Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe?

Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe?

Na mimi mlalahoi naomba kutoa hoja kidogo, kama hiki kivuko kinaendeshwa na serikali naomba sisi waenda kwa miguu tusilipe kitu. Swali la nyongeza ni je ikijengwa daraja, itakuwapo na njia ya wapita kwa miguu na ikiwepo je tutatozwa nauli ?

Inabidi ulipie hata kwa mguu, kwani pesa zitarudi je hizo bilini kadhaa.
 
Mchambuzi,

Asante kwa maoni yako ingawa naona umeingia mtego wa Waziri Magufuli wa kuhamisha mjadala wa Kivuko kuwa Mjadala wa Ubungo.

Asante sana kwa kuturudia kama ulivyoahidi, ingawa bado kuna masuala mengi ya msingi haujayajibu, kwani suala la sh. 200 ya kituo cha ubungo, kama ulinifuatilia vizuri, ilikuwa ni sehemu ndogo sana ya mjadala wangu.

Kuhusu mimi kuingia mtego wa Magufuli, suala hapa sio mtego Mheshimiwa Mnyika, kwani sote (mimi na wewe) tunatoa kauli, misimamo, na hoja zetu kutokana na uelewa wetu wa hali halisi, na sio vinginevyo. Vinginevyo, kwa mtazamo wako huo wa mitego, mimi pia ningeweza kabisa kusema kwamba hata wewe Mh. Mnyika umeingia kwenye mtego wa wabunge majirani wa jimbo lako - Waheshimiwa Mtemvu na Zungu, kitu ambacho sio kweli. Tunachokiangalia hapa ni kwamba - serikali imetoa uamuzi, na je, kauli, hoja na misimamo yetu juu ya maamuzi hayo, inaangalia hali halisi? Je hoja zetu ni za kimantiki na zenye kutumia vizuri takwimu husika? Au ni hoja zenye msukumo zaidi wa kisiasa, au kwa kutumia kauli yako 'mitego'?

Maadam sasa tumekuelewa zaidi baada ya ufafanuzi wako, hakika tuna mengi sana sasa ya kuzidi kukuhoji, lakini binafsi, nisingependa mimi na wewe tuingie katika huu mjadala zaidi humu JF, kwani kwa nafasi yako, hapa ni mahala pako pa kutoa ufafanuzi tu pale panapohitajika, na sio vinginevyo. Nadhani umenielewa. Vinginevyo sisi wana JF tupo, na tutatumia maelezo yako kuzidi kueleweshana, na kubadillishana mawazo juu ya ufumbuzi wa sakata hili.

Kazi njema Mheshimiwa.
 
Swali lako ni kuhusu 200, kwni kabla ya 200 alikuwaanafanya nini akiwa hana hela?

Sio lazima mje mjini.

kwa hili jawabu lako maana yake ni kwamba wenye haki ya kukaa mjini ni wenye hela tu, siyo?
 
kwa hili jawabu lako maana yake ni kwamba wenye haki ya kukaa mjini ni wenye hela tu, siyo?

Kama huna hela utatusumbua tu hapa mjini kwa vi-mizinga vyako vya kila siku!!
 
Wabunge wetu wa DSM wanajitahidi kucheza na akili za watu kwa swala la kupanda nauli kivuko cha Kigamboni kwa manufaa yao binafsi kisiasa na sio kwamba wanawa tetea kwa dhati wapiga kura wao wanaijidai kuwa tetea. Mimi ningewaona wamaana kama wange kataa kuongezewa posho na kuagiza fedha hizo(za ongezeko la posho) zilipwe kama ruzuku ya kuendesha kivuko cha kigamboni ili watu wavuke BURE. Kwa hili wabunge wa DSM wanatakiwa kuwaomba radhi wakazi wa Kigamboni na DSM kwa ujumla kwa kitendo chao cha kuwatetea KINAFIKI
 
Muulizeni Mh Mnyika msimamo wa chama chake juu ya sakata hili. Tumemsikia Mwenyekiti wa CCM-Dar, kijana wa ENL, akimshukia Maghufuli!
 
NDIO!!
Sasa kwanini tunaongeza nauli? hili ile ipatikane ya kuendesha cha Pangani? Kilombero? au?
Magufuli si alisema kuwa Kigamboni inaendeshwa kwa hasara na ina hudumiwa na vivuko vingine?
huoni kuwa katu danganya?

Thamani ya 200 huioni?
Pople sana ndugu yangu unless wewe ni Fisadi au ni mzee wa Rushwa,
Tajiri yeyote na mtu yeyote anayejali matumizi na bajeti kwa vyovyote 200 ni kubwa sana, just Imagine ni watu wangapi kwa siku wana vuka pale? Ndio maana huwa tunaibiwa sana, Fikiria kampuni ya simu inawateja 5Mil ikiwaibia wateja wake wote kila mmoja ndani ya wiki 200 200, ni shilingi ngapi? Tuache dharahu!!!!

