Ndege mpya za serikali ziko njiani kuja

Ndege mpya za serikali ziko njiani kuja

Kuna mtu kamzuia asifanye kazi?
Ndio kuna watu kila kukicha wao ni kumpinga tu Rais, wanamzuia kwa vijimaneno vyao visivyokuwa na maana. Rais Magufuli anafanya kazi nzuri lakini kuna watu wenye chuki binafsi, wanajifanya hawaoni, hawasikii. Narudia kuandika tena; Rais Magufuli, fanya kazi baba wala usiyumbishwe na kelele za vyura.
 
si
Acha mawazo potofu wewe, fanya kazi na utakula chakula. Nani kakuambia pesa za kununulia ndege ni za kukununulia wewe chakula? Usipofanya kazi utakaa na njaa yako.

sijasema mimi nina njaa nasema wenye njaa walioteketezwa huko bukoba kwasababu serikali imekula pesa zao za misaada na zingine wamenunua mitumba ya ndege laana za wana bukoba zitawafika tu na natumaini hiyo mitumba ya ndege haitaendelea kamwe in 1 yrs hizo ndio laana za wahanga wa Bukoba.


swissme
 
We nae tumia akili kidogo. Maendeleo kuja ni lazima ufuate vipaumbele sahihi. Ukianza kununua gari badala ya kusomesha watoto na kuwapa huduma bora za makuzi utajiri utaishia kwako. Wao watarudi umaskini tu.

Na hilo ndo tatizo kubwa la waswahili. Mnapenda sana show games na kuamini maendeleo yanakuja tu bila kusotewa.
Nani kakuambia watoto wa Watanzania hawasomi? Tena sasa hivi Elimu ni bure mpaka form 4. Mimi watoto wangu wanasoma, wa kwako hawasomi? Acheni kuishi maisha ya kukariri ninyi. Ndege zinazonunuliwa leo ni sehemu moja wapo ya uwekezaji. Siku ikifika ndege hizo zitaleta faida ambayo itatumiwa kwenye sekta zingine kama hiyo sekta ya elimu. Acha mawazo potofu wewe. Watu kama wewe ndio wale mnaokula mpaka mbegu kisa mnanjaa, matokeo yake mvua zikija hamna cha kupanda, mnabakia kuwa na njaa kali zaidi kuliko ile ya mwanzo. Tumia akili zako kijana.
 
si


sijasema mimi nina njaa nasema wenye njaa walioteketezwa huko bukoba kwasababu serikali imekula pesa zao za misaada na zingine wamenunua mitumba ya ndege laana za wana bukoba zitawafika tu na natumaini hiyo mitumba ya ndege haitaendelea kamwe in 1 yrs hizo ndio laana za wahanga wa Bukoba.


swissme
Laana ya kuku haimpati Mwewe hata siku moja. Huu ni ushabiki wa kitoto kabisa, eti, Serikali imekula pesa za misaada, hivi ninyi watu hata kufikiri tu kidogo mnashindwa? Pesa zilizopatikana zinatumika kujenga hospitali, shule na miundo mbinu iliyoharibiwa na tetemeko, tena pesa zenyewe hata hazitoshi. Hata kama zingegawiwa kwa waathirika, bado kila mmoja angepata kiasi kidogo sana ambacho kisingemsaidia chochote kile. Tumieni akili za kuzaliwa ninyi CHADOMOOOOO!
 
