Nawafikishieni Ujumbe Mnaoendesha IST na Vitz

Kuna mwanasiasa kasema mkishanunua IST na VItz na kuanza kuvaa kaptura fupi weekend mnajiona mmepatia sana maisha, mnajihisi ni middle class kumbe ni masikini wenye nafuu! Mjumbe hauwawi, weekend njema!
Mwambie aje alipe madeni ya mabenki kwanza ndiyo aongee.
 
Sasa ukikutana na mtu anasukuma discovery kwanza kala jeanz casual, shati au tishet casual kiatu ni american boot, timberland, clacks na hana maneno mengi utaona mezani pana grants, Jackdaniel, gordon, halafu akipigiwa simu haongei kwa sauti kubwa ni kidogo kakata utaona kama sio discovery, VW , Ranger, Range hapo unajua mipango ipo yaani full of civilization
Acha kabisa
 
Kuna
Binafsi nimemuelewa sana Lema. Ni sawa na banker sijui cashier akishapata kibarua bank anahesabu hela nyiingi za watu anavimba mbaya, jioni sijui ijumaa kavaa zake kinjuga na slippers, juu jezi yake na iphone hale second hand, jeuri zote town anamiliki kwakua anamudu kununua bia 2 na kitimoto basi anaona maisha ameyamaliza ilihali amejaa madeni kibao anajiona middle class family wakati kajamba nani mwenzetu tu. Yaan kuna mtu akishakua na kitu kidogo anaona maisha ameyamaliza. Huwezi muelezea masuala ya nchi akakuelewa. Yeye ilimradi kakshahara kake kameingia, IST yake inapata wese basi.. kutwa mliman city

Tuwajuze tu, maisha baado sana. Hamjayapatia. Na vinjuga muvifue hivyo na matishet yenu. Alaaaaa.
Kuna mmoja huyo anatimua vumbi balaa na taa 'amezimeremetesha' ni vujo Tu.
Huwa nazikubali Sana IST hata ivyo
 
Mshamba Sana aliyeongea hivyo..
Hana akili..
Watu Wana Range Rover na bado Wana IST ..

Kulazimishana mitazamo ya kisiasa in a very abusive language...

No wonder naamini ana background ya ujambazi...

Mwanasiasa anatakiwa ashawishi watu
Sio Ku attack na kuponda certain group
..... siasa za CHADEMA hizo....

.......hao ndio NGULI wa siasa za CHADEMA.....

......SIASA ZA "TUG OF WAR....

#HakunaNamnaKaziIendeleeTu
 
Kuna mwanasiasa kasema mkishanunua IST na VItz na kuanza kuvaa kaptura fupi weekend mnajiona mmepatia sana maisha, mnajihisi ni middle class kumbe ni masikini wenye nafuu! Mjumbe hauwawi, weekend njema!

Hahahaaa kuna jamaa ni TISS yaani yeye akija hata bar kunywa gari yake aizimi anaacha inaunguruma mpaka amalinze kunywa au kula! Huwa najiuliza kama anaiga viongozi wa serikali wanavyofanya kwenye mafuta ya bure ina maana akiwa nyumbani kwake gari nayo haizimi au mwembewe/showoff?
 
Mimi nina vitz old model hata hapa ninaiendesha hiyo gari. Mbali na hayo nina Harrier Hybrid nina Prado na pia nina gari zingine za biashara. Sijawahi kujutia kuwa na Vits.

Mnaowaita maskini ukute wana maisha mazuri mara kumi ya wewe mwenye gari kama Subaru.

Kuna dogo mmoja alinichomekea vits nikamwambia kuwa mwangalifu akasema kwenda zake na gari ya house girl. Gari aliyokuwa anaendesha ni ya chini kuliko niliyomnunulia mwanangu anayeanza chuo kikuu


Ukinunua viatu vizuri ukaweka kwenye kabati kisha ukavaa ndala miba na vyupa vitakuchoma tu bila kujali una viatu nyumbani.
 
Mwanaume above 30 years kuendesha IST ni unajisi. Hiyo ni gari ya kuhonga. Makonda was very right.
 
Kuna mwanasiasa kasema mkishanunua IST na VItz na kuanza kuvaa kaptura fupi weekend mnajiona mmepatia sana maisha, mnajihisi ni middle class kumbe ni masikini wenye nafuu! Mjumbe hauwawi, weekend njema!
Vipi kuhusu kushika smartphones mbilimbili na kuning'iniza funguo kwenye luksi naona hujalizungumzia ndugu mleta mada
 
Kuna siku sijui nilikuwa nawaza wapi nikajikuta nimefunga mlango kwa nguvu kidogo
Nikasikia “sister hili siyo grili polepole tu unafungika”

Wabamiza milango mnazingua.
 
Mungu akitaka kukushusha anakupa kiburi, dharau, majivuno na mengine kama hayo.

KWELI, leo hii kuna mtanzania mwenye akili zake timamu anaweza kuponda ist zinazomilikiwa na watanzania wenzake?

Labda sio mtanzania anayefahamu hustles halisi za watanzania ambao wengi wetu tunapambania milo mitatu kwa siku.

Wamiliki wa gari mitumba mmeanza kuzodoana? Ngozi nyeusi imelaaniwa.

Anyway sisi wa ist tuendelee kumpa 'Mungu utukufu wake kwa kutuheshimisha na ist zetu'. Amen.

Punguzeni vurugu bwana

Mbona sisi na passo zetu barabarani tumetulia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom