Nawaunga Mkono Madaktari

Mkuu wangu nakubaliana sana na wewe toka mwanzo isipokuwa nilichoitaka kusema ni kwamba ulijaribu kutolisema wazi kwamba mbegu ya matatizo yetu ni AFYA kuwa biashara.

Na hapana sii kweli kwamba AFYA kuwa biashara ni sera ya Kihafidhina sii kweli kabisa isipokuwa Uhafidhina unamlinda mwananchi na biashara inabakia mikononi mwa wananchi. Sio lazima Afya iwe biashara hata kidogo usitumie Uhafidhina wa Marekani maana mazingira tofauti. Canada, japan na nchi kibao AFYA ni bure na wahafidhina wapo isipokuwa matumizi yasiyokuwa na sabau ndio hatutaki. Marekani wanazo Hospital za bure lakini ia zipo Private tunachokataa wahafidhina ni kuona huduma hizi zinafanywa na serikali tu na kumfunga mwananchi ktk maamuzi ya afya yake.

Tatizo la Tanzania ni pale tulipoifanya AFYA kuwa biashara wakati huo huo serikali inaingiza mafedha kibao ktk subsidies ambazo hazitoi nafuu kwa mwananchi. Hivyo mimi kama Mhafidhina napinga matumizi mabaya ya fedha zetu na hivyo kutaka ruzuku zote zikatwe na tuunde mfumo mpya ambao Hospital binafsi zitapewa ruzuku tu ikiwa watatoa huduma hizo bure au karibu na bure laa sivyo wajitegemee na tutawajengea sera za kuwawezesha kuendesha biashara zao.

Serikali itaendelea kutoa huduma bure za Afya kulingana na mazingira yetu maana tuliupata Uhuru wetu kwa kupigania mambo haya. Na lazima tuya enzi ndio Uhafidhana wenyewe..

Hivyo kuna mambo mengi sana watu huchanganya baina ya UBEPARI na UHAFIDHINA ingawa kweli Uhafidhina unatetea zaidi kuboresha miundombinu inayozalisha kazi hivyo kuwapa nafuu wawekezaji wa ndani na sio Nje maana Uhafidhina tunapinga sana wageni.. Utajirisho wa wananchi ndio huzaa ajira na ajira ndio huboresha maisha ya wananchi na sio kutoka chini kwenda juu. Ukimwezesha mtu kujenga kiwanda kwa kodi nafuu unamhamasisha kujikuza na kutoa ajira zaidi hivyo ujenzi unaanza ktk uwekezaji.

Hakuna mahala popote panaposema Uhafidhina unapinga elimu na Afya bure kwa wananchi wake isipokuwa unatazama kwanza biashara inaweza vipi kuleta maendeleo dhidi ya serikali kujihusisha. Hivyo Mhafidhina yeyote hapa Canada ukimwambia US wanalipia Afya na shule tunacheka sana! kwa sababu kodi ya mwananchi inatumika pale inapohitajika zaidi na maswala yote ya biashara unawaachia wananchi serikali haiweki mguu isipokuwa kujenga policies zinazowawezesha hawa wawekezaji kukua kibiashara bila kuumiza wananchi.

Pili, swala la kutojua kama serikali imefilisika.
Mkuu wangu sina maana ya wewe isipokuwa hoja nzima mnashindwa kuelewa kwamba hapa tulipofikia serikali yetu IMEFILISIKA!...Ukweli ndio huo, serikali inatumia mabillioni ya fedha zake ktk vitu ambavyo havina mpango na matokeo yake tunakwama hapa tulipokwama isipokuwa wengi hawafahamu na nikadhani na wewe pia hufahamu hilo.

Sasa wewe nambie Madaktari wanagoma kwa sababu ya posho lakini wameweka na ati vifaa vya kutendea kazi havitoshi...hii kweli inaingia akilini?.. Miaka yote ya Udaktari wao wamefanya kazi hii ktk mazingira magumu zaidi enzi za mwalimu leo hii ubora wa Hospital wakati wewe mwajiriwa inakuwa sababu ya mgomo wako?. Sababu zote walizotoa hazina maana zaidi ya madai ya posho kwa sababu tu Pinda kapitisha ongezeko la posho za wabunge..peroid!.. Ni ujinga toka kwa serikali na ujinga toka kwa Madaktari maana wanatuumiza sisi wananchi.

