SODIUM CYANIDE
JF-Expert Member
- Jun 5, 2013
- 691
- 1,166
Hii ndio shida ya kutoka familia duni. Badala ya wao kukuongoza kwenda kwenye mafanikio wanazidi kukudidimiza kwa kukuona mkombozi wa ukoo wakati bado haujaota mizizi.
Yaa unaweza kupata vihela ukasema ngoja niwasaidie saidie, bajeti zako zikibana ukashindwa kuwasaidia kama mwanzo hizo lawama zitakazotoka huko siyo za dunia hii, hadi utaambiwa mkeo kakuroga ili usiwasaidie, umaskini kwenye jamii za kiafrika ni mtihani mkubwa.Saidia kiasi unachoweza huwezi kumridhisha mwanadamu.
Halafu wakishazoea kupewa kila wakiomba wanaambizana na foleni inaongezeka. Siku usipowapa utakoma.
Kweli kabisa mkuu unapokaribia mwisho wa mwezi simu zinakuwa nyingi nyingi mwingine anakwambia nilitaka nikusalimie tu kumbe anakuandaa kisaikolojia mwisho wa mwezi akupige kizinga, imefikia hatua nimeshaogopa kupokea simu za watu ninao wafahamu kwa kuhofia kuombwa pesaNa waajiriwa ndo wana balaa kubwa, ikishafika mwisho wa mwezi simu zinaanza kupigwa. Unaweza kupata kiasi fulani cha pesa, wakati unatafakari kufanyia ishu zako, simu ya kuomba msaada inaingia, wakati mwingine kuna roho ambazo zinakusudia kukukwamisha. Wewe fanya mambo yako unavyofikiria, lawama za hao ndugu waomba misaada zisikukwamishe kufikia malengo yako ya kimaisha
Badilisha no basi mambo yasiwe mengiKweli kabisa mkuu unapokaribia mwisho wa mwezi simu zinakuwa nyingi nyingi mwingine anakwambia nilitaka nikusalimie tu kumbe anakuandaa kisaikolojia mwisho wa mwezi akupige kizinga, imefikia hatua nimeshaogopa kupokea simu za watu ninao wafahamu kwa kuhofia kuombwa pesa
Halafu kuna wale ambao ni mfanyakazi kabisa ana mshahara wake, anakuazima tuseme elfu ishirini au hamsini lakini anachuna kurudisha, sijui ni kwamba anaiona ni pesa ndogo kwako au ndo kukosa ustaarabu.Kweli kabisa mkuu unapokaribia mwisho wa mwezi simu zinakuwa nyingi nyingi mwingine anakwambia nilitaka nikusalimie tu kumbe anakuandaa kisaikolojia mwisho wa mwezi akupige kizinga, imefikia hatua nimeshaogopa kupokea simu za watu ninao wafahamu kwa kuhofia kuombwa pesa
Mi naona wanataka kubadilisha maisha yao kupitia mgongo wangu, wengi wao wanatunga uongo wa mambo makubwa makubwa ili tu wakunase kumbe wanaenda kushughulikia mambo madogo madogo kwenye familia zaoInaonekana elimu yako huitumii vzr, uogope lawama ama usiogope still zitakuwa palepale.
Wa kuwasaidia ni ndugu zako wa damu na wazazi tuu. Hao wengine saidia endapo kuna tatizo kubwa mfano kuugua, kufiwa, ajali n.k lakini sio eti kila ndugu anakuomba vocha na ww unakubali kuwapa.
Mfano Ndugu akija anaaomba pesa mwanae anaumwa usitoe pesa mpaka uhakikishe kweli mwanae anaumwa na yeye kamuuguza mpaka amefikia mahali amekwama. Yani hakikisha kwanza yeye kama yeye kashafanya efforts zimegonga mwamba ndipo kweli umsaidie.
Sio mtoto kaugua mafua tuu eti ndugu anakuomba pesa ampeleke hospitali wakati yeye hajafanya efforts zozote za kutafuta pesa. Shubamiiittt[emoji49]
Unforgetable
Asante sana kwa ushauri mkuu
Nimejaribu hilo mpaka sasa ninazo line 4 lakini cha ajabu zote wanazo walitoa kwa bi mkubwaBadilisha no basi mambo yasiwe mengi
Umeeleza vizuri sana sina budi kusema asante kwa ushauri huu mzuri ulionipaMkuu ukitaka kufanikiwa jiandae ku-sacrifice bahadhi ya mambo, either watu, vitu ama tabia fulani, nilikuja kugundua hilo too late nikiwa second year chuo maana nilikuwa natuma hela home sana aisee kwa ndugu ndo usiseme hizi hamsini, laki laki mbili mpka laki tatu nimetuma sana tu, but nilijifunza kitu mkuu,
katika maisha hatakama una roho ya huruma na nia ya kusaidia watu, sikuzote jaribu kutumia hekima, huwezi msaidia mwingine ilihali wewe huna uwezo wa kutatua hata bahadhi ya matatizo yako mwenyewe, yaani unatengeneza jina kwingine huku unaumia na kujilaumu na huu siyo msaada wenye baraka, sikuzote fanya kile kilicho ndani ya uwezo wako, usijaribu kutoa msaada ambao unazidi uwezo, utaumia na hutoona baraka za misaada hiyo kwasababu utakuwa ni wa kujilaumu kama hivi, so angalia uwezo wako, thathmini malengo yako ya baadae, jipangie bajeti yako kisha angalia kipi niweke wapi na kwasababu gani, baada ya hapo mtu akikutafuta mwambie ukweli huna hela, acha kuwa "Mr.nice guy" hutotoboa haya maisha leo wala kesho kwasababu wanaokuangalia wengi.
Naomba kunukuu kutoka kwa mzee wangu wa busara.
