Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,303
What is it?
Its a fact
When has this government been awake? With the hike in nauli, its still asleep
What is it?
Asante kwa mchango wako,
Tunachokijadili ni ongezeko la sh. 200 tu, mjadala kuhusu wenye baiskeli za guta hatujauingia bado; vinginevyo, nakubaliana kimsingi na hoja kwamba magufuli angeomba tu msamaha kwa kauli zake, lakini uamuzi wake juu ya nauli, kwa mazingira ambayo so far tunaeleweshwa na kuyaelewa, ni maamuzi sahihi;
Root imefichwa, mengine yote humo ni siasa, serikali haina hela ya ruzuku, wamepandisha nauli kukata makali ya ruzuku, wakisema hayo ni watajimaliza kuna issue ziko related na hizo zitaibuka, huko ndio ukweli wanakata rukuzu
hakuna faida inayopatikana kwenye kivuko kiasi cha kununua kivuko kingine hapo kachanganya habari
Na mimi mlalahoi naomba kutoa hoja kidogo, kama hiki kivuko kinaendeshwa na serikali naomba sisi waenda kwa miguu tusilipe kitu. Swali la nyongeza ni je ikijengwa daraja, itakuwapo na njia ya wapita kwa miguu na ikiwepo je tutatozwa nauli ?
Mkuu mchambuzi,Hivi tunatambua kweli kwamba daraja likijengwa litakuwa na urefu wa kilometa kama saba kuanzia linaponyanyuka kurasini na hadi linapotua kibada? itagharimu sh ngapi kwa dala dala kilometa saba, kama kilometa tatu kuanzia ferry hadi posta ni sh 300?
Na je, hivi tunatambua kwamba daraja likikamilika, sio kwamba litashukia upande wa pili wa feri kule kigamboni, bali kibada, na itahitaji kupanda daladala kwa kilometa kama 18 ili kufikia upande ule wa chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere? jumla ya umbali huu wa kilometa zisizopungua 25 itakuwa sh ngapi kwa daladala? ni dhahiri itakuwa hata mara tano ya nauli mpya ya kivuko; kwa mtazamo wangu finyu, economics za daraja zimekaa ovyo sana, kwani ni bora ulipe sh. 5000 kupita na gari kwenye pantoni, kuliko kujaza mafuta kwenye gari yatakayoweza kukuzungusha na gari lako kwa hizo kilometa 25 ili ufike upande ule wa kivukoni - maeneo ya chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere; vile vile, wakazi wengi sana watachagua kuendelea kupanda pantoni la sh. 200 kuliko kulipa pengine nauli ya daladala ya sh. 1,000 ili wafike upande wa pili kwa kuzunguka kwa njia ya daraja kupitia kurasini - kibada;
Na ni hapo ambapo wananchi hawa watatubu kwa kosa la kumzomea magufuli mwaka 2012 kuhusu nauli ya sh 200;
Mkuu mchambuzi,
Hilo daraja feasibility yake siyo kwa usafiri wa wakazi wa Dar tu.
Pamoja na mambo mengine ni upanuzi wa container terminal ya Dar port, kitu ambacho ni muhimu sana as stipulated in the Southern corridor development schemes.
Very very economically feasible. I stand to be corrected but I'm for it!
iwapo ferry hadi posta ni umbali wa kutembea kwa miguu wa kama km 3, lakini wengi wanalipa nauli ya daladala sh 300,badala ya kutembea, kwa mtazamo wako, unadhani kweli wananchi watatembea juu ya daraja lile kwa umbali wa km sio chini ya saba kutoka kurasini hadi kibada? personally, i doubt it;
Totally agree with your angle.Serikali ikisema haina ruzuku kwa Kigamboni, tutawauliza mbona mnapandishiana posho Bungeni? Mbona mna wabunge wa viti maalum 100 bungeni tunaowalipa kwa kuzaliwa wanawake tu? Mbona safari za viongozi zinakuwa na msururu wa watu, kisha first class, na hatuelewi faida yake? ...
Totally agree with your angle.
Ila, ni afadhali tuachane na ruzuku kwa watu ambao kiukweli wanaweza kumudu 200 shs.
Na hayo mafedha ya posho yaelekezwe kwenye ruzuku za social services.. eg Healthcare and Education for the needy.
iwapo ferry hadi posta ni umbali wa kutembea kwa miguu wa kama km 3, lakini wengi wanalipa nauli ya daladala sh 300,badala ya kutembea, kwa mtazamo wako, unadhani kweli wananchi watatembea juu ya daraja lile kwa umbali wa km sio chini ya saba kutoka kurasini hadi kibada? personally, i doubt it;
Yep,Totally.
But the government needs to come with other austerity measures. Sio watuambie Kigamboni tu
Nimesoma mahali kuwa kwenye kivuko cha Likoni huko Mombasa ambacho ni sawa na cha Kigamboni, abiria wanavuka bure. Eti kinachotozwa kodi ya kuvuka ni vyombo vya moto tuu ikiwamo magari na pikipiki. Hivyo, gharama za kuendeshea kivuko hicho zinatokana na kodi za vyombo vya moto. Hili linawezekana kwa kivuko cha Kigamboni?
