Kama kijana nayeipenda nchi yangu, nayependa amani, demokrasia na maendeleo nafanyaje?
Nafanyaje Askari wanaposherehekea ushindi wa dhulma wa chama tawala kwa kuimba 'soldier nyakua'?
Nafanyaje mheshimiwa rais anapotoa ilani ya kumshughulikia Mkurugenzi atakayemtangaza mpinzani kuwa mshindi kwenye uchaguzi?
Nafanyaje napoona viongozi wangu wa chama, wapenda demokrasia na amani, wakidhalilishwa na polisi kila leo,wakinyang'anywa Mali zao kwa nguvu, wakilazimika kuzunguka mahakamani kila uchao na wakidhalilishwa wao na familia zao?
Nafanyaje napoona vijana wenzangu wa Rika wakishawishiwa na kushawishika kwamba demokrasia haina nafasi Bali siasa za visasi, hujuma na matumizi ya nguvu ya dola ndio mtindo wa kileo?
Nitaendeleaje kuamini katika uchaguzi huru na wa haki wakati tume yenyewe ya uchaguzi haiamini Wala vyombo vya dola haviamini?
Kwanini wakati wa apartheid vijana wa Afrika kusini walikuja kujifunza hapa mbinu za uasi?
Kwanini hawakuitisha tu mikutano ya siasa nchini kwao na kwenda kupiga kura?
When democracy has no chance, it is the responsibility of everyone and anyone to give it a chance!
SOLDIER NYAKUA, NYAKUA!
Kimsingi tumechelewa sana, yaliyotokea monduli juzi yalishawahi kutokea wakati fulani na Nassary alipigwa vibaya wakati huo lowasa ndo sterling wa ccm monduli.
Kimsingi lowasa anaijua vizuri siasa na wapiga kura wa Tz, alifahamu fika kuwa ccm itachukua nchi kwa gharama yoyote ile na yeye akibaki ccm ndo mwisho wake kisiasa, solution, hamia cdm gombea urasi na status yake kwenye national politics itabaki kuwa juu na amefanikiwa sana.
Cdm wanaelewa sana ugumu wa kuitoa ccm madarakani kwa karatasi ya kura, so yoyote anakuja kwao hata km ni mbaya kiasi gani, ukweli ni kwamba hakuna ubaya wa mtu utakaoweza kuizidi ule wa ccm na mfumo wake, hivyo pokea wote including lowasa na sumaye aliyewahi kusema 'ukitaka mambo yako yaende vizuri ingia ccm'.
Hapa sina lengo la kuwalaumu cdm wala kina lowasa na wenzake bali ni kujaribu kuonesha ni kwa kiasi gani tumechelewa sana kudai true democracy kwa njia yoyote ile. Mifano ni mingi sana kuelewa kuwa uhuru wa 1961 niwakubadili tu utawala ila mifumo ya ukoloni bado inatutawala kupitia watu weusi.
Kwa urahisi kuwa ccm haiwezi kutoka madarakani kwa kura hata km uchumi ufe kiasi gani angalia Zimbabwe pale ambapo jina ccm bado haijachokwa na siku ikichokwa angalia yaliyotokea Kenya. Kabla kanu haijafa, iliua upinzani wa kweli ikatengeneza kwa kwake chini ya kibaki ambaye miaka yote toka uhuru amekuwa kanu km waziri na makamu wa raisi. Sasa yupo kenyata ambaye 2002 alikuwa mgombea uraisi wa kanu, 2008-2013 waziri wa fedha chini ya kibaki na 2013-leo ni raisi, jiulize ni lini kanu ilikufa?
Mwisho, ccm haiwezi kuachia madaraka kwa njia ya kawaida ya karatasi ya kura kwa sababu kuu tatu; #1. Ujinga na umaskini bado ni mkubwa sana, yaani bado wapo wengi tu wanaoipa kura, #2. Mfumo wa uchaguzi haiko huru na kamwe hawatauweka huru kwa kuombwa, #3. Bado mfumo wa utawala unaendelea kujali interests za wakubwa duniani.
Mwisho kabisa, exception, #1. inawezekana ccm kuondoka pale ambapo tutapa mgombea uraisi ambaye ataungwa mkono na idadi ya kutosha, at least 75% ya wapiga kura wote nchi nzima ktk nafasi zote yaani udiwani, ubunge na uraisi, #2. Siku wakiaamya kuvunja mfumo unalinda interests za wakubwa duniani.
Kwa mapni yangu, hii exception #1 tuipatie nafasi 2020 kupitia Tundu Lissu, alishawahi kuifuta ccm jimbo kwake, anaweza kuifuta Tz.