Ndugu wanachangia kunirudisha nyuma kimaendeleo

Ndugu wanachangia kunirudisha nyuma kimaendeleo

ndugu mnawaponda , lakini ukiumwa uko hoi kitandani ndio watakuhudumia, siku ukiwa na familia , halafu ufiwe ndio utakapoona umuhimu wa ndugu, hata yule ndugu yako masikini kabisa utataka aje , halaf sasa kwenye msiba ndugu zako wasipokuja, marafiki, wafanyakaz wenzako watakusimanga kweli kweli! tuwapende ndugu, pesa / mali utakufa utaziacha
Udugu ni jambo jema, na kusaidiana katika shida kama maradhi, kesi na kifo ni jambo muhimu na hatupasi kulipuuza hata kidogo. Lkn suala la kuombana hela kwa ajili ya matatizo madogo madogo tu si la kuliendekeza kwasababu kila mtu hayo matatizo madogo anayo na hayawezi kwisha
 
Umeweka ukaribu na ndugu wengi ambao hawana faida ivi kipi kinakufanya umpigie mjomba, shangazi, bibi, kila wiki au kila mwezi simu unaisi hawatakuomba pesa bqdilisha namba weka baba mama na ndugu wachache ambao aya ukiwa na shida wanaweza kukusaidia hii dunia ukiwa na huruma sana tegemea maumivu yasiyoisha
 
Jifunze kuishi kwa saound (uwongo) kijana kua muigizaji tunga matatizo ya uwongo wape promise za uwongo yan wavute karibu waone kama vile ni mambo tu hayajakaa sawa lakini una nia ya dhati kuwasaidia

Uwe unawasoma psychology yao ukigungua tu hii simu n ya kuomba pesa pokea halafu anza wewe kutaja mahitaji yako ya kipesa huku ukitaman kama ungepata mtu wa kukukopesha yani hvyo ukijifanya baba huruma utakufa maskini
😂😂😂😂😂 dah! Yote ya nini hayo? Kamwe usiweke promise usiyo na malengo ya kuitimiza, kwani ukijibu sina watakuua?!!
 
Panga vitu unavyotaka kufanya ukipata hela nunua au fanya moja kwa moja hutobaki na hela ukiombwa hutokua na cha kuwapa
 
Dawa mtu akikuomba pesa mwambie nakuazima, siku nyingine akirudi kukopa mwambie kumbuka nakudai nilipe kwanza hela yangu then nikupe hapo utawakata vilimi
 
Miezi saba tu umeshaanza kupiga kelele....
 
Ukishapata na mke utaombwa sehemu mbili...
 
Ukishapata na mke utaombwa sehemu mbili...
Nikishatoa mahari kwao na mwanamke biashara ya kifedha inakuwa imejifungia hapo zaidi zaidi labda kuwe na shida kubwa kabisa ya kuhitaji msaada wa hali na mali tofauti na hapo siwezi
 
Mungu hapendi unavyolalamika. Fanya kadri moyo wako unavyoona. Ujuwe hata hiyo ajira hautadumu maana umeshajilaani. Fanya toba pia.
 
Hawa ndugu zangu wana lawama balaa usipo wageia kidogo ni matatizo ila sasa imefikia point na mimi nimechoka kutegemewa kwa kila kitu sasa make naona ndoto zangu hazitotimia kwa mwendo huu ila sasa nifanyeje kuepukana na hii hali kiasi kwamba uamuzi wangu usimkere wala kumuumiza mtu? Shida ndo iko hapo
Dah..Kama unazo za kutosha wape TU ndugu wa karibu Sana pamoja na madem zako....Hao wengine wafungulie group la WhatsApp liite WAVIZINGA atakaye left ndiyo amajileftisha mazima....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Au kila atakayekupiga mzinga mwambie aje kuchukua nyumbani...hata wale wa mbali watumie nauli.....kisha wape appointment ya muda sawa wote...bandika list ya vizinga vyao kwenye mlango wa kuingilia ndani....halafu nunua kreti zako 2 za soda...mpe kila mgeni....baada ya hapo utaishi kwa raha[emoji2960]
 
Back
Top Bottom