesi mahakamani ya uhujumu uchumi, dhamana ni mali isiyo hamishika ndugu ajitolee. utanipa mrejesho.
Ndio maana nikaamua kuleta hoja yangu hapa ili nipate madini kama haya hakika JF ni jumba la Great thinkers of all timesHuko kunaitwa kunasa kwenye tope na hakuna namna ya kuweza kujinasua kwa kuwa huo ndio utaratibu wa kiafrika tuliowekewa na waliotutangulia. Umeomba ushauriwe nini cha kufanya katika hilo, naamini utapata ushauri wa juu juu tu ambao hautakusaidia kupata ufumbuzi bila kujua mzizi wake. Kwa kuwa wewe hukushiriki kupanga safari yako ya kuja Duniani, huwezi kuwa na maamuzi yatakayokunufaisha wewe peke yako bila kuwahusisha waliokutangulia, waliochangia mafanikio yako na wanaokuzunguka bila kuwepo kwa mgogoro.
Kulipa fadhira kwetu sisi waafrika ni kitu kisichohitaji kujadiliwa na kama ukijifanya huelewi watakusema sana na mwishowe utatengwa na kutishiwa kupata laana ili hata kile ulichokipata usikifurahie. Kitu unachoweza kufanya kwa sasa ni kujitahidi SANA, ili usizae kwa lengo la mtoto wako kuja kukutunza wewe na ukoo wako, badala yake kama utaamua kuzaa basi uwe umejipanga vizuri kumhakikishia mwanao elimu ili akipata kazi aende akajitegemee bila kuwa na mzigo wa kukutunza wewe na washirika wako. Kukinga ni rahisi sana kuliko kutibu.
Kwa hali uliyonayo, unatakiwa uanze kuwaelimisha watu wako wa karibu kuhusu mzigo mzito wanaokutwisha wakati ndio kwanza unaanza maisha. Kufa na tai shingoni hakutakusaidia kwani huenda ukaanza mgogoro na mweza wako kuhusu kutoa huduma zaidi kwa watu wa pembeni zaidi ya familia yako ambayo ni mke na watoto wako basi.