Huitaji kuwa fisadi kujua maana halisi ya thamani ya shs, ukweli utabaki palepale, shs 200 haina thamani hii ni karibu na bure kumbuka hapa hatuongelei shs 2000, hakuna uwiano wa mfano wa kampuni ya simu na nauli ya feri, kivuko cha Pangani kinajiendesha chenyewe kwasababu watu wa Pangani waliamua siku nyingi kulipa nauli inayoenda na wakati, hawapo kwa kutegemea favors za wanasiasa.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
We jamaa wa wapi? au unafikiria kutuimia MASABURI? aliyekuambia kwetu KIMBIJI tunauwezo wakumiliki hilo gari ni nani? uwezo wetu ni baiskeli na guta kama hujuhi.
hona hapa!
NDIZI_KTK_BAISKELI_PIX_NO_1.JPG
images
4544488.jpg
712073214.JPG
Guta na mizigo[1].jpg
02.JPG
chakachua%2Bndizi.jpg
IMG_0649.jpg
Sawa sina tatizo na hili lakini yafanye kazi intra-Kigamboni (within Kigamboni, Sokoni <--->Dukani<---->Nyumbani) basi,
sio
inter-city (Kigamboni<----> Dar es Salaam (mzizima)​
 
Majibu Yangu Kwa Mheshimiwa Mnyika

Nianze kwa pongezi za dhati kabisa kwa Mh. Mnyika kwa majibu yake mazuri sana kwa Magufuli, juu ya mambo yafuatayo: Kituo cha Ubungo, Barabara za juu kwa juu, Wakala wa majengo (TBA), na Mafuriko Da-es-salaam.

Majibu haya yangeweza kabisa kunifanya nifunike kombe mwanaharamu apite &#8211; kwa maana ya kwamba ningeacha majibu haya mazuri yebebe pia udhaifu wa hoja za Mnyika kuhusu kigamboni. Badala yake, nimeona kwamba, maadamu sasa Mh. Mnyika ametuelewesha msimamo wake ulitokana na msukumo gani, binafsi nimeona sio vyema kuachilia baadhi ya hoja zake zipite bila mimi kama mtoa mada, kulitolea majibu. Majibu haya nayaelekeza kwenu nyinyi wadau ilituyajadili, siyaelekezi kwa Mh. Mnyika, kwani, kutokana na nafasi yake, sioni kama ni busara sana kumtaka kila wakati aje humu kutoa ufafanuzi, ingawa uhuru huo anao. Mniwie radhi kama ni majibu marefu mno.

Pengine nianze kwa kusema kwamba, kwa maoni yangu, ni muhimu Mnyika akubali tu kwamba ALIKURUPUKA NA MSIMAMO WAKE JUU YA ONGEZEKO LA NAULI KIGAMBONI, hata akiingiza katika Mlinganyo (Equation) huu, Maguta, Bajaji, Magari, na Baiskeli, mbali ya wavuka kwa Miguu. Nitafafanua baadae kidogo. Vinginevyo, kitendo cha Mnyika kukubali kwamba alikurupuka, hata ndani ya nafsi yake pekee (sio lazima mbele ya umma), kwamba hakuwa makini, ni kitendo ambacho kitamsaidia yeye binafsi (sio sisi), kuwa mwangalifu zaidi katika maamuzi yake siku za usoni. Wengi wetu tunampa heshima kubwa sana kama mmoja wa wabunge mahiri, waelewa na makini sana, tuliowahi kuwapata bungeni, na binafsi, nisingependa hadhi yake hiyo ipotee, hasa tunapoelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015. Mimi ni mwana CCM lakini kwa kweli, Where Credit is Due, it has to be Granted, kwani, kwangu binafsi, Tanzania inakuja kwanza, na Siasa inafuata Baadae sana.

Majibu ya Mh Mnyika kuhusu Kigamboni, bado yanaonyesha kwamba, hakuwa na haja ya kujiingiza katika sakata hili: aidha angelikwepa kabisa, au basi angalau angelitolea msimamo baada ya kulichambua kwa umakini wa hali ya juu. Vinginevyo, ukweli unabakia wazi kwamba, Jimbo la Mh. Mnyika (Ubungo), halipakani moja kwa moja na eneo la ferry (tofauti na Ilala na Temeke). Lakini kama aliona ni muhimu alitolee msimamo, aidha kwa nafasi yake kibunge, au kichama, angalau basi ingekuwa baada ya kulichambua suala zima &#8216;ndani-nje', ili msimamo wake uwe na sifa kuu mbili &#8211; CONSISTENCY/UTHABITI & LEGITIMACY/UHALALI, hata kwa miaka kumi ijayo. Vinginevyo, ufafanuzi wake juu ya Kigamboni, unazidi kuacha maswali mengi zaidi ya majibu.

Katika mjadala wangu wa awali nilisisitiza kwamba katika mazingira kama haya, ni muhimu kiongozi awe na sifa pamoja na hizi zifuatazo:

· Consistency au uthabiti katika maamuzi na utendaji, na sio leo hili, kesho lile.
· Upeo na uelewa wa mambo anayoyasimamia au zungumzia kwenye umma.
· Ujasiri wa kuwaambia hali halisi wapiga kura wake, bila ya uwoga.
· Uwezo wa kutofautisha baina ya hoja/maamuzi ya kisiasa na yale ya kimantiki.
· Msimamo usiobadilika/kuyumba kutokana na upepo wa kisiasa.
· Ujasiri wa kusimamia kitu anachokiamini/maamuzi magumu.
· Uwezo wa kufikiri kabla ya kufanya maamuzi muhimu/kutoa kauli au msimamo mbele ya umma.

Katika sakata la Kigamboni, Mnyika anafeli kwenye baadhi ya vigezo hivi. Inawezekana wengi mkalipinga hili, lakini hili ni suala la muda tu, kabla hamjabaini ukweli huo.

