Tanzania nchi yangu ninakulilia na nitakulilia mpaka pumzi yangu ya mwisho

Kamkunji

Member
Sep 14, 2023
92
274
Ndugu zangu salamu zangu ziwafikie popote pale mlipo kwenye sayari hii ya dunia, huku niliko namshukuru Mungu nimeshazoea, ahsanteni kwa maombi yenu.

Sijui ni mimi tu ama tupo wengi,
wakati ninakua, muda mwingi nilipenda kukaa na mzee wangu na wazee wengine wa pale mtaani huku wakibadilishana mawazo na kupiga stori zao za zamani na maisha yanavyobadilika kila uchwao, tabia hiyo ninayo mpakal leo kila nipatapo wasaa, hua nakaa na wastaafu kadhaa wananipa ABC za maisha na mtazamo wao kuhusu uelekeo wetu kama taifa.

Nakumbuka mwaka 2007, mzee wangu aliwahi kuniambia hii nchi inaonekana kama haina mwenyewe, kila apatae nafasi anajilimbikizia mali, na kusaini mavitu ya ajabu ajabu huko kwa nafasi yake, anakula percent, muda wake ukiisha anakaa pembeni anaanza kula kuku kwa mrija huku nchi ikibaki palepale ama kurudi nyuma kimaendeleo zaidi ya ilipokua
ni kwanini viongozi wengi wa nchi yangu hawaipendi nchi yao kutoka moyoni, wanaipenda kutoka mdomoni tu ili kupata kile wanachokihitaji.

Hivi ndugu yangu ushawahi fikiria hii nchi pamoja na kila kitu ilichonacho kuanzia mbuga, madini na rasilimali nyingine kibao ina uelekeo wowote kweli?

kila mtu akisema aisuse hii nchi na tusizungumze huko mbeleni kizazi chetu kitataabika sana, ni sawa uwe tajiri uzae mtoto aishi kwenye maisha ya kitajiri halafu ukifa arudi kua fukara wa kutupwa, maana yake misingi haikuwa mizuri.

hivi viongozi wetu mnadhani hizi mali tulizobarikiwa na Mwenyezi Mungu tunazokula na kutumia vibaya kama nchi hazitoisha..? kuna siku zaja hizi mali zitaisha na kizazi chetu kitataabika sana sababu ya tamaa zetu, mali binafsi haijawahi kutosha, tujifunze kuridhika kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

kuna wakati nafanya kazi nchi moja West Africa mzalishaji mkubwa wa dhahabu Africa, nchi ya Ghana, ilitangaza kufilisika huku ikimwachia malikia Elizabeth akijichotea tu na kutengeneza reserve kubwa ya dhahabu ambayo kila mtu alipoiona alishtuka, japo si kutoka Ghana tu, na ya kwetu lazima imo.

Yaani kuna wakati nikilala nakosa usingizi kabisa, ni kweli nina vingi vya kuwaza kama familia yangu, mke wangu na watoto lakini nikishamaliza kuwaza hivyo vitu vidogo hugeukia kuwaza vitu vikubwa ikiwemo uelekeo wa nchi yangu, hasa nchi watakayoishi hawa watoto wangu tuseme miaka 50 ijayo.

Hua najiuliza hivi kweli kuna siku nitakufa na kuacha nchi yangu hivi hivi ikiwa haina malengo ya kitaifa au hata kama yapo hayatekelezeki, ..? sasa nilikuja kufanya nn hapa?

Ni nani atakuja kuikomboa hii nchi ili isonge mbele hata kizazi kitakachokuja mbeleni kijivunie kuzaliwa kwenye nchi hii ya asali na maziwa?

kwann mifumo inaweka watu wenye akili halafu siasa inawaharibu na kua watu wa ajabu ajabu, kwani lazima wote tufe tukiwa matajiri wa kutisha?

Hii nchi haina mwenyewe kweli? kama wasemavyo, au wenye nayo ndio hao wenye tamaa za mali wasiotosheka.


Kwa nchi hii naapa hapa hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote wala lolote mbele ya kiongozi wa chama tawala, yaan hata watu wa Vetting wanafanya kazi under pressure ya chama, msione wanakosea kila siku, si wao, ni pressure za kazi, watu wote wa idara za ulinzi na usimamizi wa mali za umma wanafanya kazi chini ya pressure ya chama, na wengine wana hadi kadi za chama, ni nini hiki.

kwani wanasiasa wetu wapendwa hasa chama tawala mnaipeleka wapi hii nchi

Nalia mimi, nalia sana, sijui tufanyeje ndugu zangu, kweli tutaondoka duniani na kuiacha nchi yetu ikiwa hivi, maana hata ustawi wa familia zetu wakati mwingine utategemeana na ustawi wa nchi yetu pendwa, haijalishi tutaziacha na mali kiasi gani familia zetu
 
Kama mjukuu tu wa nyerere hajui inch inaenda wapi how me and you.........
 