Nimesoma mahali kuwa kwenye kivuko cha Likoni huko Mombasa ambacho ni sawa na cha Kigamboni, abiria wanavuka bure. Eti kinachotozwa kodi ya kuvuka ni vyombo vya moto tuu ikiwamo magari na pikipiki. Hivyo, gharama za kuendeshea kivuko hicho zinatokana na kodi za vyombo vya moto. Hili linawezekana kwa kivuko cha Kigamboni?
Hili la kivuko cha Kigamboni linageuzwa kisiasa kwasababu wananchi wa Kigamboni ni muhimu sana kwa wanasiasa wetu au ni kwasababu wabunge hawa wa Dar wanajaribu kulishupalia kujikweza kisiasa? Mh. Magufuli aliweka wazi baadhi ya vivuko na gharama zake, kivuko cha Pangani nimewahi kukitumia sikuona wananchi wa Pangani wakilalamika kulipia shs 200; ukiangalia kwa undani wananchi wa Pangani hawana shughuli kubwa za kiuchumi ukilinganisha na Kigamboni, kumalaumu mh. Magufuli si suluhisho ukweli nauli ya shs 100 haiendani na wakati; hawa waheshimiwa wabunge wanajaribu kulitumia hili swala la kivuko kutulaghai wananchi, hawa si wenzetu; kwanza wangetueleza wamejiongezea vipi posho hadi shs 200,000 kwa siku? Hata kuongezeka kwa nauli ya feri Kigamboni inachangiwa na kuongezeka kwa gharama za serikali, posho za wabunge ikiwa ni mojawapo. Tusikurupuke tu kumlaumu mh. Magufuli kwa hisia zinazojengwa kisiasa tujaribu kuangalia ukweli wa suala zima kwa mapana na marefu.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Technically sirahisi kulinganisha tu kama hivyo, kuna vitu vingi vinachangia
Kwa mfano traffic ya magari na vyombo vyengine kwenye pantoni ni kubwa kiasi gani ukilinganisha na gharama za usafiri? Traffic ya magari na vyombo vyengine ipo wakati wote au ni wakati wa kwenda na kutoka makazini tu?
Juu ya kusema hayo, kuna vingi ambayo Tanzania inaweza kufanya lakini haifanyi kwa sababu wananchi hatupo tayari. Tukiwa tayari serikali itatekeleza
Nimesoma mahali kuwa kwenye kivuko cha Likoni huko Mombasa ambacho ni sawa na cha Kigamboni, abiria wanavuka bure. Eti kinachotozwa kodi ya kuvuka ni vyombo vya moto tuu ikiwamo magari na pikipiki. Hivyo, gharama za kuendeshea kivuko hicho zinatokana na kodi za vyombo vya moto. Hili linawezekana kwa kivuko cha Kigamboni?
Totally agree with your angle.
Ila, ni afadhali tuachane na ruzuku kwa watu ambao kiukweli wanaweza kumudu 200 shs.
Na hayo mafedha ya posho yaelekezwe kwenye ruzuku za social services.. eg Healthcare and Education for the needy.
Tatizo lipo hapa, Wengi wakina nani? Vibopa wenzio wa CCM? AU? Tuwe wa kweli wakazi wakigamboni majority hawawezi kulipa hiyo 300 kwa km 3, Tuache huongo, Mnaolipa hiyo nauli ni Nyie wahuko Mwenge, Masaki na Mbezi, Ili kugeuza na hayo magari mpate siti.iwapo ferry hadi posta ni umbali wa kutembea kwa miguu wa kama km 3, lakini wengi wanalipa nauli ya daladala sh 300,badala ya kutembea, kwa mtazamo wako, unadhani kweli wananchi watatembea juu ya daraja lile kwa umbali wa km sio chini ya saba kutoka kurasini hadi kibada? personally, i doubt it;
Mkuu daraja likijengwa panton itaendelea kuwepo kama kawaida. Mkuu nina shaka kwamba hilo daraja litakuwa la kulipia kwa kuwa huu ni mpango wa (PPP). Tutasikia wiki ijayo kwa kuwa ndio ujenzi wa daraja utakuwa unazinduliwa rasmi. Lakini asilimia kubwa ni kwamba hilo daraja litakuwa la kulipia.Ni muhimu kuwa iwekwe japo kama itatumika kwa watu wachache sana. Pia ninadhani pantoni liendelee kuwepo japo daraja likijengwa ili kurahisisha hali ya usafiri jijini
Mkuu vivuko vingi hapa nchini vimenunuliwa kwa mkopo toka World Bank. Ni vichache sana tumenunue kwa pesa zetu. Lakini jamani mbona hatujiulizi ni kwa nini bei ya sukari imepanda kutoka 500 hadi 2,000 kwa kilo ma hatukugoma. Watu wa kigamboni waligoma kulipa bei ya sukari baada ya kupanda? Sishangilii kupanda kwa nauli kwa kuwa kuna kiloo kwamba kuna ivujaji wa mapato hapo feri. Serikali ingeziba kwanza mianya kisha ikapandisha nauliUkweli ni kuwa Kigamboni ni Nyomi Nyomi wakati wote( Na ndio maana wakajenga kipya kikubwa zaidi na mara nyingi vina operate Viviwili kimoja ngambo na kingine ngambo nyingine vinapishana katikati), watu kibao, Magari Kibao sasa inakuwaje wanakifananisha na cha Kilomberro, Ambacho mara nyingi kinaenda Tupu?