Kweli serikali imefilisika na sii uongo na sababu kubwa ni hizi posho na matumizi yasiyokuwa ya msingi. Tunatumia fedha nyingi sana ktk recurrent expenditures badala ya kuboresha huduma zenyewe. Wabunge wana vikao mia kwa mwaka wote wakichota ruzuku lakini ufanisi ktk kazi hakuna. na kila tunapojiuliza kwa nini tumeshindwa zinaundwa tume nyingine kuchunguza na kuchukua posho zaidi. Sasa hivi ktk kufikiria Tanzania yenye mabadiliko wanaunda tume kuunda dira ya nchi wakati Katiba haijafikia muafaka.. Haya yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi na Ufafidhina tunajali sana kodi za wananchi zinatumika vipi.
 
Kwani wlaipojenga Hospitali hizi walitegemea ruzuku za serikali? mbona zilikuwa zikitoa huduma hata kabla.. mimi sielewi unakotaka kwenda haswa.. Nachosema maadam ni Hospital private serikali haitakiwi kuweka mguu wake. Wizara ya Afya inatakiwa kuwa na idara zake na CSSC haitakiwi kuwa moja ya idara hizo. kabish

Huu ni mtazamo wangu unaweza kutokubaliana lakini binafsi sikubaliani na sera za CCM wala CDM zinapohusisha kanisa ktk maswala ya kiutawala ktk wizara zake. Nimejieleza vya kutosha subsidies zinaweza kutoka tu pale chombo kinachotoa huduma kitawapa wananchi nafuu kubwa ya gharama lakini haya ya kumwona daktari kwa Tsh 50,000 wakati wamepewa ruzuku ni wizi sitojali nani anafanya hivo..Na madaktari leo ni mashahidi kuwa hata hizo huduma zeneywe ni mbaya kutokana na uwekezaji mbaya.. I think it's about time tuwawajibishe wahusika na kutambua kwamba mfumo huu haufai na umeharibu kabisa huduma za Afya nchini... Nimemaliza ukitaka nisome hutaki niache na mtazamo wangu...
- Sikubaliani na hotuba ya Dr.Slaa Kilombero!...
 
Mimi ni mmoja ya watu nisiyeunga mkono MGOMO wa madaktari.
Nakubaliana kwamba madai yao ni ya msingi sana na serikali ndio kiini cha yote na inatakiwa iyashughulie haraka sana. watu wamekuwa wanaunga mkono kwa ushabiki tu na sio kwa kuangalia uhalisia na uzito wa jambo, hv utajisikia mama yako au baba yako akifa kisa mgomo wa madaktari?

ushauri wangu:
Km kweli sisi wananchi tunaumizwa na madai ya madaktari inatakiwa sisi ambao ni wazima tufanye maandamano nchi nzima kushinikiza serikali iwatatulie madai yao huku wao wakiwa wanaendelea na matibabu. lakini swala la kukaa na kutafuta nani mwenye makosa au wa kumkomoa kati ya serikali na madaktari tujue tunachekelea vifo vya wajawazito, vikongwe, wagonjwa wa moyo etc. Tuache ubinafsi na ushabiki usio na maana juu ya swala muhimu la afya zetu. sidhani km muda huu ukipata ajali mbaya na ukapelekwa ICU utaendelea kuchekelea mgomo wa madaktari. wengi mnachekelea kwa kuwa ni wazima wa afya.\

nawasilisha
 
Kalumekenge alikataa kwenda shule
baba yake akiambia fimbo imchampe
fimbo ikakataa
akuambia moto uichome fimbo
moto ukakataa
akayaambia maji yauzime moto
maji yakakataa
akamwambia mbuzi ayanywe maji
mbuzi akakubali
kimbembe kikaanza
maji yakakubali kuuzima moto
moto ukakubali kuichoma fimbo
fimbo ikakubali kumchapa kalumekenge
kalumekenge kwa kuogopa kuchapwa akaenda shule
sasa swali
kati ya serikali na madaktari ni nani anamwakilisha kalumekenge?
 
Mkuu you are very wrong. It has just occurred that we have hospitals built and run by religious organizations. The fact that these have played a fundamental role in giving health services to people Particularly in rural areas, it was inevitable and wise to argument the efforts rather than replicating. Fika Litembo,usokami, Ikonda,Ipamba to name just a few and you might have a change in your stance.
 