hujui chochote umekariri Chadema tu, wewe unachojua ni CCM na chadema basi...serikali inadai inataka iwapaishe masikini kwa kuwapunguzia matajiri, hapo hapo inanunua ndege nyingi kwa kipindi kifupi, ambazo wana afford matajiri, mwenye income ya kupanda hizo ndege atakuwa nani? wangepeleka umeme na barabara kijijini sio kununua ndege zitakazokosa wateja, fool
Akili za kitoto na ushabiki wa kitoto kabisa. Kama wewe huna pesa za kupanda ndege, shauri yako. By the way, Serikali hainunui ndege ili kila Mtanzania apande hizo ndege! Kenya wana shirika kubwa sana la ndege na wana ndege nyingi sana kutuzidi sisi, lakini je, Wakenya wote wana afford usafiri wa ndege?
Hizi ndege ni uwekezaji utakaoeleta faida kubwa hapo baadaye. Kuhusu ujenzi wa barabara na miundo mbinu mingine, hayo ni mambo ambayo yanafanyika. Umeme umeanza kupelekwa huko vijijini unakosema wewe au na hilo nalo hujui?? Kwa kifupi, Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kufanya mambo yote kwa mara moja. Kipaumbele kwa sasa ni kufufua shirika la ndege na mengine yatafuata baadaye. Hata hii dunia haikuumbwa kwa siku moja.
Tatizo lenu ninyi ni chuki tu za kisiasa ndio zinazowasumbua, na wengine mlikuwa mnaishi maisha kama mko "peponi" kwa pesa za "dili" sasa Magufuli amewatumbua mmebakia kumpinga tu humu JF.
Hata mpige kelele mpaka mchoke, ndege zitanunuliwa, Rais Magufuli atafanya alichoamua, na tena ataendelea kutawala mpaka 2025. Mtakoma ubishi.
Viva Magufuli, viva!
 
Siku zikitoa Bongo nazima tv yangu siku nzima maana kufanya mambo bila priority ni zaidi ya kero na maudhi matupu.

Ni kero na maudhi kumsikia mtu anajisifu kununua ndege kwa cash wakati wanafunzi wanakosa mikopo,madaktari na waalimu hawajiiriwa,madawa hospitalini shida,watumishi stahiki zao hawalipwi,watu wamesitishiwa ajira zao,wahanga wa tetemeko wanateseka,n.k.
Kama utatulia kidogo na kufikiria anachojaribu kufanya JPM ni kupunguza gharama ya uendeshaji ili kufidia maendeleo. Wakati wa awamu ya nne mambo yalikuwa mabaya mno kiasi recurrent expenditure ilikuwa maradufu ya development expenditure. Jifunze utawala kidogo. Hakuna nchi iliyoendelea kwa kujali kulisha watu na kuwastarehesha tu, kulipa stahiki za wale nk. Kuna wakati lazima uwe katili na kutazama 'bigger picture'. Watakaokufa waache wafe ila watakaobaki na watakaozaliwa wataishi vizuri. Nchi zote zimejitolea mhanga, tena saa nyingine kwa thamani ya kutisha! Leo mwaisifu China lakini hujui katika miaka ya 60-70 zaidi ya Wachina milioni 200 walikufa katika Cultural Revolution (nenda kasome hiyo). Leo yamewafaa au la?
Maadamu kuna taswira nzuri ya mustakbali, acha JPM aminye tu.
Tatizo la Miafrika iko so selfish ...wataka wafaidi wao tu, tena hivi sasa! Hakuna kufikiria mustakbali wa nchi au kizazi kijacho. Mlistarehe sana nyie chini ya JK!
Kwa hili endelea JPM, minya hadi kijulikane!
 
Nani kakuambia watoto wa Watanzania hawasomi? Tena sasa hivi Elimu ni bure mpaka form 4. Mimi watoto wangu wanasoma, wa kwako hawasomi? Acheni kuishi maisha ya kukariri ninyi. Ndege zinazonunuliwa leo ni sehemu moja wapo ya uwekezaji. Siku ikifika ndege hizo zitaleta faida ambayo itatumiwa kwenye sekta zingine kama hiyo sekta ya elimu. Acha mawazo potofu wewe. Watu kama wewe ndio wale mnaokula mpaka mbegu kisa mnanjaa, matokeo yake mvua zikija hamna cha kupanda, mnabakia kuwa na njaa kali zaidi kuliko ile ya mwanzo. Tumia akili zako kijana.
Nimemaliza kusomesha we dogo. Hiyo elimu bure wala sitaongelea hapa maana ni janga lingine.

Halafu mfano uliotoa unamuhusu alienunua ndege cash (kala mbegu) halafu anaomba msaada wa madawati (kulialia njaa).
 
Nafikiri dira imebadilika kutoka kuwa nchi ya viwanda mpaka kuwa nchi ya madege.
 
wanunue tu sisi tunakomalia ugali dagaa na dawa za kienyeji
 
Nimemaliza kusomesha we dogo. Hiyo elimu bure wala sitaongelea hapa maana ni janga lingine.

