Hapo nimeanza kumuelewa..
Ndoa nyingi zinavunjwa na ndugu na wazazi...
Ndio maana saa nyingine ukijua tabia ya ndugu zako unatakiwa usiwaweke karibu na ndoa yako...
Ingawa kuna ndugu wenye busara pia..
Najua ikija kwenye elimu ndugu wengi huo utakuwa ushauri wao...
Nakumbuka dada yangu alipata chance ya kusoma Ph.D mume wake akawa hataki...wakati yeye pia ni Ph.D holder...
Dada angu akukubali akasema ntasoma tu utake usitake...ila akasema sitaenda soma nje ntasomea hapa hapa ntakuwa na joint registration na chuo cha US ili muda mwingi niwe TZ...
Mumewe akaenda kumshitaki kwa baba...
Baba angu akamsema sana dada yangu kuwa si vizuri kujiamulia mambo bila kupata baraka za mumeo...dada yangu mpaka alilia mbele ya baba siku hiyo...hakuamini...
Baada ya siku moja baba kampigia simu dada yangu anamwambia, 'wewe ulitegemea niseme nini kwa mkwe wangu...acha ujinga nenda shule...yeye mbona msomi'
Kweli dada yangu sasa ana Ph.D na ndoa bado anayo...lakini she was ready for anything kwani alimuona mumewe selfish ...ila na baba nae ndio aliua kabisa...
Afu tukienda kwa baba anatusimulia huku anacheka xxx(shemeji yetu) anachekesha sana; anaogopa mkewe kusoma kwa kuwa watalingana...