Ikiwa serikali inatoa billioni 90 kila mwaka kwa kanisa mlitegemea itapata fedha wapi zaidi za kuboresha Hospital zake..


Jokes aside, Mkandara unaamini kwa dhati sababu kubwa inayofanya wakubwa wapelekwe India kwa matibabu ni kwa sababu inatoa ruzuku kwa hospitali zinazoendeshwa na kanisa? Hebu angalia hiyo list ya madai ya madaktari kwa makini tena. Halafu unganisha na EPA, meremeta, na majinamizi mengine yanayofanana na hayo.
 

Mkuu,

Nimefurahi sana kutambua rasmi kwamba Mkandara ni Mhafidhiana. Hili litatusaidia sana kubadilishana mawazo humu ki-tikadi. Nadhani unakubaliana na mimi kwamba Siasa za vyama vyetu Tanzania – CCM, Chadema, CUF, etc, haziendeshwi kwa itikadi. Lakini tuliache hilo kwa sasa.

Kwanza kuanzia, nakubaliana na wewe kwamba Uhafidhiana na ubepari ni vitu viwili tofauti, ingawa wengi hawalifahamu hilo. Lakini muhimu lingine ni kwamba, ubepari na soko huria ni vitu vyenye uhusiano tu, lakini havifanani, kwani Soko lipo katika mifumo mingine yoyote, kinachobadilika chini ya mfumo wa ubepari ni kwamba tu, soko sasa linakuwa la ‘huria'.

Lakini kabla sijaenda mbali, naomba kujitambulisha rasmi leo kwako kama Mjamaa wa Kidemokaria (a Social Democrat). Kwa maana hii, wakati wewe ni muumini wa mrengo wa kulia, mimi ni muumini wa mrengo wa ‘kushoto-kati', kwa kuendana na mpangilio wa itikadi hapa chini, ambapo eneo la KATI ni lile kati ya Uliberali na Ujamaa wa Kidemokrasia likiwa ndio mrengo wa kati, ambayo pia ndio itikadi ya Chadema.

Ukomunisti>Ujamaa=>Ujamaa-wa-Kidemokrasia=Uliberali=>Conservative Liberals=>Uhafidhiana

Sisi na nyinyi tuna tofauti nyingi za msingi, lakini muhimu zaidi ni kwamba pia tuna mambo mengi ya msingi tunayofafana. Naomba unielewe naposema SISI sina maana ya CCM,kwani CCM haina dira. Nikisema sisi maana yangu sisi waumini wa itikadi ya ujamaa wa kidemokrasia, itikadi ambayo bado hakuna hata chama kimoja Afrika inaifuata.

Nianze na tofauti kati ya sisi wajamaa wa kidemokrasia na nyinyi wahafidhiana: Sisi na nyie tunatofautiana juu ya kiwango cha ushiriki wa serikali katika umma na uchumi, kupitia aidha huduma za kijamii kama vile afya elimu, n,k, au mashirika ya umma, katika shughuli za utoaji wa huduma na na uzalishaji. Nyinyi mnahimiza sekta binafsi kuwa mstari wa mbele zaidi, na ikiwezekana, serikali kutojiingiza kabisa. Ni wenzenu chini ya itikadi ya "Conservative Liberals", ndio wana ka-uvumilivu kidogo na serikali katika masuala haya, Sio nyinyi. Lakini pamoja na tofauti hizi, sisi na nyinyi tunafana katika kitu kimoja cha msingi sana: Sote tunaamini juu ya umuhimu wa kuwepo kwa mfumo wa kibepari, na tunapinga itikadi za kijamaa na kikomunisti ambazo lengo lake kuu ni kuusambaratisha na kuutokokomeza mfumo wa kibepari katika jamii.

Suala la muhimu sana kusisitiza hapa ni kwamba, sisi "Wajamaa wa Kidemokrasia", tunaamini umuhimu wa Ubepari, ili mradi tunapewa uwezo wa kuukemea pale unapoenda mrama - hasa pale ubepari unapoumiza watu wa hali ya chini. Iwapo tunapata nafasi ya kuunda serikali, ni muhimu kwetu sisi ubepari utuvumilie, kwani ili kuepusha chuki kama zile za kikomunisti au Kijamaa dhidi ya ubepari, sisi hatuna tatizo na uwepo wake ilimradi serikali yetu inapata nafasi ya kuweka muundo thabiti wa kugawanya utajiri wa taifa, mfano kupitia kodi za aina mbali mbali, lakini pia uwepo wa huduma za kijamii – afya, elimu, makazi n.k, kwa wananchi wote wasiojiweza. Hilo likishindikana, sisi na ubepari hatuwezi kukaa meza moja kwani tuta twangana ngumi.

