Nawaunga Mkono Madaktari

Mkuu wangu samahani sana sikuweza kukuijibu haraka kutokana na wapuuzi fulani waliokuwa wakinihemea karibu kwa mashuzi ya mdomo.. Nashukuru sana tumefika mahala labda tuelimishane ktk maswala muhimu zaidi ya kijamii kati ya Uhafidhina na Wajamaa wa Kidemokrasia..

Kwanza kabisa naomba nikusahihishe ktk Ubepari maana hapa hili swala la Soko huria ni Azimio lililopitishwa majuzi tu ktk kuboresha nguvu ya Ubepari lakini Ubepari ulikuwepo toka enzi za mitume kina Abraham wakichunga kondoo na kuwauza nchi za jirani nao wakirudi na makasha ya dhahabu na kadhalika. Mesopotamia ilijengwa kwa biashara kubwa na elimu yetu letu asili yake imetoka huko..Ubepari kama ubepari una athari zake na ndio maana miiko inatakiwa kuwepo pasipo kujali Uhafidhina wala Ujamaa maana tunapozungumzia Biashara sidhani kama Ujamaa wa leo unapingana na dhana ya biashara na soko huria isipokuwa kwa uzito wa masharti ndipo tunapogongana...

Sasa nirudi ktk Uhafidhina wangu, binafsi kitu cha mwanzo natazama TULIPOTOKA.. sababu ya kuutaka Uhuru wetu na kisha baada ya hapo natumia Uhafidhina wangu kuweza kuulinda Uhuru kama haki yangu maana tatizo la Wajamaa mara nyingi husahau kwamba HAKI (Justice) na UHURU (Freedom) ni wa WATU sio wa viongozi au serikali. Na hawa watu wanatakiwa kulindwa kwanza kabla hujatazama nje ya mipaka hii. Ujamaa kwa aina fulani unataka kuwapangia watu maisha, kuwapangia Uhuru wao na kuwapangia hata elimu na afya zao kama vile wakati wa Nyerere ukimaliza darasa la 14 unaambia wewe unakwenda UDSM kusomea Udaktari wakati hukutaka kuwa Daktari bali Lawyer. Ujamaa wa demokrasia bado nao unawapa wananchi Haki na Uhuru kwa mafungu, hivyo Mwananchi anakuwa sii Huru bali Uhuru wake ni wa kupakuliwa ktk sahani kama unanunua biriani pale Chef Pride..Ujamaa unajenga fikra za Uhuru wa serikari au chama iliyoingia madarakani kama ndiye mdhamana wa Uhuru na Haki ya wananchi. Na ndio maana hamtaki kuondoka madarakani mnaposhindwa huwa kazi sana kuwaondoa..

Umezungumzia swala la Uhafidhina kuwakera watu wa mrengo wa kushoto na kati ati kwamba Uhafidhina hautazami watu maskini.. Kweli tunawakera lakini kwa sababu hamtazami HULKA ya binadamu na walivyojaaliwa. Katika Uhafidhina hatuamini Umaskini kuwa ni kilema au ugonjwa sugu bali ni mtu kutowezeshwa ktk hali na mali. hakuna mtu aloumbwa maskini wala kuomba kuzaliwa maskini..Mtu yeyote akipewa ELIMU bora bila shaka utapata kazi nzuri na maisha ya binadamu yanategemea kufanya kazi. Mwenyezi Mungu alisema sisi wote watoto wa Adam - Tunaishi kwa jasho letu.

Hivyo, mnapomwandaa biandamu kuboresha maisha yake ni jukumu la serikali kuhakikisha linaweza sera bora za kuzalisha ajira ua Uwekezaji..Uhafidshina unatambua hilo kwanza na Uhafidhina hauweki binadamu ktk makundi kama mnavyofikiria, japokuwa yapo kweli lakini tunachoamini ni kwamba kila mmoja wetu ameumbwa na uwezo na kipaji na anastahili kupewa nafasi kuwezeshwa na atafika popote anapotaka kufika bila kumtazama kama maskini au kilema.

Ujamaa tatizo lake unalea watu ktk umaskini wanatambua umaskini wa watu kama kilema vile.. na kusema aaah maskini hawa tuwasaidie..hivyo kuwalemaza watu hawa ktk umaskini kwa vilio na kuonewa. Tabia ya kuwalea watu kama maskini kunawajengea ukungu akilini wakaamini na kukubali matokeo hivyo wataishi kama maskini wakitegemea kusaidiwa. Haya ndio mazao ya Ujamaa na demokrasia. Tanzania leo ni mfano mzuri sana wa Ujamaa na demokrasia maana wananchi wamekubali kushindwa baada ya serikari kutowafikiria kabisa wao bali wageni ambao wanakuja nchini kuwekeza. Uhafidhina unakupa Ushujaa na ujasiri wa kusimama na kupiganisha malengo uloyaweka, unakupa Haki na Uhuru wewe mwenyewe kuamua unataka kufika wapi hakuna vikwazo bali kikwazo utakuwa wewe mwenyewe.