Nianze kwa kusema kwamba &#8211; kitendo cha Mnyika kutokuja na takwimu zenye ushawishi, juu ya gharama na mapato, maana yake ni kwamba, anakubaliana na takwimu zangu za awali kama zilivyo. Binafsi, nilitegemea katika ufafanuzi wake juu ya sababu za kupinga GN, angetuletea takwimu zenye ushawishi zenye sura kuu mbili: Moja, takwimu kuhusu gharama za uendeshaji wa kivuko cha kigamboni kwa miaka tofauti; na Pili, ruzuku inayotolewa na serikali kuendesha kivuko cha kigamboni kwa miaka mbalimbali. Vinginevyo, kwa nafasi yake, kama hana takwimu zilizo sahihi, sisi wapiga kura wake tutazipata wapi? Vinginevyo, angefanikisha hilo, angekuwa sio tu na uhalali/legitimacy ya kuhoji kauli ya serikali, bali pia uhalali wa kuipinga Government Notice. Kwa njia hiyo, msimamo wa Mnyika ungekuwa sio tu na Ushawishi, bali pia Mashiko.

Ebu tutazame ufafanuzi wake juu ya msimamo kuhusu nauli za Kigamboni. Katika ufafanuzi wake, Mh. Mnyika ana hoja kuu mbili: Moja, anasema kwamba sababu kubwa kwanini katoa msimamo wa kusitishwa utekelezaji wa GN, ni kwamba anataka serikali kwanza, itoe maelezo kwanini ongezeko la nauli limekuwa kubwa kiasi hicho.

Pili, katika ufafanuzi wake, Mh.Mnyika pia anasema kwamba, shughuli ya vivuko sio biashara, bali ni huduma, hivyo maeneo kama haya yenye vivuko, yalipaswa kuwa na madaraja ili vyombo mbalimbali vya usafiri, kama vile bajaji, maguta, pick up, n.k, viweze kupita, hivyo kupunguzia hadha wananchi. Vinginevyo, anadai kwamba, ongezeko hili kubwa la nauli, litaleta madhara makubwa kwa wakazi wa kigamboni, in terms of ongezeko la bei ya bidhaa zinazotegemea usafiri wa maguta, pick up, n.k, haswa bidhaa za vyakula.


Maoni yangu juu ya hoja hizi mbili za Mh. Mnyika.

Tukianza na hoja yake ya kwanza, Mh Mnyika anaeleza kwamba ongezeko jipya la nauli ni kubwa sana, na anatoa takwimu zifuatazo:

["&#8230;mathalani, Baskeli za matairi matatu (Guta) toka Tsh 200 hadi Tsh 1800 (Asilimia 800); bei ambayo ni kubwa kuliko ya gari ndogo; bajaj zimepanda toka Tsh 300 hadi Tsh 1300 (Asilimia 333); mikokoteni imeongezeka toka Tsh 200 hadi Tsh 1500 (Asilimia 650) na mizigo nayo inatozwa kati ya shilingi 200 mpaka 500".]

Kimsingi, kama anaangalia upande mmoja tu wa sarafu, yupo sahihi. Lakini je, mbona hatuelezi kuhusu upande mwingine wa hoja? Kwani hili suala ni la kimlinganyo/equation zaidi. Kwanini Mh Myika hajatuletea upande mwingine wa hoja? Naelewahoja yake juu ya ongezeko kubwa la nauli (kwa vipimo vya asilimia), lakini hadithi haitakiwi kuishia hapo, na badala yake, JE, Takwimu za ongezeko la gharama za uendeshaji kivuko kwa miaka 14, (1996 &#8211; 2011), kwa mtindo huo huo wa asilimia zinasema nini?
Mbili, JE, takwimu juu ya ongezeko la ruzuku ya serikali katika kipindi cha miaka 14 (hela za walipa kodi), kwa mtindo wake huo wa asilimia, zinasema nini? Asisahau kwamba ruzuku ni gharama kwa walipa kodi hao hao anaojaribu kuwatetea.

Kwani, hata katika mahesabu ya uhasibu, ili mambo yawe sawa, lazima pawe na mlinganisho wa pande mbili, vinginevyo kutatokea tatizo. Mnyika katika hoja yake, anajenga tatizo, kuliko kutatua tatizo. Hata wabunge wengine mahiri, mara nyingi (sio mara zote), huwa wanajitahidi sana kutoa kauli/msimamo, inayoangalia pande zote mbili za shillingi- i.e. msimamo unaozingatia MLINGANYO, vinginevyo, kwa hali ya sasa, msimamo wa Mnyika juu ya kigamboni, sio wa kimlinganyo, hauna mantiki, na hivyo unakosa credibity na legitimacy, kiuchumi, kiuhasibu, na pia uthabiti, sana sana, wa hoja kama kiongozi, "sio kama mwanasiasa".

Ebu tuangalie hoja ya Mh. Mnyika juu ya daraja. Mnyika anasema hivi:

["Nilitaka serikali itoe maelezo ikizingatia kwamba vivuko ni huduma sio biashara kwa kuwa maeneo mengi yenye vivuko yalipaswa kuwa na madaraja kwa ajili ya vyombo hivyo vya usafiri na wananchi kuweza kupita".]

