Ila ndugu wengine wana mambo ya ki$$enge sana.
Kwao udugu wenu unakuwa wa maana pale uwezapo kumsadia shida zake.
Kila unapopigwa mzinga na wewe unatoa tu bila kusita na bila maswali ya kipolisi, unaonekana ni ndugu mwenye faida na wa maana sana.
Siku utayosema huwezi kusaidia, udugu ni kama unaisha.
Haya mambo ni magumu sana.
Majitu mengine hata hayataki kujishughulisha, hayataki kufanya baadhi ya kazi, lakini kwenye kuomba omba ndo yanaongoza.
Jitu halina kazi. Na wala halijishughulishi kutafuta kazi. Ukiliambia au ukiliuliza kuwa kwa nini usifanye hata kazi za ujenzi au hata dei waka zingine, linaona kama umelidharau vile.
Linajiona liko juu ya hizo kazi. Lakini halioni aibu kuomba omba.
Halafu sasa majitu kama hayo huwaga hayana shukurani. Msaada wako kwake linaona kama ndo stahili yake.
I’m done helping thankless and ungrateful muthaefferz.
Done. Completely done.
Mimi watu wa ovyo hata kuniomba hela wanaogopa, kwa sababu wanajua nitawauliza business plan.
Niko radhi nimpe mtu mwenye business plan nzuri mamilioni ya shilingi aende kufanya kweli kwenye business, kuliko kumpa mtu asiyeaminika laki.
Kwa sababu huyo wa business plan unamuwezesha asimame mwenyewe na kusaidia wengine, si kila siku aombe laki laki bila kufanya kitu cha maendeleo.
Ukisema uwafungie vioo wala sikulaumu. Ila mimi nina kanuni ya kuangalia vitu vitatu.
1. Need. What is the need? Kuna vitu kama ugonjwa na misiba, kuvikatalia, hususan kama uwezo unao, ni vigumu.
2. Character. Character ya muombaji ikoje? Ni mtu wa karibu unamjua au anadanga tu? Ni mtu anayejiheshimu si ombaomba wa tabia? Ni mtu wa kuaminika kwamba akikuambia jambo anasema kweli? Maana hela nyingine unaweza kuona unatoa msaada, kumbe unampa teja anajidunga anaaga dunia. Hela yako ndiyo imemsaidia kuondoka duniani.
3.Merit. Does the person deserve it? Inawezekana mtu ni mtu wako wa karibu, lakini anachukulia vitu for granted. Mara nyingine tough love inajenga character. Inawezekana mtu humjui sana, lakini ana story ina merit sana ina deserve kusaidiwa. Inawezekana mtu anatafuta hela ya kulewa tu, hata hana shida nayo sana, ila kakuona wewe ndiye bwege mtozeni.
Mtu akiwa na need, na character na merit, kinachobaki ni kimoja tu kwangu.
4. Ability. Je, nina uwezo wa kumsaidia bila mimi mambo yangu kutetereka?
Kama jibu ni ndiyo, kuna step moja ya zaidi.
5. Kuhakiki habari zote nilizopewa kwa vyanzo tofauti. Si mtu anakwambia anafungua biashara halafu ukihakiki unaona hakuna kitu kama hicho.
Akipita uhakiki mkali kama wa wafanyakazi wa serikali ya Tanzania, hapo nakuwa sina hiyana.
Hizi hela hatuwezi kuondoka nazo dunia hii.