Siri yangu
JF-Expert Member
- Jul 22, 2023
- 1,031
- 2,038
Mungu ibariki nchi hii na watu wake, Mungu mbariki mmiliki wa mtandao huu na timu nzima ya kazi inayofanywa hapa ili sisi tupate sehemu ya kutolea dukuduku zetu.
Ndugu zangu Kwa heshima na taadhima nipo mbele yenu nami kule kero yangu hapa kwa viongozi na wataalamu wetu tuliowapa nafasi watutumikie na wawe na maono ya kesho na mbele zaidi, hiyo picha hapo juu mnaoiona ni barabara za kutengenezwa kwa greda ambazo ni za mtaa.
Hapa ni manispaa ya Kahama mji ambao unakimbia kwa kasi ya ajabu sana, eneo hili lipo Mhungula karibu kabisaa na shule ya msingi Ilindi na ni Mbugani namaanisha mbuga kabisaa ya kulimia mpunga na nyakati za masika watu wanapata taabu kukatisha hayo maeneo.
Nimekuja kwenu na kuandika makala haya ili nijijue kama labda mimi ndio nimepungukiwa na akili au tuliowapa nafasi wamepungukiwa kidogo na sio sana, Mwaka 1998 wakati mvua kubwa na mpaka ikafikia kuitwa jina Elinino ilinyesha na maeneo haya ilikuwa ni kama bahari tu hakuna mtu aliekatiza hapa pembezoni kabisaa ndio kulilimwa mpunga na watu walivuna sana mwaka huo,.
Leo hii ukifika maeneo haya serikali imeruhusu watu kuwa na viwanja humo na kutoa vibali vya ujenzi katikati ya mbuga ambayo mvua kidogo tu maji yanajaa tena kwenye mikondo wa maji na watu wanajenga na halimashauri inabariki jambo hili.
Maswali yangu ya kijinga
1. Je, Tumejenga miundombinu ya kudhibiti maji siku ikitokea mvua kubwa?
2. Je, mmejiandaa na misaada kipindi wananchi wanapigwa na mafuriko haya?
2. Je, tumejiandaa kuja kuwalaumu wananchi wetu kuwa kwanini walijenga na ili hali ninyi ndio mnatoa vibali?
3. Je, tumeshawahi jiuliza iwapo mvua za Elinino zikija na kwa bahati mbaya ikaja usiku ikanyesha mvua kwa masaa 5 nini kitatokea kwenye nchi hii?
4. Watu wetu hawana elimu kabisaa na hawajawahi kuwaza mbali je tutawalaumu ?
5. Ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa unafurahia kuja kula posho na kutoa ahadi zisizotekelezeka kama Mwakata?
6. Au na hizi fedha za maafa mtazipiga kama mlivyopiga za Bukoba ?
7. Mwisho watu wa mipango miji mlienda kufanya nini shuleni au mnakula mishahara kwa kazi gani?
Maswali ni mengi sana naweza andika hadi kesho kutwa ila naomba niishie hapa kwa umri wangu mdogo huu naombeni kama nimekosea nikosoeni kwa staha na naomba msamaha.
Wenu katika ujenzi wa Taifa
Mpitimbi ndio kwetu ukipitia Ughandi