KERO Nauli zinapanda MBEYA na SONGWE kiholela

KERO Nauli zinapanda MBEYA na SONGWE kiholela

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Umbali kutoka kyela-mbeya mjini ni km 83 nauli ilikuwa sh.7,000...imepanda Hadi sh.10,000.

Pia umbali Toka tukuyu-mbeya mjinj ni km 45 nauli ilikuwa sh.4000 imepanda Hadi 5000.

Pia umbali Toka mbeya-tunduma ni km. 103 nauli ilikuwa sh.5000 Sasa imeongezeka Hadi sh. 7000.

Yaaani tunduma-mbeya 103 kms za lami, nauli sh.7000 wakati Kyela - Mbeya km.83 nauli 10000. Huu ni wizi na Kuna viongozi wanakula rushwa Toka Kwa madereva na wamiliki ktk upangaji wa nauli..

Tunaomba kikokotoo cha nauli kiwekwe sawa na nauli zishushwe maana ni kinyemela

Tunaomba nauli zisipande Mbeya-Kyela na Mbeya - Tunduma kwasababu hata nauli zilizopo ni zaidi ya umbali..umbali kidogo kuliko nauli..

Pia wasipandishe KIHOLELA maana wameshaanza kupandisha wakati Latra haijaruhusu
 
Back
Top Bottom