Jita
Kama kijana nayeipenda nchi yangu, nayependa amani, demokrasia na maendeleo nafanyaje?
Nafanyaje Askari wanaposherehekea ushindi wa dhulma wa chama tawala kwa kuimba 'soldier nyakua'?
Nafanyaje mheshimiwa rais anapotoa ilani ya kumshughulikia Mkurugenzi atakayemtangaza mpinzani kuwa mshindi kwenye uchaguzi?
Nafanyaje napoona viongozi wangu wa chama, wapenda demokrasia na amani, wakidhalilishwa na polisi kila leo,wakinyang'anywa Mali zao kwa nguvu, wakilazimika kuzunguka mahakamani kila uchao na wakidhalilishwa wao na familia zao?
Nafanyaje napoona vijana wenzangu wa Rika wakishawishiwa na kushawishika kwamba demokrasia haina nafasi Bali siasa za visasi, hujuma na matumizi ya nguvu ya dola ndio mtindo wa kileo?
Nitaendeleaje kuamini katika uchaguzi huru na wa haki wakati tume yenyewe ya uchaguzi haiamini Wala vyombo vya dola haviamini?
Kwanini wakati wa apartheid vijana wa Afrika kusini walikuja kujifunza hapa mbinu za uasi?
Kwanini hawakuitisha tu mikutano ya siasa nchini kwao na kwenda kupiga kura?
When democracy has no chance, it is the responsibility of everyone and anyone to give it a chance!
SOLDIER NYAKUA, NYAKUA!
Jitaidi usiwe unafikiria vitu juu juu tu, Ni mahangaiko,utapoteza ndugu zako, usije ukashangaa hauna ndugu,utapoteza kila kitu na usishangae hata wewe ukapotea, bora vita vya nnchi na nnchi kuliko vita vya wenyewe kwa wenyewe,Siku nyingine ukiwa unareta Uzi kama huyu jipange kuleta sio,kuongozwa na mihemko na fikra bila kufikiria na kibaya zaidi Vitu vingine I mean wapinzani juu ya ccm sio kwamba mda Mwingine na wenyewe hawakosei hukosea ila wakitretiwa inaonekana wanaonewa msiwe wepesi kukubali taarifa wapinzani wanazotoa bila kufatilia kwa kina sana kujua ukweli Ndo sasa conferm,ila mnaletewa taarifa watu wanapanic hooo tumeonewa Habari za kusikia Watanzanua wenzangu sio nzuri fatilia au shuhudia ndo uone kama kuna kuonewa au la! ! !,kuona kuwa kila kosa eti wanaonewa kuna mda kweli wanakosea na lazima watritiwe tu wajivunze, ,wakitreatiwa eti wanaonewa sasa kama mtu kavunja sheria aachwe? Wakimsolve kaonewa wakimuacha wameogopa lazima wamsolve tu
Mimi sina chama huwa napenda kiongozi aliye bora haijalishi ni cuf,cdm,au ccm au chama chochote kikubwa anafanya kazi huyo namkubali
Kuna Siku Mbunge wa ccm ni kama Dada yetu tu,alikuja kuna kitu tulikuwa tunaongea nae akasema hivi kwenye inshu za Maendeleo mfano Serikari imefanikiwa kufanya moja mbili tatu itasema hayo Mafanikio Bungeni
Sasa cha ajabu,kila wabunge kulingana na kambi zao za chama huwa wana mikutano yao binafs au ya siri ya wabunge hao wa chama husika, sasa utashangaa Hao wapinzani Wabunge wanelewana waeke msimamo kupinga tu mradi Fulani wa Maendeleo kwa sababu zao binafsi ili tu kwamba kuitetelesha serikari kwa ajili ya Mafanikio yake ionekane haijafanya kitu,ngoja nitoe mfano swala la kuja kwa ndege kuna Siku mbunge tena mtu mzimaaa kabisa anasimama kwa hoja isiyo ya msing anapinga ujio wa ndege,wengine wanasema ndege iuzwe walete madawa,Wakati bajetinya Madawa ipo na ishaandaliwa. wengine wanasema watu wa vijijini hawanufaiki kwa ndege wanalalamika,haujui,kuwa hizi ndege zikipiga pesa kupitia kusafirisha Abiria,pesa iliyopatikana zitarudi kuwasaidia watanzania,kununua madawa,na kuinua miradi mingine na tena ndege zimefufua shirika la ndege na rada zinazidi kujengwa ili tusitegemee zile rada za kenya ambazo tulikuwa tunalipia gharama kubwa kwa Mwaka mabilioni ya pesa,Sasa Mbunge anasimama kupinga Ndege na wanannchi wenye mawazo mafupi wanamkubali ndio ni sawa eti hizi ndege kwa wanaoishi vijijini hawanufaiki
kwa kweli Ushauri tu,Watanzania umefika Wakati tusiendeshwe na Kila jambo hata la Maendeleo tunaweka siasa nakwambia hatutafika,watu wakisikia Fulani kaongea wa chama Fulani wanamkubali kama mungu wao,judge kwanza anachoongea halafu ndo uchukue hatua sio kila jambo analosema linajenga au nikweli, mengine anafanya tu kuchafua utawala kwa sababu anajua ameteka akili za wengi kwa kuwa na Maneno Mengi na hafuraii innchi kuendelea anapambana kisa vyama aonekane anaongea watu wajue kumbe na huyu yupo kwa kweli tusikubali kila kila lisemwalo na Hao wenye maneno mengi ni mawazo yangu hayo
Wana maneno mengi kuonekana na kutafuta waonekane kwenye mitandao wajulikane wapo nadhani mnawajua hapo gani wao mda wote ni siasa tu kazi hawafanyi