"Kijana wangu Mr.Purpose, ukitaka kufanikiwa katika maisha ni lazima uwe na roho ngumu na ya tofauti ambayo wengi hutafsiri kama roho mbaya. Hakuna haki duniani, na maisha hayapo fair, jiangalie wewe kwanza, jitengenezee mazingira kisha Mungu akikufungulia njia hapo sasa watengenezee na wengine kadiri ya uwezo wako kwa wakati huo. Kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kama mwanaume kulingana na malengo uliyonayo kwasasa na kwa baadae pia"
Mwisho wa kunukuu.
Mkuu wema usizidi kipimo, fanya maamuzi ambayo wewe hayatokuumiza na kujutia. Kila la kheri boss.
Nimekupa vilivyo mkuuBadili no zako zote za sm then wazijue wazazi wako pekee baada ya hapo wakanye kuwa siku wakigawa no yako utabadili na wao pia hutawapa so hawatakupata
So utabaki kusaidia wazazi wako tu kwa siri
Tumia 3-5 yrs kujipanga
Ukishakuwa sawa unaweza acha wajue no yako
Ndg yangu ukijifanya yesu mtoa misaada utakufa maskini
Wakat mwimgine roho mbaya ni nzur hata Bible inasema usitoe zaid ya uwezo wako
Unadhan ukiwanyima ndo utakuwa na dhambi?
Sasa endelea kuwa maskini
Hiki kipande kimenifurahisha sanaUnawaendekeza
Mimi nilipoamua kutafuta maisha hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuwasiliana na mm mpk wazazi wangu for 5yrs nilipotoboa ndo nikaruhusu mawsiliano but kwenye kutoa nikawa katili atlast wamenizoea kuwa hela yangu haupat bure labda baba na mama yangu pekeew
Weka fungu fulani maalum la kusaidia watu kila mwezi, kwa mujibu wa uwezo wako.Wakubwa zangu hebu tusaidiane katika hili,
Ndugu, jamaa na marafiki wanachangia kunikwamisha kupiga hatua za kimaendeleo.
Mwanzoni nilitamani sana kuwa muajiriwa baada ya kumaliza masomo yangu hatimaye kilio changu kikasikika kwa aliye juu, kama miezi saba hivi iliyopita nimetinga rasmi ajirani. Lakini ninayokutana nayo huku ni Mungu tu asaidie.
Baada ya ndugu tu kusikia nimelamba keki ya taifa sasa macho yote na masikio yote yameelekezwa kwangu simu na jumbe za kuomba pesa hazikauki kila unapokaribia mwisho wa mwezi. Hapo bado wana niliosoma nao (classmates) na washikaji niliowaacha kitaa. Meseji za "mwanangu nitoe ya vocha, mwanangu naomba nisave kiasi kadhaa" ni za kufikia. Wengine wanakuja kwa style ya kukopa then wanalala mbele mazima kwa kuwa ni ndugu unaamua kukaushia
Kibaya zaidi wengine wanaoomba ni watu wazima kabisa na familia zao mpaka unabaki kujiuliza maswali yasiyo na majibu, hivi wakati hujajiriwa walimudu vipi kulea familia zao? Waliishije? Au ni kutafutiana lawama tu ili mtu uonekane husaidii watu? Au labda kwa kuwa sijaoa wala sina mtoto wanafikiri sina majukumu?
Yes, labda wanafikiri sina majukumu lakini wanashindwa kutambua huu ndio muda wangu wa kujipanga hata mimi natamani niwe na familia kama wao nafanya kila jitihada ya kusave per month ili one day wanangu waje kuishi maisha safi wasiishi maisha niliyopitia mimi wakati nayafanya haya ndugu nao hawako nyuma kuhakikisha ndoto yangu hii haitimii wao kila kukicha ni shida zisizoisha wengine wana watoto wakubwa kabisa tunaolingana nao umri wengine nawazidi kidogo lakini wote wananitegemea mimi kuanzia baba mpaka mtoto.
Just imagine katika mazingira kama haya mtu unatokaje kimaisha? Kumbuka wanaokutegemea siyo hao tu. Infact imefikia point nimeanza kuchukia ajira yangu naona bora nisingeajiriwa tu kuepuka kubebeshwa kapu la lawama nililo nalo kwa sasa. Kila nikijitahidi kusave hamna ninachoambulia kila mmoja anataka nimtatulie shida zake.
I thought baada ya kuajiriwa nitadeal with only my parent kumbe nilikuwa najidanganya kuna kundi kubwa nyuma yangu yaani hawajui kabisa kama nadaiwa mamilioni ya pesa na Bodi ya Mikopo?
Kwa kifupi mambo yako hivo, labda tushauriane ndugu zangu mlionitangulia nyie mliwazaje kupambana na changamoto kama hizi mambo yakawa sawia bila ya kumuumiza mwingine?
ijapanda hata daraja nyie mmeshanigeuza Saccoss. Bandugu muwe na huruma hizi zama za magu siyo za kuombana hela kila wakati, kila mmoja apambane na stress zake
Jibu ni moja tu sinaMkuu wakipiga simu sema da sasa hivi wamechelewa umetoka kumtumia mtu pesa so umefulia akipiga mwingine jibu liwe hilo hilo watachoka wenyewe msaidie mtu aliyekupa hela kipindi unasoma tu wengine piga chini. Wakizidi sema umetoka kulipa kodi ya nyumba so uko vibaya au sema kuna mtu ulimkopa ndio umetoka kumlipa so huna hata mia
Mzee inaonekana umewaendekeza siku wa actie una kesi mahakamani ya uhujumu uchumi, dhamana ni mali isiyo hamishika ndugu ajitolee. utanipa mrejesho.Wakubwa zangu hebu tusaidiane katika hili,