Wiki chache zilizopita tulitangaziwa kuwa aliyekuwa makamu wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amejiuzulu nafasi hiyo. Siku chache baadaye CCM wakatutangazia kuwa wamemfukuza Nchimbi uanachama wa chama chao! Ajabu ni kuwa CCM katika taarifa yao kwa wanahabari hawakutoa fursa ya maswali.
Tangu tukio hilo kutokea Watanzania hawajapata fursa ya kumsikia wala kumuona Nchimbi mwenyewe hadharani; haijukikani kama yuko kizuizini, amekufa au yuko hai; waliojaribu kumtafuta kama alivyofanya mzee Warioba wanadai hata kwenye simu hapatikani!
Makamu wa Rais ni cheo kikubwa sana nchini, haiwezekani kutoweka bila wananchi kujua yuko wapi, huu ni uhalifu kwa taifa. Haifikiriki mtu kama Nchimbi kutoweka na kunyamazishwa kimyakimya bila serikali na au vyombo vya dola kutuambia yuko wapi.
Kuna tetesi kuwa Nchimbi hajajiuzulu; hii inaweza kuwa kweli kwa sababu yeye mwenyewe hajasikika wala kuonekana hadharani kulizungumzia suala hili. Ajabu kuu hakuna mamlaka wala taasisi yoyote imejitokeza kuhoji uhalali wa kuondolewa kwenye nafasi yake au hata mustakabali wa uhai wake; haijulikani kama yuko hai ama amekufa, kama ni mgonjwa au yuko kizuizini.
Mwaka 1984, wakati wa mfumo wa Chama kimoja, Aboud Jumbe aliyekuwa Makamu wa Rais JMT na rais wa Zanzibar alivuliwa umakamu wa raus wa JMT, urais wa Zanzibar na kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani hadi mauti yalipomkuta miaka ya 2000; angalau ilijulikana yuko wapi. Mwaka 2015, aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa, alijiuzulu na kuihama CCM, hatukuona kitu kama hiki maana aliendelea na harakati za kisiasa kama kawaida; sasa hili la Nchimbi mbona limekaa hivi? Watanzania wana haki ya kujua, kiongozi wao yuko wapi? Yuko hai? Yuko kizuizini? Yu mgonjwa?
Vv