Ni sahihi kwamba kivuko sio biashara bali ni huduma. Lakini ukweli huu ulitakiwa ndio uwe moja ya nguzo kuu za Mh. Mnyika kuangalia suala hili kwa mapana na marefu, kabla ya kuja na msimamo wake mbele ya umma.

Kwa maelezo ya Mnyika, ina maana kwamba uwepo wa daraja ungepunguza hizi kero za sasa, kwa watumiaji wa kivuko cha kigamboni. Ingawa hajatamka kuhusu suala la "opportunity cost", lakini anaashiria matumizi ya kanuni hiyo, lakini hapo hapo anashindwa kufukisha hoja nyumbani. Economics za Daraja dhidi ya Kivuko pale Kigamboni, zinatawaliwa na suala la opportunity cost. Nitafafanua.

Kwa ufupi, Opportunity Cost maana yake ni costs in terms of foregoing alternatives. Katika mazingira ya opportunity cost, ni lazima kuwe na vitu viwili ambavyo mtu au taasisi ina nafasi sawa ya kutumia/kuchagua kimoja, na kuacha kingine. Assumption hapa ni kwamba haiwezekani kuchagua vyote kwa wakati mmoja, kwahiyo, kuchagua kimoja, maana yake ni kukikosa kingine. Kitu cha msingi hapa ni kuchagua kitu chenye faida zaidi (kuliko gharama), katika wakati husika. Maisha yetu kila siku yanaongozwa na hii kanuni, ingawa mara nyingine huwa hatutambui ukweli huo. Nadhani angalau sasa tunaelewa maana ya kanuni hii, vinginevyo utafiti huru utasaidia zaidi wengine.

Tuangalie kanuni hii katika mazingira ya kigamboni. Mnyika anajaribu kutuelewesha kwamba, daraja likiwepo, wamiliki/watumiaji wa maguta, bajaji, na pick up n.k, watakuwa katika hali bora zaidi kwa kutumia daraja badala ya ferry, vinginevyo, kutokuwepo kwa daraja, huku nauli zikiwa zimepanda, kunaleta kero kwa wenye vyombo vya usafiri, akilenga zaidi madhara ya ongezeko la nauli hii kwa wakazi wa kigamboni, in terms of bei kubwa ya bidhaa kama vyakula, n.k.

Mnyika ananukuu taarifa za serikali juu ya ongezeko la nauli Kama ifuatavyo: "Guta toka Tsh 200 hadi Tsh 1800; Bajaj zimepanda toka Tsh 300 hadi Tsh 1300; Mikokoteni imeongezeka toka Tsh 200 hadi Tsh 1500". Mnyika pia anaongezea kwamba "mizigo nayo inatozwa kati ya shilingi 200 mpaka 500".

Lakini anachosahau Mnyika ni kwamba, hata daraja likiwepo leo, opportunity cost ya daraja ni kubwa mno kuliko ile ya kivuko, kwa wote, wamiliki wa maguta, bajaji, waenda kwa miguu, n.k. Mazingira ya sasa ya uwepo wa kivuko ni kwamba, mtumiaji wa kivuko anavushwa safari yenye umbali wa kati ya mita 800 hadi 1,000 za kivuko. Ebu tutazame economics za daraja, na kutazama opportunity cost kwa watembea kwa miguu, bajaji, maguta, mikokoteni n.k, kwa kuangalia matumizi kati ya Daraja na Kivuko cha ferry.

Leo hii, eneo kuu la shughuli za walio wengi (kiuchumi) kigamboni halipo mbali sana baada ya kuvuka n'gambo ya pili. Maeneo yenye shughuli nyingi ni yale ya pale mwanzoni, mpaka maeneo ya Mji Mwema kwa Mzee Jumbe. Kwa njia ya kivuko cha ferry, ili mmiliki wa Guta, Mkokoteni bajaji, pick up, n.k aweze kumvusha mteja wake kwa njia ya pantoni, ni lazima akabiliane na uhalisia ufuatao: Ni lazima ajiandae kuvusha chombo chake na mteja wake kwa umbali wa mita kati ya 800 &#8211; 1000 na kulipa hiyo 1,500, pamoja na gharama za mzigo, sh 500, pamoja na ya nauli atakayomtoza abiria/mteja wake, kumpelekea safari yake baada ya kivuko.

Ebu tuangalie mbadala wa Daraja. Katika mazingira haya, mmiliki wa bajaji au guta, au pick up, ni lazima akabiliane na uhalisia ufuatao: Ni lazima awe na mafuta (bajaji/pickup), au kifua (guta/baiskeli), ya kumvusha daraja lenye urefu wa kilometa sio chini ya saba (7) kutokea &#8216;take off' ya kurasini hadi &#8216;landing', ya Kibada. Akitua Kibada, itamlazimu kuendelea na safari tena kuelekea kwenye main business center (upande wa pili wa ferry). Hivyo, itamlazimu tena kuendelea na safari ya umbali wa kilometa sio chini ya kumi na nane (kutokea kibada hadi maeneo ya mji mwema/ferry). Kwahiyo ni dhahiri kwamba, kwa wastani, matumizi ya daraja yanamwongezea mtumiaji wa chombo cha usafiri umbali wa kilometa 25 au zaidi kufika ng'mabo ya pili, wakati mbadala wa kivuko cha ferry, umbali wake ni kama mita 800 hadi 1,000. Kwa hali hii, Je:

