Jensen salamone
JF-Expert Member
- Sep 28, 2019
- 320
- 642
Wakubwa zangu hebu tusaidiane katika hili,
Ndugu, jamaa na marafiki wanachangia kunikwamisha kupiga hatua za kimaendeleo.
Mwanzoni nilitamani sana kuwa muajiriwa baada ya kumaliza masomo yangu hatimaye kilio changu kikasikika kwa aliye juu, kama miezi saba hivi iliyopita nimetinga rasmi ajirani. Lakini ninayokutana nayo huku ni Mungu tu asaidie.
Baada ya ndugu tu kusikia nimelamba keki ya taifa sasa macho yote na masikio yote yameelekezwa kwangu simu na jumbe za kuomba pesa hazikauki kila unapokaribia mwisho wa mwezi. Hapo bado wana niliosoma nao (classmates) na washikaji niliowaacha kitaa. Meseji za "mwanangu nitoe ya vocha, mwanangu naomba nisave kiasi kadhaa" ni za kufikia. Wengine wanakuja kwa style ya kukopa then wanalala mbele mazima kwa kuwa ni ndugu unaamua kukaushia
Kibaya zaidi wengine wanaoomba ni watu wazima kabisa na familia zao mpaka unabaki kujiuliza maswali yasiyo na majibu, hivi wakati hujajiriwa walimudu vipi kulea familia zao? Waliishije? Au ni kutafutiana lawama tu ili mtu uonekane husaidii watu? Au labda kwa kuwa sijaoa wala sina mtoto wanafikiri sina majukumu?
Yes, labda wanafikiri sina majukumu lakini wanashindwa kutambua huu ndio muda wangu wa kujipanga hata mimi natamani niwe na familia kama wao nafanya kila jitihada ya kusave per month ili one day wanangu waje kuishi maisha safi wasiishi maisha niliyopitia mimi wakati nayafanya haya ndugu nao hawako nyuma kuhakikisha ndoto yangu hii haitimii wao kila kukicha ni shida zisizoisha wengine wana watoto wakubwa kabisa tunaolingana nao umri wengine nawazidi kidogo lakini wote wananitegemea mimi kuanzia baba mpaka mtoto.
Just imagine katika mazingira kama haya mtu unatokaje kimaisha? Kumbuka wanaokutegemea siyo hao tu. Infact imefikia point nimeanza kuchukia ajira yangu naona bora nisingeajiriwa tu kuepuka kubebeshwa kapu la lawama nililo nalo kwa sasa. Kila nikijitahidi kusave hamna ninachoambulia kila mmoja anataka nimtatulie shida zake.
I thought baada ya kuajiriwa nitadeal with only my parent kumbe nilikuwa najidanganya kuna kundi kubwa nyuma yangu yaani hawajui kabisa kama nadaiwa mamilioni ya pesa na Bodi ya Mikopo?
Kwa kifupi mambo yako hivo, labda tushauriane ndugu zangu mlionitangulia nyie mliwazaje kupambana na changamoto kama hizi mambo yakawa sawia bila ya kumuumiza mwingine?
Sijapanda hata daraja nyie mmeshanigeuza Saccoss. Bandugu muwe na huruma hizi zama za Magufuli siyo za kuombana hela kila wakati, kila mmoja apambane na stress zake