Blender
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 4,633
- 7,639
Kitendo cha kuagiza mchele nje ya nchi siyo kitendo cha kukiacha kipite hivi hivi tu kama ni jambo la kawaida na halina maana yoyote. Jambo hili ni ishara mbaya sana na siyo dalili nzuri sana huko tuendako kama taifa.
Haiingii akilini kabisa kuona nchi kama Tanzania eti tunaagiza mchele nje ya nchi! Yaani kivipi? Kwamba Tanzania imeshindwa kuzalisha mchele wa kutosha ? Kwamba Tanzania mavuno ya mpunga hayakuwa mazuri au ni nini? Kwamba idadi ya watu imeongezeka ghafla binu vuu? Kama haya ni sahihi sasa je? Zile takwimu tunasomewaga pale bungeni na waziri bashe huwa anazitoa wapi? anapika takwimu? Anadanganywa? Au ni nini haswa?
LAKINI haya tuliyaonya mwanzoni kuwa Tanzania inauza sana chakula nje ya nchi na mazao ya chakula yanasafirishwa sana kwenda nje ya nchi ,tukajibiwa kuwa hayo ni mambo ya soko la EAC na hatujui kitu tukae kimya.
Round ya Kwanza, Mwaka 2021-2022 tuliagiza Mchele from Japan.
Round ya pili, 2024.
Sasa ivi tunaagiza kutoka India, wa Indi wenye maghala ya kuhifadhia chakula hapa Dar watapiga Sana mpunga kupitia Wazir bashe
Hali hii ni ishara mbaya sana na siyo ya kubeza kwa kuwa tunajua muda wowote tutatangaziwa kuwa kuwa uhaba wa mafuta ya kupikia nchini. Tulishakuwa na uhaba wa kila kitu hii ni dalili kuwa uchumi wa nchi yetu una suffocate na taifa liko kwenye CRISIS. Tujipange mapema na hakuna haja ya kufichaficha mambo.
Ivi ni lini SSH atakuja kugundua kuwa bashe anafanya biashara ya chakula kupitia wafanya biashara wa kubwa, pasipo Halali na kuliingiza nchi kwenye hasara ya kutumia fedha nyingi za kigeni kununua chakula na pembejeo .
Sasa hatuwezi kukaa kimya na kutohoji nchi inapita kwenye majanga ya kila aina na kila kona watu wanalalamika halafu tuone ni suala la kawaida tu . Hapana haiwezikuwa kawaida na lazima tuwe wakweli na wawazi kuwa tuna shida mahali na tuwe na majibu ya kuwapa wataanzania.
Hili suala la kuagiza mchele kutoka nje siyo la kubeza na ni suala linalotaka majibu na tafakari nzito sana.