CHADEMA yamuonya Nape kwa kauli yake kuwa CCM itaongoza nchi hata kama ni kwa kura za wizi

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa BAVICHA, Julius Mwita, amelaani na kumuonya vikali Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, kwamba achunge ulimi wake.

Kiongozi huyo wa Bavicha ametoa kauli hiyo kufuatia kauli ya Nape hapo juzi akihutubia mjini Chato, Geita. kwamba CCM itaendelea kutawala hata kama ni kwa kuiba kura.

Kauli hiyo ya Nape iliwashangaza wananchi wengi na kusema kiongozi huyo ameamua kusema ya moyoni kutokana na chama hicho kuchukiwa na wananchi wengi kwa sasa.

Katibu Mkuu huyo wa Bavicha amesema mwaka huu hakuna hata kura moja itakayoibiwa, na CCM ijiandae kukabidhi madaraka kwa UKAWA kwa amani.

Kauli ya Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye, kudai chama chake kitaendela kuongoza nchi hata kama ni kwa kura za wizi, chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibuka na kumjibu kuwa hizo ni ndoto za mchana.

Akizungumza na NIPASHE kwenye ofisi za Chadema Wilaya ya Chato, Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (Bavicha), Julius Mwita, alisema chama chake kipo kwenye maandalizi kamili ya kuingia Ikulu na kwamba mbinu za CCM kuendelea kuiba kura mwisho wake umefika.

Alisema kila mbinu chafu za CCM zilizoandaliwa kuhujumu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu zimeshabainika ikiwamo kuagiza magari 700 ya kutawanya wananchi kwa maji ya kuwasha, badala ya kujikita kubuni mbinu bora za kudhibiti mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe wanaouawa bila hatia.

"Nikuhakikishie kuwa mwaka huu Chadema kupitia Ukawa tunaingia madarakani...hivi sasa CCM wanaweweseka tu wasijue la kufanya ndiyo maana wamekuwa na foleni kubwa ya wagombea urais kana kwamba ni taasisi ya kuchezewa hadi na wasomi wa darasa la saba," alisema.

Alisema tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu imejionyesha kwenye uchaguzi mdogo uliomalizika ambapo Ukawa ulikishusha CCM katika viwango vya ushindi kutoka aslimia 95 hadi kufikia asilimia 64 na kwamba hatua hiyo ni wazi kwamba Ukawa wanakwenda kuchukua dola.

Akizungumza hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara wilayani Chato mkoani Geita, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdurahman Kinana, aliwataka wafuasi wa chama hicho kuikosoa serikali ya CCM inapofanya mambo yasiyopaswa na ikiwezekana wafanye maandamano kupinga badala ya kusifia kila kitu.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida Nnauye, alisisitiza kuwa CCM kitaendelea kuongoza nchi kwa kuwa ni chama makini na kwamba hata kama itakuwa kwa kura za kuiba na kudai kuwa bao ni bao hata kama ni la kidole iwapo kama mwamuzi hataweza kuona.

Kauli ya Nape ilipokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo huku wakidai ameamua kutoa siri inayowafanya CCM kupata ushindi katika chaguzi zilizopita huku wengine wakisifia kuwa ni wakongwe wa siasa na kwamba mbinu zote za ushindi wanazo.

Chanzo: Nipashe

Hata hii hujaona au umelewa ushabiki tu ''View attachment 262744
 
Kauli ya Nape ni kauli ya hatari mno! Sijui hata kama anafahamu uzito wa kauli hiyo.
 
Acha uongo wewe. Wapi Nape kazungumza kuwa CCM itashinda hata kwa kuiba kura?CCM inapenda zaidi nchini na haihitaji ramli kujua hilo.
 
Nape amelewa sana madaraka, yaani anautangazia umma kuwa wapo madarakani kwa wizi wa kura!!!
 
