Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,128
- 8,058
Ndoa ni agano takatifu linalomuunganisha mwanaume na mwanamke mbele za Mungu. Hata hivyo, ndoa nyingi zimevunjika au zimejaa migogoro mikubwa isiyoelezeka, kiasi cha kuwafanya wengine wafikirie kukataa ndoa.
Matatizo ya ndoa wakati mwingine chanzo chake ni cha kiroho. Biblia inatufundisha kuwa katika ulimwengu wa roho kuna falme, mamlaka za giza na majeshi ya pepo wabaya (Waefeso 6:12). Miongoni mwa mapepo hayo kuna mapepo yaliyojikita kuharibu au kuvunja ndoa tu. Katika mada hii, hebu tujifunze kuhusu mapepo hayo, namna yanavyofanya kazi, na jinsi ya kuyashinda.
1. Pepo la Mafarakano
Hili ndilo pepo linaloleta mgawanyiko, kutokuaminiana, na maamuzi ya haraka ya kuachana. Huchochea mizozo midogo kuwa mikubwa na hufanya mme amuone mke wake ni adui na mke naye anamuona mme wake ni adui.
Ukiona dalili hizi ujue pepo la mafarakano limeingilia ndoa yenu: Kutoelewana kwa kila jambo dogo, hasira zisizoelezeka na uamuzi wa kutengana.
2. Pepo la Kiburi na Majivuno
Hili ni pepo linalowafanya wanandoa washindwe kuomba msamaha au kukubali makosa yao. Hufanya kila mtu ajione yuko sahihi muda wote.
Dalili: Kukataa ushauri, kutotii, kuendekeza visasi na kushindwa kuwa mnyenyekevu.
3. Pepo la Uzinzi na Tamaa ya Mwili
Hili ni mojawapo ya mapepo yanayoharibu ndoa. Ni pepo linaloingiza tamaa ya mme au mke kutoka nje ya ndoa na kuchochea mahusiano ya nje ya ndoa.
Dalili: Kutokuwa na hamu ya mwenzi wa ndoa, kulinganisha mume/mke na watu wa nje, kutazama ponografia, na usaliti.
4. Pepo la Ubaguzi na Ukosefu wa Upendo
Pepo hili husababisha upendeleo wa watoto, kutowajali wazazi wa mwenza, au kuona mwenzi hana thamani.
Dalili: Maneno ya dharau, ukosefu wa huruma, na kukosa kushirikiana majukumu ya ndoa.
5. Pepo la Uvivu na Usingizi
Hili ni pepo linalozuia maombi au kuleta usingizi wakati wa ibada ya pamoja nyumbani, au wanandoa wanapotaka kusoma Biblia. Wanandoa wanapokosa kujenga msingi wa kiroho pamoja, mapepo yanapata nafasi.
Dalili: Kukosa hamu ya maombi ya pamoja, kuchoka kiroho, na kukwepa ushauri wa kiroho.
6. Pepo la Fedha na Uchumi
Mapepo haya huchochea migogoro katika matumizi ya fedha au kutoridhika na hali ya kifedha ya mwenza.
Dalili: Kugombania mshahara, kutokuwa wazi kifedha, au kunung’unika juu ya hali ya maisha.
7. Pepo la Mauti
Hili ni pepo hatari sana linalotenda kazi katika mazingira ya huzuni kali, kukata tamaa, au hasira ya kupindukia ndani ya ndoa. Linaweza kumshawishi mmoja wa wanandoa ajiue, au atake kumuua mwenza wake.
Dalili: Kauli za kukata tamaa kama vile "afadhali nife", vitisho vya kujiua au kuua, vurugu kali, au hata kufanya maandalizi ya kujiua.
Katika Yohana 10:10 tunasoma: “Mwivi haji ila aibe na kuua na kuharibu; mimi nalikuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele.” Mwizi anayetajwa hapo ni shetani/mapepo. Mojawapo ya kazi zao ni kuwashawishi watu wajiue.
Katika sehemu inayofuata tutaangalia jinsi ya Kupambana na Mapepo Hayo...