Mwanangu Tanzania, Nchi ya AGANO, Usiogope

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,110
22,563
Salaam , Shalom!!

Angalizo: Jiepushe kuandika kejeli au upuuzi juu ya maneno ya unabii huu, maana maneno haya, yametoka katika kinywa Cha Mungu kupitia kinywa Cha Nabii wake, Ili kujiepusha na mapigo na LAANA.

UAMSHO UTAANZIA TANZANIA, AFRICA KWENDA DUNIA NZIMA.

Nitamimina uamsho wangu Kwa nchi zote ambazo hawaniamini Mimi Yesu, Nchi ambazo wanasema Eti sikufufuka, kwamba nilikufa kama WANADAMU wengine , nitajifunua kwao na nitatuma wahubiri wangu kupeleka INJILI yangu katika Nchi hizo, asema BWANA.

(Mathayo 24:14)
Tena habari njema ya ufalme, itahubiriwa katika Ulimwengu wote, kuwa ushuhuda Kwa mataifa yote, hapo ndipo Ule mwisho utakapofika.

Roho wangu atatumika tena kwenu Kwa kuwa, nimesikia vilio na kuomba kwenu, asema BWANA. Nitatimiza neno LANGU sawasawa na Neno langu KATIKA KITABU Cha
(Yoeli 2:28).

Hata itakuwa,baada ya hayo, ya kwamba, nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili, na Wana wenu waume Kwa wake, watatabiri, wazee wenu ,wataota ndoto na vijana wenu wataota maono.

TANZANIA NI NCHI YA AGANO.

Nimeweka AGANO nawe mwanangu Tanzania, utakuwa Nchi yangu itakayotumika kupeleka INJILI yangu duniani kote, INJILI ya nyakati za mwisho asema BWANA .

(Mathayo 24:14)
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika Ulimwengu wote, kuwa ushuhuda Kwa mataifa yote, hapo ndipo Ule mwisho utakapofika.

UAMSHO TANZANIA.

UAMSHO wangu hivi sasa, utakuja na utakatifu, zamani nilimimina uamsho wangu Kwa wote Ili nijulikane ULIMWENGUNI, lakini WANADAMU hawakuacha dhambi zao, uchawi uliingia Kanisani, Wachungaji ambao sikuwaita, walioingia Kanisani na kujiita Wachungaji,

Mimi Yesu ndiye Mchungaji wa Kweli, waliotangulia ambao sikuwaita, hao ni waongo, ni wale wasiohubiri maisha ya utakatifu Kwa watu wangu. ( Mathayo 24:24) watatokea makristo na manabii wa uongo.

Hasira yangu ikiwaka, msiizuie, upole wangu ukija, msiizuie.

DINI, NJIA, IMANI,KANISA MOJA TANZANIA
Nimeona bidii, nimeona unaonewa mwanangu Tanzania, nitaweka dini Moja, njia Moja ndani ya nchi yangu Tanzania. Nitawaondoa wote wanipingao, wategemeao majini, Mizimu,uchawi ,wao wajiitao kuwa ndio waabuduo halisi ilhali ni waongo, Mwanangu Tanzania Tegemeeni JINA LANGU pekee, YESU.

MATETEMEKO,MAFURIKO YAJA JUU YA NCHI
Mwanangu Tanzania usiogope, yanakuja Matetemeko na maji na mafuriko yaletwayo Kwa mkono wa yule mwovu sawasawa na ilivyotabiriwa katika
(Mathayo mtakatifu 24:7,9,).

7: Maana Taifa litaondoka kupigana na Taifa, na ufalme kupigana na ufalme, kutakuwa na njaa, MATETEMEKO ya nchi Mahali Mahali.

9: Wakati huo watawasaliti ninyi mpate DHIKI, nao watawaua, nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote Kwa ajili yangu.

Nitakusambaza mwanangu Tanzania katika Nchi mbalimbali, nitaweka AGANO na wewe,

Nimeona bidii, nimeona pia unaonewa Tanzania, lakini usiogope, Mimi ni BWANA, Nitakuokoa, maana nimekuchagua.

Amani iwe nawe mwanangu Tanzania, maji na mafuriko, na Matetemeko yanakufuatilia, Yana mwisho wake, na mwisho wake ni Mimi BWANA, USIOGOPE!!

USIOGOPE, USIOGOPE MWANANGU TANZANIA.

Ikiwa hujaokoka fuatisha Sala hii;
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO. AMEN

Amen.

Source. Mtume Meshack.
 
Back
Top Bottom