1. Moja, tofauti na umbali wa sasa wa mita kama 1,000 kwa pantoni, kipi nafuu? Nauli mpya ya kivuko au gharama za kupitia njia ya daraja (kilometa 25)? In other words: wamiliki wa maguta, Bajaji, Mikokoteni, Pick up, Lorry, na watembea kwa miguu, daladala n.k, mbadala upi ni nafuu kwao, in terms of gharama, Daraja (km 25) au kivuko chini ya nauli mpya?
2. Mbili, msafirishaji wa bidhaa za vyakula, na mnunuzi wa vyakula hivyo kule kigamboni, ana unafuu katika mazingira yepi in terms of gharama za vyakula? Usafiri wa kilometa 25 kupitia daraja au nauli mpya kupitia kivuko cha mita 800 &#8211; 1,000?
3. Na tatu, katika sababu zinazopelekea ongezeko la bei ya bidhaa za vyakula Kigamboni, suala la ferry peke yake linachangia asilimia ngapi? Factors zipi nyingine zinachangia bei ya bidhaa hizo?

Napenda kuyatolea majibu maswali haya, lakini naona majibu yapo wazi, hivyo nitakuwa napoteza muda.
Sasa niingine kwenye hoja ya pili ya Mh. Mnyika. Mnyika anasema kwamba hoja ya magufuli to justify ongezeko la nauli kigamboni, lisiige ongezeko la vivuko mikoani. Mnyika anasema, &#8216;vivuko nchini vinatofautiana gharama za uendeshaji, na pia umbali'. Huyu ni mtu yule yule ambae awali anasema kwamba, kivuko sio biashara bali huduma, ikiwa na maana anatambua kwamba shughuli ya kivuko haiwezekani kuendesheka bila ruzuku (kodi za wananchi) toka serikalini. Tuanze na hoja yake ya kwanza - tofauti za gharama za uendeshaji.

Ebu tuziangalie hizi gharama. Kwa ujumla wake, gharama za vivuko vyote ni pamoja na:

1. Mafuta ya Diesel
2. Mishahara kwa wafanyakazi
3. Matengenezo ya pantone/kivuko
4. Idadi ya masaa/muda wa kupatikana huduma

Ingawa katika ufafanuzi wa Mnyika, hakutoa takwimu kusindikiza hoja yake kuhusu tofauti ya gharama za vivuko nchini, common sense inatueleza kwamba kivuko cha kigamboni kina gharama kubwa zaidi kuliko vivuko vingi (kama sio vyote), kwa sababu kuu tano.

Kwanza, tofauti na vivuko vingi, Kigambani ina pantoni mbili.
Pili, kwa wastani, pantoni za kigamboni ni kubwa zaidi, hivyo kupelekea gharama za mafuta n.k, kuwa kubwa zaidi.
Tatu, kivuko cha kigamboni kina watumishi wengi zaidi, kwani askari peke yake pale, idadi yao inazidi 50.
Nne, pantoni za kigamboni zina mahitaji makubwa sana ya matengenezo ya mara kwa mara kuliko mengine yoyote kutokana na mileage covered, lakini pia mazingira ya pale. Kuliwahi tolewa taarifa jinsi gani uchafu uliokithiri maeneo yale unavyoharibu injini za pantoni. Tatizo hili huchangia sana huduma kusimama ili wazamiaji waweze kuingia kwenye injini kutoa nyavu za wavuvi, una pia chafu unaosukumwa na meli kubwa za nje zinazopita katika mkondo ule.
Tano, tofauti na vivuko vingine nchini ambavyo huduma zake uanza saa kumi na mbili asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni, kivuko cha kigamboni huduma zake ni masaa 24, na huduma ya masaa 24, iliendelea kwa muda mrefu chini ya nauli za zamani. Sasa tunajua vivuko hivi vinaendeshwa kwa hasara, na ndio maana ruzuku ya serikali ni muhimu. Kwahiyo, kitendo cha huduma kigamboni, kutolewa kwa masaa 24, kinapelekea huduma ile kuendeshwa kwa hasara kubwa zaidi, hivyo kuhitaji ruzuku zaidi kutoka serikalini. Tusisahau kwamba ruzuku, hizi ni hela za walipa kodi, na kwamba ruzuku ikipungua, ni ahueni kwa walipa kodi, hasa wale ambao katika maisha yao yote, hawajawahi kutumia kivuko kile. Haya ni baadhi ya masuala yanayopunguza nguvu hoja ya Mnyika kuhusu tofauti za gharama.

Tuangalie hoja ya pili ya Mnyika ya kupinga msimamo wa Magufuli kwamba nauli mikoani huwa zinapanda- pale ambapo Mnyika anaposema kwamba vivuko vinatofautiana umbali. Je, Mnyika ana takwimu gani juu ya tofauti kati ya umbali wa kivuko mfano cha Pangani na Umbali wa Kigamboni? Ebu tuangalie maana ya neno &#8216;distance" katika mazingira haya. Distance ni maelezo ya &#8216;kinyumerali' kuhusu umbali uliopo baina na vitu (objects). Na kuna namna kuu mbili za kuangalia &#8216;umbali'. Kwanza, ni distance travelled (mfano ferry kilometers per day), na pili, ni distance measured (mfano kilometa, maili, mita n.k). I am convinced kwamba Mh. Mnyika hakufikiria vizuri tofauti hizi, na hivyo kuja na conclusion kwamba, kwa vile kivuko cha kigamboni kina umbali wa kama mita 800 hadi 1,000, huku kile cha pangani kikiwa zaidi ya hapo, basi gharama za kuendesha kivuko cha pangani ni kubwa kuliko zile za kigamboni. Anachotakiwa kukiangalia Mnyika hapa sio umbali wa kutoka point A hadi B, bali ferry kilometers travelled in a day. Hakuna shaka kwamba kivuko cha kigamboni kinasafiri umbali mkubwa kuliko vivuko vingi (kama sio vyote), kutokana na idadi ya abiria waliopo inayopelekea huduma kuendeshwa masaa 24. Nitafafanua.