Sasa tuje kwenye hoja yako nyingine, pale unaposema:

Hakuna mahala popote panaposema Uhafidhina unapinga elimu na Afya bure kwa wananchi wake isipokuwa unatazama kwanza biashara inaweza vipi kuleta maendeleo dhidi ya serikali kujihusisha
.

Itikadi nyingi za kushoto, ikiwa pamoja na yetu ya Ujamaa wa Kidemokrasia zinakerwa na sera zenu nyingi ambazo kwa kweli hazijali watu maskini katika jamii. Sera zenu nyingi zinachangia sana kuongezeka kwa pengo kati ya watu wa kipato cha juu na kipato cha chini. Lakini hamkosi kuja na hoja kukinga msimamo wenu. Mnadai kwamba – pengo kati ya watu wa juu na wa chini ni kichocheo muhimu kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuongeza ubunifu ili na wao wafanikiwe katika maisha. Na ndio maana, in the same vein, mnaamini kwamba huduma za bure za serikali zinajenga muundo unaolea wavivu, ambao wanaishi kwa kutegemea government handouts. Ni kwa sababu hizi, nyinyi huwa hamkubaliani na huduma bure za afya, elimu, n.k, kwa umma.

Kuna hoja yako nyingine unasema kwamba:

Marekani wanazo Hospital za bure lakini ia zipo Private tunachokataa wahafidhina ni kuona huduma hizi zinafanywa na serikali tu na kumfunga mwananchi ktk maamuzi ya afya yake.

Hoja hii ni ya kawaida sana miongoni mwenu, na inasisitiza kwamba ni muhimu kwa serikali kuwaachia wananchi wachague/wawe na choice, sio kuwafunga wategemee huduma za serikali pekee. Suala hili kwa kiasi fulani nakubaliana nalo, kwani ushindani ndio msingi wa ufanisi. Lakini kwa kiasi fulani nina reservation juu ya suala hili katika mazingira yetu ya Tanzania.

Naomba nikuulize:

Je kwa Mtazamo wako, katika mazingira ya Tanzania ambako tuna hospitali nyingi tu za binafsi, mfano kwa Dar-es-salaam zipo Agha Khan, Hindu Mandal, TMJ, Trauma Center, Regency n.k, kwanini hatuoni wakazi wengi wa Dar-es-salaam wakifurika kwenye hospitali hizi, na badala yake wanafurika kwenye hospitali za Mwananyamala, Ilala (Amana)na Temeke, kiasi cha kulala hata sakafuni wakati kuna vitanda wazi vingi tu Agha Khan, Hindu Mandal, TMJ, Trauma Center, Regency?

Unapendekeza suala la mfuko maalum wa ruzuku ambapo hospitali binafsi ambazo zitaweza kutoa huduma kwa gharama karibia na bure, kama sio bure, zitapewa fedha kutoka katika mfuko huu. Hili ni wazo zuri sana. Lakini je, hauoni kama hapo ni mgongano wa ki-itikadi? Iwapo unagombea uongozi, kwa msimamo huo, wahafidhiana hawatakupa kura, kwani, suala la mfuko wa ruzuku ya afya maana yake ni Serikali kuendelea kuwepo katika sekta hii, kwani hizi bado ni fedha za walipa kodi. Vinginevyo, tafisri yangu kuhusu hoja yako ya mfuko wa ruzuku ya afya ni kwamba, ni muhimu kwa serikali kuendelea kushiriki kutoa huduma za afya, lakini njia ya ruzuku ya afya, ndio njia ya ufanisi zaidi, kwani njia hii itaipunguzia serikali mzigo (walipa kodi), tofauti na mfumo wa sasa wa serikali kutoa huduma za afya moja kwa moja, ambao unaendeshwa kwa ufanisi wa hali ya chini sana. Nakubaliana na wewe katika hili.

Vinginevyo nakubaliana na wewe kwamba matumizi ya ovyo ya serikali ya sasa, katika vitu visivyokuwa na maana yamechangia sana nchi kufilisika, hivyo kuathiri shughuli nyingi sana za kiuchumi na kijamii zilizokuwa chini ya serikali.
 