Halafu mfano uliotoa unamuhusu alienunua ndege cash (kala mbegu) halafu anaomba msaada wa madawati (kulialia njaa).
Mtalalama sana lakini hakuna kitakacho badilika. Ndege zitanunuliwa, na mengine mengi ya maendeleo yatafanyika, mpende msipende, Magufuli ndio Rais na yeye na Serikali yake wanafanya yale ambayo wanaamini ni muhimu kufanyika. Mimi namuunga mkono Rais wangu katika jitihada zake za kufufua shirika la ndege. Naamini sipo peke yangu, tunaomuunga mkono Rais Magufuli tupo wengi tu. Ninyi wafuasi wa CHADOMOO endeleeni kupiga domo.
Viva Magufuli, viva!
 
Very good move by JPM kuwa na airline kunaongeza sana GDP na kuitangaza nchi vizuri katika nyanja ya utalii nk. Huyu ndie rais anayewafaa Watnzania walipa kodi, sio wale wanaopiga magendo na kufikiria utajiri una njia ya mkato. Kuendele kwa nchi ni lazima kufunga mkanda na kuboresha kila nyanja.
 
Kwa budge ipi? Manake budget ya mwaka huu ilikuwa ni ndege mbili.... Sasa pesa za hizi nyingine zimeidhinishwa na nani?
 
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya kutengeneza ndege ya Bombardier yenye makao makuu nchini Canada kununua ndege tatu mpya miezi michache tangu iliponunua ndege mbili mpya za Bombardier Q400.

Ndege za CS300 zinauwezo wa kubeba abiria 150 kila moja tofauti na Q400 ambayo inabeba abiria 70.

Mkataba huo mpya unahusisha ununuzi wa ndege moja aina Bombardier Q400 inayotarajiwa kuwasili nchini mwakani na ndege nyingine mbili ni Bombardier CS300 ambazo haijajulikana zitawasili lini.



========

Bombardier CSeries will sell both the Government of Tanzania, which represents its first order in seven months for its new commercial aircraft.


In total, the transaction includes two CS300 and a Q400 aircraft. According to list prices, the order is valued at 203 million US.

The aircraft will be operated by Air Tanzania, the national airline of the United Republic of Tanzania.

The last order of CSeries was in April, when the US carrier Delta Air Lines has confirmed the purchase of 75 CS100 aircraft, a firm order valued according to catalog prices, is estimated at US $ 5.6 billion .

Monday, Bombardier had delivered its first CS300 – the largest device family CSeries aircraft – the Latvian carrier airBaltic, its launch customer.

cwynnlrucaacozw.jpg


This aircraft, which can carry up to 160 passengers, must make its first commercial link between Riga and Amsterdam on 14 December.

Overall, airBaltic ordered 20 Bombardier CS300 devices.

So far, the aircraft manufacturer and rolling stock received 360 firm orders for its new aircraft, including 235 for the CS300.


Source: The Quebec Telegram
Hapa kazi tu
 
Hapa Wachawi wa Maendeleo watakuja tu, na nimeona hapo Juu wameanza kulalamika, mtalalamika sana mwaka huu, na bado mwakani mtalia sana macho ya damu, lakini lazima Tununue Ndege.

Ninyi ndo awamu ya nne mlilalamika sana kuwa eti hata Rwanda wametuzidi, sasa mlidhani fedha za kununulia hizo ndege zingetoka wapi?

Lazima tufunge mkanda hadi malengo yetu yatimie, sasa hatutamsikiliza mtu tena hadi pale Ndege zetu zitakaponunuliwa, na bado Reli ya Standard gauge pesa zote zinaenda kwa kampuni husika, yaan mikanda tuliyojifunga tutaifungua mwaka 2019
ujumbe umewafikia mkuu.
 
Wakati tunapambana kupata maendeleo ya vitu tukumbuke maendeleo ya watu. Maendeleo ya vitu ni Barabara, Reli, Ndege, Meli nk. Maendeleo ya watu ni Elimu bora kwa wote, Huduma bora za afya, Ajira, Makazi, Chakula nk.
Waelekeze
 
Back
Top Bottom