Kwa Tanzania yetu ya leo hii, hajtujui tumesimama wapi wala tumetoka wapi.. hatujui na ndio maana hatuna hata Historia ya Uhuru wetu isipokuwa kwa Udini na Ukabila..Haya tukiweka na mchanganyiko wa kukubali Ubepari wakati bado kiimani Watanzania wengi ni Wajamaa au Liberal wamekosa HOPE kabisa... Hivyo ili nao watoke wameona UFISADI ndio njia pekee ya kutokea maana serikali haijui imesimama wapi..Kina JK kwa kuchanganyikiwa hawaoni ubaya kwa mwenyezaji kutoka nje ambaye kwa aina fulani anarudhisha UKOLONI mamboleo kuwekeza nchini maadam ati anakuza GDP..Na mimi mhafidhina sikubaliani na uwekezaji wa wageni- GDP nitaikuza mimi mwenyewe toka pale nilipo hata kama ilikuwa -20 ndipo naweza kujipima uwezo wangu kuzalisha..

Sasa Tazama, Nyerere ambaye alikuiwa Mjamaa haswa alifanya nini? alikataa kuwaleta wawekezaji nchini kuchimba madini yetu akisema yabakie huko chini hadi vijana wake watakapoweza kushimba wenyewe.. Huyu Mjamaa lakini katumia Uhafidhina ktk kupinga kukoloniwa tena..Ufafidhina kwa nchi kama Tanzania unautazama kwa mazingira tulipata UHURU wetu, nini zilikuwa itifaki zetu na malengo gani tuloyaweka while fighting the power..Mawazo hayo yanatakiwa kuenziwa na ndipo uhafidhina wangu unapotulia kama maji mtungini..

Kuhusu swali lako la wagonjwa wanaokwenda Mwananyamala, Temeke na Ilala ni mpango wa serikali ambao unawataka wagonjwa waende kwanza Hospital zao kisha wanakuwa reffered Muhimbili au hospital hizo. Huu ndio utaratibu uliopo na ndio maana unaona watu wengi wanakwenda kwanza ktk Hopitalk za majimbo yao kabla hawajapelekwa za Kitaifa. Mimi sioni tatizo kabisa hapa mkuu wangu, huu ni mpango mzuri sana na umeondoa sana mlindikano wa watu Hospital kuu. Isipokuwa tatizo linakuja kwamba hizo Hospital za Temeke, Ilala na Mwananyama zinatakiwa kuboreshwa zaidi ili zipate kuwa na vitanda vingi zaidi..

Halafu kama kweli huwa zimejaa lakini kuna vitanda Muhimbili au AghaKhan viko wazi basi hii inaonyesha mipango mibovu ya ushirikiano baina ya hizi Hospital maana Huku majuu kuna utaratibu mzuri sana baina ya daktari wako na Hospital zote zinazohusiana na maradhi yako. Na sababu nyingine inaweza kuwa gharama maana kutokuwepo mfumo bora wa tiba unajenga matabaka ya wagonjwa ayani asiye na uwezo aende Ilala, Temeke na Mwananyamala aliki akiugua Mchambuzi hupelekwa Muhimbili au Lugalo moja kwa moja.

Ndipo mimi napopingana na mpango nzima wa Afya nchini na kusema unajenga matabaka. Wahafidhina hawawezi kunipinga mimi naposema serikali itoe ruzuku kwa wananchi.. Hata kidogo labda huyo mhafidhina kichaa ambaye hafahamu tumefika hatua gani.. Mkuu wangu bado kabisa tupo ktk Transition ingawa kina JK na wasomi wetu wanadai tumeisha toka huko sasa tunaelekea ktk Transformation. Kwanza kabisa Uhafidhina unajali AFYA ya wananchi na pengine tunaweza sema kuliko hata wajamaa kwa sababu tunaenda na mahesabu. Sasa unapokuwa ktk Transition unakutana na vikwazo vingi na kimojawapo ni kwamba wananchi wenyewe wazawa hawana uwezo wa kujenga majengo makubwa kama Hospital iwe hata ya Mwananyamala.. sii rahisi, hivyo hatuwezi kudai hii ni biashara maana majengo haya siyo biashara isipokuwa watoaji huduma za AFYA. Na ndio maana unaona tunakubali sana kutoa fedha za uwekezaji ktk majengo ya Hospital lakini Hospital yenyewe inajiendesha ikiwa na uongozi wake kama shirika binafsi bila kuingiliwa na wanasiasa kama tunavyoona Tanesco. Hospital hizi zinafanya biashara na kuajiri madaktari bingwa hivyo kuwapa mtihani mkubwa viongozi wake hata kama mteja wake mkubwa ni serikali yenyewe - Umenipata hapo!.