Kwanza, Takwimu zinasema kwamba watumiaji wa kivuko cha kigamboni ni karibia elf arobaini (40,000). Sina uhakika kama Mnyika anajua hili. Ebu tuangalie huko Pangani. Kwa mujibu wa takwimu juu za idadi ya watu, PANGANI kama moja ya wilaya zilizopo mkoani Tanga, ina jumla ya wakazi elfu arobaini na tatu (43,000). Ina maana kwamba Kivuko cha Kigamboni kinasafirisha idadi sawa na wakazi wa wilaya nzuma ya Pangani.

Ni muhimu kwa Mh Mnyika, na wabunge wengine, kuweka pembeni masuala ya siasa, au hoja za kutoshirikishwa katika maamuzi, na badala yake kujikita katika hoja iliyopo mbele yao. Ni muhimu waelewe facts zifuatazo:

1. Katika nchi yoyote ile, kivuko chini ya serikali huwa ni huduma na sio biashara. Mnyika kalielezea hili tayari.

2. Huduma ya kivuko cha namna hii, uendeshwa kwa hasara wakati wote, hivyo kuhitaji ruzuku ya serikali, ambazo ni fedha za walipa kodi.

3. Kivuko cha Kigamboni kinaendeshwa na hela za walipa kodi kama vilivyo vingine huko mikoani, lakini pamoja na hayo, nauli za kigamboni zilibakia katika bei moja kwa miaka 14, huku nauli katika vivuko vingine zikiongezeka kutokana na kupanda kwa gharama ya uendeshaji wa mafuta, matengenezo, n.k, gharama ambazo, wananchi wa DSM wamekuwa wanalipiwa kupitia ruzuku ya serikali kwa miaka 14.

4. Katika kipindi cha miaka 14 ambacho kivuko cha kigamboni kilikuwa hakijapandisha nauli (1996 &#8211; 2011), bei ya mafuta ya Diesel imeongezeka mara 4, kutoka sh. 500 kwa lita mwaka 1996, hadi sh. 2000 mwaka 2011.

5. Mwaka 1996 (kwa wastani), dollar moja ilinunuliwa kwa shilling 580, wakati kwa wastani, mwaka 2011, bei ilikuwa, shillingi 1,650. Ni dollar hii ndiyo inayotumika kuagizia mafuta ya Diesel kutoka nje kuendesha vivuko vya kigambani, pangani, lugolola, chato, kisyore, kirambo, utele, nyakarilo, chatobukombo, n.k.

6. Wastani wa bei ya mafuta katika soko la dunia mwaka 1996 ilikuwa $20.46 kwa pipa; Wastani, bei ya hiyo mwaka 2011 ilikuwa $87.48. katika kipindi hiki, nauli kigamboni hazikupanda.

7. Katika huduma za vivuko, waenda kwa miguu sio sehemu muhimu ya mapato, na ndio maana nchi nyingine huwa wanavuka bure. Mapato ya vivuko vyote duniani ni vyombo vya usafiri kama vile pikipiki, magari, bajaji, n.k, sio waenda kwa miguu, ndio maana mara nyingi, waenda kwa miguu hupita bure. Pia, katika economics za ferry, hakuna ubaguzi wa kuangalia pick up, lorry, basi, gari, au bajaji inavuka kwa malengo gani (biashara au kwenda kupunga upepo south beach), ndio maana hakuna price discrimination katika hilo, na badala yake, wote hulipa bei sawa. Lakini kwa sababu serikali haina uwezo mkubwa kifedha, iliamua kwa kipindi kirefu sana, kubakisha nauli kwa waenda kwa miguu kuwa sh. 100, ambayo ni kiwango kidogo sana.

8. Tusisahau kwamba pale Kigamboni &#8211; JWTZ na vifaa yao vyote, Polisi, Magereza, Wazee, Wanafunzi, na pia Watoto chini ya umri wa miaka 14, hawalipishwi nauli. Na kundi hili huwa kubwa sana pale kigamboni.

9. Na mwisho, pamoja na kwamba vivuko vingine vimekuwa vinatoza viwango tofauti huko mikoani, suala la msingi hapa ni kwamba &#8211; vivuko vyote vinaendeshwa kwa hasara, hivyo kulazimu ruzuku (kodi ya wananchi), kutoka serikalini, Kwahiyo sio politically correct kutetea ongezeko upande mmoja wa walipa kodi, na kupinga upande mwingine wa walipa kodi.

Je, wadau, kwa mtazamo wenu sasa, hoja za msingi za kina Mnyika na wenzake, ni ipi hasa:
1. Huduma za kivuko haziendani na ongezeko la nauli?
2. Nauli haziendani na ubora wa huduma?
3. Nauli haziendani na hali ya kiuchumi ya watumiaji wa kivuko kile?
4. Wabunge hawakushirikiskwa katika maamuzi, hivyo wamedharauliwa?
5. Magufuli kavunja sheria?
6. Mapato yanayopotea kwa siku yadhibitiwe ili nauli ibaki kuwa ile ile ya zamani badala ya hii mpya?