Bado sijajuwa vizuri mafundisho ya uislamu yamebeba nini ndani yake, maana kila sehemu ni ulalamishi wa Waislamu kuona kwamba wakristo wanapendelewa, ni hatari zaidi kukuta muislamu ambaye ameelimika kuona anashabikia upuuzi huu.
 
Nawaunga mkono madaktari hivi wanasiasa maarufu wako upande gani?
 
Utajisikiaje kama mama yako au baba yako atakufa kwa kupatiwa huduma mbaya na daktari ambaye amechoka na anayefikiria biashara zake badala ya wagonjwa?
 
Nawaunga mkono madaktari hivi wanasiasa maarufu wako upande gani?
Nadhani ni busara zaidi kwa wanasiasa kukaa pembeni ili kuondowa zile propaganda kwamba wanachochewa na Chadema, ningependa zaidi kuona asasi za kiraia zikishikana bega kwa bega na madaktari, hata hawa wanaoitwa MEWATA sijasikia wakiongea lolote.
 

kwa saabbu babako mama yako house girl/boy wanauwezo wa kufia appolo ndio maana waandika hivi ' ikiwezekana wenye wagonjwa wawaweke kwenye magari nao waandamane mpwa kenya wanakula shavu na wagonjwa walikomaa tena wengine walipata uponyaji unachotkaiwa kuwaa mbia wanamaombi na wewe mwoombee wakati w a huu mgumu watu waendelee kupona watoke hospital wakirudi wakutanena yale ma shuka ya davos
 
Kuna dk mmoja kaweka wazi siebdi kazini sitaki kudanganya nafsi yangu
kwa nini niende huku moyo unahuzunika alafu nikiumia sna nimwongezee dose mgonjwa wakati ninaohangaika nao wako kwenye ac..bora abakinyumban so we kama mtanzania sasa mwambie mungu akusamehe dhambi zote ulizofanya kwa kuwaza kunena na kutenda na kwa kutotimiza wajibu upi usiniulize then mwombe awaponye wagonjwa wa muhimbili ukiwemo wewe mens usiumwe wakati huu wa mgomo mpwa maana utatuingiza kwenye mawazo wa jamvini
 
Mtaandamana wapi na kuna al shabaab?waache wenyewe maDR ambao wanajua ni namna gani kiatu kinawabana wagome mkuu!
 
Mchambuzi yote uliyayasema yana ukweli mkubwa sana. Lakini, ni matokeo ya sera naul uongozi wa CCM. Hatuwezi kabisa kutenganisha matatizo haya na uongozi wa kisiasa uliopo, siyo?
 
haya mkuu,ngoja waje wenyewe!watategua kitendawili hiki cha Kalumekenge
 

mkitaka kuandamana watasema kuna chama kimepanga huu mgomo,bora liende kimya kimya tuone watasingizia nini,nachojua serikali kwa sasa wanatafuta pa kutokea mkipanga maandamano tu,si muda mrefu utamwona wasira anaongea upupu!!!
 
Mchambuzi yote uliyayasema yana ukweli mkubwa sana. Lakini, ni matokeo ya sera naul uongozi wa CCM. Hatuwezi kabisa kutenganisha matatizo haya na uongozi wa kisiasa uliopo, siyo?

Mwanakijiji,

Upo sahihi, mzigo huu ni wa CCM na Serikali yake. Muundo uliopo sasa ni ule ule ulikuwepo hata chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa. Kilichobadilika sana sana ni ushiriki wa sekta binafsi baada ya mageuzi ya kiuchumi kuingia, vinginevyo sekta ya umma na ya NGOs, hata wakati wa ujamaa zilikuwa zinashiriki kama ilivyo sasa.

Mtunzi wa "3 Tier System" ya sekta ya afya: Primary, Secondary, Tertiary, ni yule yule aliyetunga a "3 Tier System" ya sekta ya elimu - Primary, Secondary, Tertiary, ambae ni serikali ya TANU/CCM. Na kama ukiangalia kwa umakini, system zote hizi zina matatizo kwa upande wa ufanisi. Inawezekana kuna umuhimu wa kuzibakisha in the same order lakini kuna ulazima wa kurekebisha vitu vingi sana, kwani RASILIMALI WATU ya Nchi (HUMAN CAPITAL), ni zao la elimu bora na afya bora, sekta ambazo haziendeshwi kwa ufanisi hivi sasa, chini ya serikali ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…