Mkuu ukitaka kufanikiwa jiandae ku-sacrifice bahadhi ya mambo, either watu, vitu ama tabia fulani, nilikuja kugundua hilo too late nikiwa second year chuo maana nilikuwa natuma hela home sana aisee kwa ndugu ndo usiseme hizi hamsini, laki laki mbili mpka laki tatu nimetuma sana tu, but nilijifunza kitu mkuu,
katika maisha hatakama una roho ya huruma na nia ya kusaidia watu, sikuzote jaribu kutumia hekima, huwezi msaidia mwingine ilihali wewe huna uwezo wa kutatua hata bahadhi ya matatizo yako mwenyewe, yaani unatengeneza jina kwingine huku unaumia na kujilaumu na huu siyo msaada wenye baraka, sikuzote fanya kile kilicho ndani ya uwezo wako, usijaribu kutoa msaada ambao unazidi uwezo, utaumia na hutoona baraka za misaada hiyo kwasababu utakuwa ni wa kujilaumu kama hivi, so angalia uwezo wako, thathmini malengo yako ya baadae, jipangie bajeti yako kisha angalia kipi niweke wapi na kwasababu gani, baada ya hapo mtu akikutafuta mwambie ukweli huna hela, acha kuwa "Mr.nice guy" hutotoboa haya maisha leo wala kesho kwasababu wanaokuangalia wengi.
Naomba kunukuu kutoka kwa mzee wangu wa busara.
"Kijana wangu Mr.Purpose, ukitaka kufanikiwa katika maisha ni lazima uwe na roho ngumu na ya tofauti ambayo wengi hutafsiri kama roho mbaya. Hakuna haki duniani, na maisha hayapo fair, jiangalie wewe kwanza, jitengenezee mazingira kisha Mungu akikufungulia njia hapo sasa watengenezee na wengine kadiri ya uwezo wako kwa wakati huo. Kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kama mwanaume kulingana na malengo uliyonayo kwasasa na kwa baadae pia"
Mwisho wa kunukuu.
Mkuu wema usizidi kipimo, fanya maamuzi ambayo wewe hayatokuumiza na kujutia. Kila la kheri boss.