Nimalizie kwa kusema tu kwamba, kwenye suala la kivuko cha kigamboni, wapo watanzania wanaolipia kivuko kile kupitia ruzuku ya serikali kuu (inayotokana na kodi ya wananchi kwa serikali kuu), wakati wengi wa watanzania hawa hawakitumii, na pengine wengi zaidi hawatakitumia kivuko hiki katika maishayao yote. Hii sio sawa (hili ni suala la externalities), kwani kwa mtindo huu, ina maana kwamba hata wakulima wa huko Iringa, Mtwara, Singida n.k, wanatozwa fedha (kupitia kodi kwa serikali kuu), kuendesha kivuko cha kigamboni, ambacho hakina maslahi yoyote ya maana katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii, za kila siku.

Katika mazingira haya, Je, implication ya Msimamo wa Mnyika kusitisha zoezo la ongezeko ya nauli ni nini?

NI GHARAMA ZISIZO NA MAANA KWA MLIPA KODI KIJIJINI. Kuchelewesha ongezeko la nauli kama anavyotaka Mnyika, ni kuwagharimu wakulima vijijini zaidi, kwani kama tulivyokwisha ona, the more serikali inatoa ruzuku, the more wakulima wanahenya kuendesha kitu wasicho na faida nacho, moja kwa moja. Vinginevyo, Mnyika kukubali nauli mpya ziwe effective, maana yake ni kwamba, sasa itapelekea serikali kupunguza ruzuku (hivyo mzigo wa walipa kodi), na badala yake, &#8216;actual users' wa kivuko kile (hawa wakazi 40,000) ndio wawe na jukumu kubwa zaidi la kukiendesha kivuko kile. Ni muhimu kwa Mh Mnyika na wenzake kuelewa hii "Trade-Off", baina ya kusitisha nauli mpya, na ile ya kukubali viwango vipya, kwani, wanaweza kudhania kwamba wanapunguza maumivu upande mmoja, bila ya kujua kwamba kumbe wanazidisha maumivu upande mwingine, tena ule unaoishi katika mazingira ya umaskini uliokithiri kupita ya mjini (wakulima vijijini). Na hii ni moja ya sababu kubwa kwanini nasema kwamba, katika sakata hili, Mh Mnyika na wenzake wanapwaya katika vigezo vile juu ya kiongozi bora, nilivyo viainisha awali.

Vinginevyo, ni dhahiri kwamba, binadamu wote tuna mapungufu, lakini kwa nafasi zenu za uongozi, suala la kuwa makini zaidi, kabla ya kutoa msimamo mbele ya umma, mara nyingi husaidia sana. Matumizi ya kanuni kama vile "Process of Elimination", ni moja ya njia zinazosaidia sana katika hilo.


 
halafu ndugu mchambuzi, kwa nini ulifanya ceteris peribus ukabakia na nauli ya binadamu tu? Kwenye uzi wako kuna 100, 200 na 300 tu. Kwa kuacha variables nyingine (guta, bajaji, gari n.k.) unadhani hoja yako sahihi?

Niliamua to hold suala la watembea kwa miguu constant kwasababu - mapato ya kivuko chochote duniani ni magari, pikipiki n.k, sio watembea kwa miguu. Katika nchi zote, gharama za watembea kwa miguu zinabebwa na wenye magari, pikipiki, n.k, pamoja na ruzuku ya serikali. Ndio maana mara nyingi (sio zote), watembea kwa miguu huwa hawalipishwi nauli. Lakini kwa mazingira ya Tanzania, ilibidi serikali itoze nauli, japo kidogo, kwa kiwango ambacho kilibakia chini sana kwa miaka 14. Na kusema ukweli, ongezeko jipya la Sh. 200 (ingawa ni by 100%), bado ni dogo sana, kwani, pamoja na ukweli kwamba serikali haina pesa za kuendesha kivuko kile kwa ufanisi, bado wapita kwa miguu wanatozwa bei karibia na ya bure. Isitoshe, kuna sehemu ya wananchi hawalipi kabisa, mfano askari wa aina zote pamoja na magari yao na vifaa vyao, watoto chini ya umri wa miaka 14, wazee, wanafunzi, etc, na hawa ni wengi sana katika kivuko kile.

Hizo ndizo sababu kwanini niliamua kujadili suala la watembea kwa miguu independently kwanza, kabla ya kuangalia suala la bajaji, magari, maguta n.k, ambayo ongezeko la nauli haliwezi kwepeka. Nimetoa ufafanuzi zaidi katika majibu yangu kwa Mh. Mnyika hapo juu.
 
Mkuu Mchambuzi, ufafanuzi wako unaleta maana zaidi ya porojo.
Bajaji mpya hutumia lita moja kwa kilometa 35.
0.7 litres kwa kilomita 25.Ambayo ni sawa na shs 1400$ kwa bei ya sasa ya mafuta.
Bajaji kama siyo mpya inaweza kutumia lita moja ya petroli kwa umbali huo.
Kwa hiyo, wakazi wa kigamboni watakaotumia bajaji kwenda mjini, watatumia karibu shilingi 2000 kuvuka ng'ambo ya pili.
Kwa hivyo hiyo 1300 hata daraja likjengwa, ndiyo itakuwa gharama ya bajaji kwenda ng'ambo ya pili.