Na uzuri wa Demokrasia ni pale pande hizi mbili zinapopambana kisi kwamba hata sisi wahafidhina tunakubali baadhi ya huduma kama hii hasa inapolenga AFYA na wananchi tunachokipinga tu ni kama huduma hii itamgharimu mwananchi zaidi ktk kodi na afadhali angehudumiwa na Private hospital akilipa mwenyewe. Kwa hiyo kwa nchi nyingi za Kibepari zimegundua kwamba huduma kama asfya ni fedha ile ile inatoka mfuko huu na kwenda mfuko mwingine..gharama ambayo ungeilipa wewe kwa tiba serikali inachukua fungu hilo na kukulipia wewe toka ktk kodi yako na ndio maana Canada na nchi nyingi zinazotoa huduma hizi tuna kodi kubwa sana kutokana na maswala ya Afya na Elimu kuwa bure..

Marekani bado wana ugoinjwa wa kufikiria kwamba watumishi wa serikali ni wazembe ukiwapa AFYA na ELIMU wanaziboronga na kuwa huduma mbaya sana kwa sababu in general mfanyakazi wa serikali hana uchungu..Lakini nadhani baada ya kutazama nchi nyingine wanagundua kwamba elimu na AFYA ktk nchi hizo imezidi kuboreka zaidi baada ya kuzifanya mandatory na HAKI ya mwananchi.. na kinachofunga zaidi ni imani yetu ktk HAKI na UHURU. Tunataka mtu achague yeye mwenyewe anataka kusomea nini, shule gani atibiwe na daktari au Hospital gani badala ya kuwa reffered to kama tunavyofanya Tz. Na huwezi kutatua tatizo hili bila kuujua mfuko wa mtu isipokuwa ukimpa mtu jukumu hilo anajua vizuri uwezo wake hivyo kujipangia malengo na sio kupangiwa..

Duh! nimeongea sana mkuu wangu tutaendelea baadaye..
 
Mkuu wangu nakuelewa sana na ndicho nilichokisema huko nyuma nikashambuliwa baada ya kuwalaumu wanaohusika na AFYA nchini.. Nimewaomba waiweke hapa Artical 1 vifungu A hadi D tuvisome sote na tujue kina nano wa kuwalaumu watu wamenigeuka kwa sababu tu taasisi husika inawahusu.

Mkuu wangu Bongo huwa naenda kila mwaka na hukaa miezi zaidi ya minne toka 2005, sasa huwezi nambia kwamba siijui hasa alwatan ambaye nashinda kutwa mujini vijana wa mujini. Naijua Bongo kama kiganja cha mkono wangu mkuu wangu.
 
Dah Mkuu Mkandara na August, aksanteni sana kwa ufafanuzi wenu.

Kimsingi nadhani katika madai yao hayo yapo yale ambayo yanatugusa moja kwa moja wananchi mf. vifaa vya kututibia, vitanda e.t.c. Kwa hali hii suala lao linatugusa moja kwa moja na sisi wananchi na ndio maana toka kwanzo nilisema tusiishie kupiga kelele tu kuwa wagome, wasitibu wagonjwa lakini wanaozidi kuumia ni sisi wenyewe. Hebu tujiulize ni lini serikali ilishawahishtakiwa kwa kusababisha vifo vya wananchi wake kwa uzembe? ni mara ngapi wanaotupiwa lawama ni madaktari ilhali uzembe unaweza kuwa umetokana na serikali yenyewe? Mfano mgonjwa anafia hospitalini kwa sababu tu hakuna dawa ya kumtibia? huo si uzembe wa daktari anayemtibu ni wa serikali lakini lini serikali waliwajibika kwa hili na mengine kama haya?? Sisi ndio tunaoangamia, tunapoteza ndugu na jamaa zetu na kubaki na mapengo yasiyozibika kwenye familia zetu na mbaya zaidi wakati mwingine tunarudishwa nyuma kimaendeleo kwani pengine anayeondoka anakuwa ndiye tegemezi letu.