Bavicha baada ya kuona saccos yenu ya wachaga inakufa mnaanza propaganda za uongo kama babu yenu anayeiba wake za watu,wekeni ushahid hapa
 
Acha uongo wewe. Wapi Nape kazungumza kuwa CCM itashinda hata kwa kuiba kura?CCM inapenda zaidi nchini na haihitaji ramli kujua hilo.

Sijui shule na sayansi ya utawala kama unaijua
Ccm siku zote imekuwa ikisema" chama dola na udhindi ni lazima kwa kuwa"

Usalama wa Taifa ni ccm,
Polisi ni ccm,
Jeshi la wananchi ni ccm,

Kupitia hawa,watapiga mabomu,watateka masanduku,wakipinga waagiza polisi wawapige kuua na vyovyote vile

Bvr tu mnatumia viongozi wa ccm bila udara ya uhamiaji kusema hawa sii raia mulikuwa wapi kabla?
 
CCM imshukuru sana sana Kinana although nafahamu anavumilia mengi lakini hawa vijana wa JK wangekizamisha chama chetu kabisa!/
Hawafai hawafai hawafai zidini kuwakumbatia!
 
ULAYA huyu angetakiwa kujieleza na angefurushwa ktk nafasi yake.
Siyo tu angestahili kufurushwa, bali angestahili kuwa kizuizini akisubiri kufunguliwa mashtaka ya uhaini ya kutaka kuleta machafuko nchini.

Lakini cha ajabu mamlaka za nchi yetu zitamtazama tu wakiiona hiyo kauli ni ya kawaida sana.

Hata hivyo kutokana na kufunguka huko kwa Nape, wananchi tumepata ushahidi usio na shaka yoyote kuwa kumbe ule ushindi wa kishindo ambao CCM wamekuwa wakitamba nao, tokea mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi uanze upya mwaka 1995, kumbe chama hicho kimekuwa kikifanya wizi wa kura ikishirikiana na Tume ya uchaguzi ambayo haiko huru!
 
Sasa Nyie Mnaokanusha Ni Akina Nape? Nape Kama Hakusema Aje Hapa Akanushe Alafu Watu Wafunguke Maana Alishalekodiwa,
 
Sijui shule na sayansi ya utawala kama unaijua
Ccm siku zote imekuwa ikisema" chama dola na udhindi ni lazima kwa kuwa"

Usalama wa Taifa ni ccm,
Polisi ni ccm,
Jeshi la wananchi ni ccm,

Kupitia hawa,watapiga mabomu,watateka masanduku,wakipinga waagiza polisi wawapige kuua na vyovyote vile

Bvr tu mnatumia viongozi wa ccm bila udara ya uhamiaji kusema hawa sii raia mulikuwa wapi kabla?

BAVICHA sasa wanapepesuka na wameanza kuongea ovyo ovyo! Teh teh wakiambiwa waweke ushahidi unaruka teh teh hao ndo cdm kwa sound!
 
Siyo tu angestahili kufurushwa, bali angestahili kuwa kizuizini akisubiri kufunguliwa mashtaka ya uhaini ya kutaka kuleta machafuko nchini.

Lakini cha ajabu mamlaka za nchi yetu zitamtazama tu wakiiona hiyo kauli ni ya kawaida sana.

Hata hivyo kutokana na kufunguka huko kwa Nape, wananchi tumepata ushahidi usio na shaka yoyote kuwa kumbe ule ushindi wa kishindo ambao CCM wamekuwa wakitamba nao, tokea mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi uanze upya mwaka 1995, kumbe chama hicho kimekuwa kikifanya wizi wa kura ikishirikiana na Tume ya uchaguzi ambayo haiko huru!

Wekeni ushahidi hapa wa sound clip na sceen short ya story ya gazeti mbona mnayumbayumba!
 
Nape anajindanganya,mkiiba kura mimi niko tayari kuanza kwa kumuuwa mama yangu ambaye ni ccm,kisha nitatoka nje.................hakika msidharau kauli ya nape ndiye msemaji wa ccm.
 
Back
Top Bottom