 
Mnyika amewapotosha wananchi kwa kuwafanya waamini kuwa kuna mbadala sawa wa kivuko na daraja. Kuwa sehemu ile ile iliyopo kivuko, basi inaweza kuendelezwa kwa kuwekwa daraja na hivyo masafa yanayovukwa kwa kivuko ndio hayo hayo yatakayovukwa kwa daraja

Alipaswa aelewe mapema na azingatie kuwa technically hilo haliwezekani hususan kwenye eneo ambalo tayari limeshaendelezwa kama Kigamboni/Magogoni
 
Mkuu Mchambuzi, ufafanuzi wako unaleta maana zaidi ya porojo.
Bajaji mpya hutumia lita moja kwa kilometa 35.
0.7 litres kwa kilomita 25.Ambayo ni sawa na shs 1400$ kwa bei ya sasa ya mafuta.
Bajaji kama siyo mpya inaweza kutumia lita moja ya petroli kwa umbali huo.
Kwa hiyo, wakazi wa kigamboni watakaotumia bajaji kwenda mjini, watatumia karibu shilingi 2000 kuvuka ng'ambo ya pili.
Kwa hivyo hiyo 1300 hata daraja likjengwa, ndiyo itakuwa gharama ya bajaji kwenda ng'ambo ya pili.


Soby,

Nashukuru sana kwa takwimu hizi, kwani zilinisumbua kidogo, nikaamua kuachana nazo wa sasa. Imesaidia sana kujaza flesh kwenye majibu yangu kwa Mh. Mnyika. Na pia mzunguko wa hilo Daraja kwenye picha, ni dhahiri mpaka waje kufika n'gambo ya pili, lazima uwaache hoi wamiliki wa maguta, baiskeli, n.k., tofauti na mbadala wa kivuko ambao ni cheaper na mfupi zaidi i.e. efficient kwa mtumiaji by all means.

Lakini kwa vile wahusika pamoja na wote wanaowaunga mkono ni wanasiasa (na sio viongozi), ni dhahiri watarudi humu na majibu ya kisiasa, ya kupindisha pindisha mambo, na ya kutokubali ukweli kwamba kuna masuala waliya 'over look', ili mradi msimamo uwe msimamo.
 
Mnyika amewapotosha wananchi kwa kuwafanya waamini kuwa kuna mbadala sawa wa kivuko na daraja. Kuwa sehemu ile ile iliyopo kivuko, basi inaweza kuendelezwa kwa kuwekwa daraja na hivyo masafa yanayovukwa kwa kivuko ndio hayo hayo yatakayovukwa kwa daraja

Alipaswa aelewe mapema na azingatie kuwa technically hilo haliwezekani hususan kwenye eneo ambalo tayari limeshaendelezwa kama Kigamboni/Magogoni

Upo sahihi. Nadhani watu wengi wanapotoshwa au jipotosha kwa kuwa na mtazamo huo.
 
Muulizeni Mh Mnyika msimamo wa chama chake juu ya sakata hili. Tumemsikia Mwenyekiti wa CCM-Dar, kijana wa ENL, akimshukia Maghufuli!

Ni dhahiri utakuwa wa kisiasa zaidi kama ulivyokuwa wa Mwenyekiti Guninita.
 
umetumwa na mafisadi kaka maana gazeti lao la uhuru kila siku linamwandika magufuli,mnyika mtu makini sana,hawezi kukurupuka hata dk.slaa ulimsikia tushughurikie matatizo ya wananchi kwanza.unaonekana huna huruma na watanzania wenzako unajali siasa kuliko matatizo ya tanzania.over
 
umetumwa na mafisadi kaka maana gazeti lao la uhuru kila siku linamwandika magufuli,mnyika mtu makini sana,hawezi kukurupuka hata dk.slaa ulimsikia tushughurikie matatizo ya wananchi kwanza.unaonekana huna huruma na watanzania wenzako unajali siasa kuliko matatizo ya tanzania.over
Hutaki daraja? Kama unataka, 2015 itabidi kilomita 7 mpaka mjini.... sawa na Temeke-posta. Mia tatu.
 
Hutaki daraja? Kama unataka, 2015 itabidi kilomita 7 mpaka mjini.... sawa na Temeke-posta. Mia tatu.

Na hizo kilometa 7 ni kama anakaa at landing point ya daraja pale kibada, vinginevyo kama amejenga maeneo ya mji mwema, au mbele zaidi kurudi kule mwalimu nyerere memorial, jumla ya umbali ni kilometa si chini ya 25 kutoka Dar-es-salaam. Nauli ya mia tatu haitatosha.

Sielewi kwanini watu wanaliweka suala hili kisiasa zaidi wakati ni common sense. Lakini ni hao hao wanalalamikaga kwamba tatizo la nchi yetu ni kwamba viongozi wanaendesha mambo kisiasa zaidi.
 
kwa hili jawabu lako maana yake ni kwamba wenye haki ya kukaa mjini ni wenye hela tu, siyo?

Ibara ya 17 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi:
["Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi, na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa katika Jamhuri ya Muungano."]

Swali la msingi hapa ni, Je, haki hii inalindwa vipi na Katiba?
 
Back
Top Bottom