So ni vema tukaungana wote kwa pamoja na kuangalia namna ya kuufikisha ujumbe kwa serikali iwe ni kwa maandamano au njia nyingine yoyote kama kulala barabarani kama wazee wa Afrika Mashariki.

Ila wasiwasi wangu juu ya nguvu ya maandamano hayo. Hawa wakuu wasijeishia kusema waache waandamane leo kesho watarudi makazini!!
 

Nyumba zenyewe sisi mawaziri hatuzitaki na wengi hatujaamia, wanajikomba sana kwa mawaziri wakati tuna uwezo wakujenga nyumba zetu.
 
Siungi mkono madaktari kugoma kwanza hawana uzalendo hasa wa muhimbili. Huwa hawawatendei haki wagonjwa wa hali ya chini. Mtu ukiwa wa hali ya chini ukaenda muhimbili utashangaa make unaweza ishia kupata ugonjwa wa frustration hasa ukilazwa.

Kwa hiyo wangekuwa wanajali watu wa hali ya chini ungewaunga mkono?
 
Samahani...nadandia treni kwa mbele...! Mkuu hii ya 40,000 kumuona daktari umeshaisema mara nyingi na kama kumbukumbu zangu hazijakosea ulishawahi kusema pia kuna wakati mlishindwa kumlipia mgonjwa wenu kwenye hizi hospitali zinazopokea ruzuku ikabdi mumpeleke India... Hivi hauwezi kweli kutuambia jina la hiyo hospitali? Ni hilo tu.
 
Inashangaza kuona wafanyakazi wa sekta nyingine wametulia as if wamaridhika na kipato chao
 
Serikali imefanya miscalculation kubwa sana ya kutoelewa hisia za taifa. Walifikiria kuwa wananchi watawakasirikia madaktari na madaktari watapoteza support. So far, overwhemingly wananchi wako na madaktari! It just make sense!
 

Sisi tutaendelea kupambana na kuwa expose mafisadi wa mali ya umma hadi kieleweke hasa wa kanisa...hata kama utatokwa na mapofu hatutaacha..maana dhulma lazima ikemewe hadi wananchi watakapoelewa..na kuchukua hatua ..mtaendesha wenyewe hizo projects za kanisa siyo kwa mihela ya umma... Unalialia nini sasa unapenda kupendelewa...wazima kweli nyie
 
Serikali imefanya miscalculation kubwa sana ya kutoelewa hisia za taifa. Walifikiria kuwa wananchi watawakasirikia madaktari na madaktari watapoteza support. So far, overwhemingly wananchi wako na madaktari! It just make sense!

Nani amefaidi na nani amepata hasara? think of common mwananchi..
 
Nani amefaidi na nani amepata hasara? think of common mwananchi..

Mabadiliko yana gharama; wakati mwingine ni gharama kubwa kweli! Jiunge nasi kuishinikiza serikali to show leadership and resolve this conflict. Usiitetee serikali wakati inaboronga kwani ni kujaribu kuwa upande mbaya wa historia. Ni lazima uwe unaishuku serikali na usiogope kuikosoa kwa sababu utaonekana mpinzani au utaonekana unaionea serikali. Mara zote try to push the government.
 

Unaonaje tukiwashauri serikali wachukue zile bil. 90 za MoU ya kanisani wawape madaktari itakuwa sawa?
 
Unaonaje tukiwashauri serikali wachukue zile bil. 90 za MoU ya kanisani wawape madaktari itakuwa sawa?

Sure, why not! na wakishatoa hizo unaamini zitatatua tatizo la mgogoro wa wa sekta ya afya? Kama unaamini hivyo I support hiyo.
 
Sure, why not! na wakishatoa hizo unaamini zitatatua tatizo la mgogoro wa wa sekta ya afya? Kama unaamini hivyo I support hiyo.

Bil.90 si ndogo inaweza kutatua tatizo sana maana kwasasa hazijulikana zinaenda wapi hasa?

Kama ndivyo washauri wananchi wa support kuondoa MoU ya kanisa na serikali as an immediate solution; sauti ya wakristo imekosekana sana kwenye jambo hili utakuwa wa kwanza kuthubutu
 
.....Naomba nisiumwe kwa hali hii i wil easy die
 


Mbona unafanya kazi nzuri tu keep doing. Huitaji kuwashawishi wanchi unahitaji kuitaka serikali kuvunja hiyo MoU. Tatizo nikuwa huoni serikali ndiyo inahusika na yote mawili -la MoU na la madaktari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…