Ndugu zangu salamu zangu ziwafikie popote pale mlipo kwenye sayari hii ya dunia, huku niliko namshukuru Mungu nimeshazoea, ahsanteni kwa maombi yenu

Sijui ni mimi tu ama tupo wengi,
wakati ninakua, muda mwingi nilipenda kukaa na mzee wangu na wazee wengine wa pale mtaani huku wakibadilishana mawazo na kupiga stori zao za zamani na maisha yanavyobadilika kila uchwao, tabia hiyo ninayo mpakal leo kila nipatapo wasaa, hua nakaa na wastaafu kadhaa wananipa ABC za maisha na mtazamo wao kuhusu uelekeo wetu kama taifa,

Nakumbuka mwaka 2007, mzee wangu aliwahi kuniambia hii nchi inaonekana kama haina mwenyewe, kila apatae nafasi anajilimbikizia mali, na kusaini mavitu ya ajabu ajabu huko kwa nafasi yake, anakula percent, muda wake ukiisha anakaa pembeni anaanza kula kuku kwa mrija huku nchi ikibaki palepale ama kurudi nyuma kimaendeleo zaidi ya ilipokua
ni kwanini viongozi wengi wa nchi yangu hawaipendi nchi yao kutoka moyoni, wanaipenda kutoka mdomoni tu ili kupata kile wanachokihitaji

Hivi ndugu yangu ushawahi fikiria hii nchi pamoja na kila kitu ilichonacho kuanzia mbuga, madini na rasilimali nyingine kibao ina uelekeo wowote kweli..?

kila mtu akisema aisuse hii nchi na tusizungumze huko mbeleni kizazi chetu kitataabika sana, ni sawa uwe tajiri uzae mtoto aishi kwenye maisha ya kitajiri halafu ukifa arudi kua fukara wa kutupwa, maana yake misingi haikuwa mizuri

hivi viongozi wetu mnadhani hizi mali tulizobarikiwa na Mwenyezi Mungu tunazokula na kutumia vibaya kama nchi hazitoisha..? kuna siku zaja hizi mali zitaisha na kizazi chetu kitataabika sana sababu ya tamaa zetu, mali binafsi haijawahi kutosha, tujifunze kuridhika kwa manufaa ya vizazi vijavyo

kuna wakati nafanya kazi nchi moja West Africa mzalishaji mkubwa wa dhahabu Africa, nchi ya Ghana, ilitangaza kufilisika huku ikimwachia malikia Elizabeth akijichotea tu na kutengeneza reserve kubwa ya dhahabu ambayo kila mtu alipoiona alishtuka, japo si kutoka Ghana tu, na ya kwetu lazima imo

Yaani kuna wakati nikilala nakosa usingizi kabisa, ni kweli nina vingi vya kuwaza kama familia yangu, mke wangu na watoto lakini nikishamaliza kuwaza hivyo vitu vidogo hugeukia kuwaza vitu vikubwa ikiwemo uelekeo wa nchi yangu, hasa nchi watakayoishi hawa watoto wangu tuseme miaka 50 ijayo

Hua najiuliza hivi kweli kuna siku nitakufa na kuacha nchi yangu hivi hivi ikiwa haina malengo ya kitaifa au hata kama yapo hayatekelezeki, ..? sasa nilikuja kufanya nn hapa..?

Ni nani atakuja kuikomboa hii nchi ili isonge mbele hata kizazi kitakachokuja mbeleni kijivunie kuzaliwa kwenye nchi hii ya asali na maziwa..?

kwann mifumo inaweka watu wenye akili halafu siasa inawaharibu na kua watu wa ajabu ajabu, kwani lazima wote tufe tukiwa matajiri wa kutisha..?

Hii nchi haina mwenyewe kweli...? kama wasemavyo, au wenye nayo ndio hao wenye tamaa za mali wasiotosheka

Kwa nchi hii naapa hapa hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote wala lolote mbele ya kiongozi wa chama tawala, yaan hata watu wa Vetting wanafanya kazi under pressure ya chama, msione wanakosea kila siku, si wao, ni pressure za kazi, watu wote wa idara za ulinzi na usimamizi wa mali za umma wanafanya kazi chini ya pressure ya chama, na wengine wana hadi kadi za chama, ni nini hiki

kwani wanasiasa wetu wapendwa hasa chama tawala mnaipeleka wapi hii nchi

Nalia mimi, nalia sana, sijui tufanyeje ndugu zangu, kweli tutaondoka duniani na kuiacha nchi yetu ikiwa hivi, maana hata ustawi wa familia zetu wakati mwingine utategemeana na ustawi wa nchi yetu pendwa, haijalishi tutaziacha na mali kiasi gani familia zetu
Usijekuta unalia kila siku lakini unawapa CCM kura kila mwaka.
 
Back
Top Bottom