Jensen salamone
JF-Expert Member
- Sep 28, 2019
- 320
- 642
- Thread starter
- #181
hii kitu sijawahi kufikiria, kuweka ndugu kabisa kwenye biashara?Kwa mfano una kampuni ambayo ina branches kila tawi unaweka ndugu hata mmoja
hii kitu sijawahi kufikiria, kuweka ndugu kabisa kwenye biashara?Kwa mfano una kampuni ambayo ina branches kila tawi unaweka ndugu hata mmoja
Asante kwa ushauri mzuri chief [emoji120][emoji120]Bro, umeandika kwa uchungu sana. Kama nakuona vile.
Kikubwa bwana "do your things first". You can't save everyone! Jesus the saviour had died for them, so you are not Jesus ( kama una imani ya kikristu).
Unaweza saidia wale waliopo katika vicinity yako, hasa wazazi wako pamoja na ndugu zako wa karibu. Amini hili ni kundi pekee linalokutakia mema na limekuwa nawe wakati wote. Usiumize sana kichwa na hao wanaofumuka kama volkano baada ya kuona una ajira/mafanikio.
"You can do more by first puting yourself into a strong position, have a limit to your kindness"
Tumia nafasi yako kujiimarisha kwanza. Kusaidia watu ni jambo zuri, lakini wema usizidi uwezo wako.
Hawajawahi kuchangia chochote kwenye elimu yangu ni wazazi wangu pekee walihusika kwa 100% tangu nimeanza chekechea mpaka nimemaliza
Sikiliza bwana mdogo, SERIKALI YA MTU NI KICHWA CHAKE MWENYEWE na wewe ndio muamuzi wa maisha yako. Waswahili sio watu wa kucheka nao, wakijikata hata na kiwembe wakati wa kukata kucha watalalama utadhani wamefanyiwa operesheni ya figo, FANYA HIVI:Hawa ndugu zangu wana lawama balaa usipo wageia kidogo ni matatizo ila sasa imefikia point na mimi nimechoka kutegemewa kwa kila kitu sasa make naona ndoto zangu hazitotimia kwa mwendo huu ila sasa nifanyeje kuepukana na hii hali kiasi kwamba uamuzi wangu usimkere wala kumuumiza mtu? Shida ndo iko hapo
Nice words.Bro, umeandika kwa uchungu sana. Kama nakuona vile.
Kikubwa bwana "do your things first". You can't save everyone! Jesus the saviour had died for them, so you are not Jesus ( kama una imani ya kikristu).
Unaweza saidia wale waliopo katika vicinity yako, hasa wazazi wako pamoja na ndugu zako wa karibu. Amini hili ni kundi pekee linalokutakia mema na limekuwa nawe wakati wote. Usiumize sana kichwa na hao wanaofumuka kama volkano baada ya kuona una ajira/mafanikio.
"You can do more by first puting yourself into a strong position, have a limit to your kindness"
Tumia nafasi yako kujiimarisha kwanza. Kusaidia watu ni jambo zuri, lakini wema usizidi uwezo wako.
Ushauri mzuri.Mkuu ukitaka kufanikiwa jiandae ku-sacrifice bahadhi ya mambo, either watu, vitu ama tabia fulani, nilikuja kugundua hilo too late nikiwa second year chuo maana nilikuwa natuma hela home sana aisee kwa ndugu ndo usiseme hizi hamsini, laki laki mbili mpka laki tatu nimetuma sana tu, but nilijifunza kitu mkuu,
katika maisha hatakama una roho ya huruma na nia ya kusaidia watu, sikuzote jaribu kutumia hekima, huwezi msaidia mwingine ilihali wewe huna uwezo wa kutatua hata bahadhi ya matatizo yako mwenyewe, yaani unatengeneza jina kwingine huku unaumia na kujilaumu na huu siyo msaada wenye baraka, sikuzote fanya kile kilicho ndani ya uwezo wako, usijaribu kutoa msaada ambao unazidi uwezo, utaumia na hutoona baraka za misaada hiyo kwasababu utakuwa ni wa kujilaumu kama hivi, so angalia uwezo wako, thathmini malengo yako ya baadae, jipangie bajeti yako kisha angalia kipi niweke wapi na kwasababu gani, baada ya hapo mtu akikutafuta mwambie ukweli huna hela, acha kuwa "Mr.nice guy" hutotoboa haya maisha leo wala kesho kwasababu wanaokuangalia wengi.
Naomba kunukuu kutoka kwa mzee wangu wa busara.
"Kijana wangu Mr.Purpose, ukitaka kufanikiwa katika maisha ni lazima uwe na roho ngumu na ya tofauti ambayo wengi hutafsiri kama roho mbaya. Hakuna haki duniani, na maisha hayapo fair, jiangalie wewe kwanza, jitengenezee mazingira kisha Mungu akikufungulia njia hapo sasa watengenezee na wengine kadiri ya uwezo wako kwa wakati huo. Kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kama mwanaume kulingana na malengo uliyonayo kwasasa na kwa baadae pia"
Mwisho wa kunukuu.
Mkuu wema usizidi kipimo, fanya maamuzi ambayo wewe hayatokuumiza na kujutia. Kila la kheri boss.
Mwanzoni nilitamani sana kuwa muajiriwa baada ya kumaliza masomo yangu hatimaye kilio changu kikasikika kwa aliye juu, kama miezi saba hivi iliyopita nimetinga rasmi ajirani. Lakini ninayokutana nayo huku ni Mungu tu asaidie.